25-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Markaz Kununua Chakula Cha Zakaatul-Fitwr Mapema Ili Kuwuazia Waislamu
Markaz Za Kiislamu Kununua Chakula Cha Zakaatul-Fitwr Mapema Ili Kuwuazia Waislamu
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Markazi za Kiislamu nchi za Magharibi inataka kununua vyakula kama mchele, mapema sana kabla ya 'Iyd tuseme siku kumi kabla. Kisha watatangaza kuwa wako tayari kupokea pesa za Zakaatul-Fitwr kutoka kwa Waislamu ili wazigawe kwa ajili yao. Hii ni kwa sababu haiwezekani kununua kiasi ya chakula wakipokea pesa siku mbli kabla ya 'Iyd. Nini Hukmu Yake?
JIBU:
Hakuna ubaya kwa Markazi kununua chakula mapema kisha kuwauzia wanaotaka kununua Zakaatul-Fitwr kisha kuigawa kabla ya wakati wake.
[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn [Fataawaa (71475)]