17-Uswuul Al-Fiqhi: Watu Wa Rai Na Watu Wa Hadiyth: Ahl Al-Hadiyth Na Ahl Ar-Ra-ay
WATU WA RAI
AHL AL-HADIYTH
Huenda ukweli huu ukaja kuwa makini zaidi pale tutakapotaja chimbuko la fikra mbili za kisheria yasiyokuwa rasmi; watu wa Rai au Ahl ar-Ra-ay, na wale wa Hadiyth au Ahl al-Hadiyth, na kutokea kwa tofauti baina
Waandishi wa Historia ya Sheria ya Kiislamu, wanasisitiza kwamba watu wa fikra za Rai, wa Ahl ar-Ra-ay ilikuwa ni kupanuka kwa elimu iliyotolewa na ‘Umar na ‘Abdullaah bin Mas’uud ambao miongoni mwao Swahaabah, walikuwa na upana wa kupanga katika matumizi
Wanahistoria hao hao wanafafanua kwamba, hao watu wa Hadiyth wa Ahl al-Hadiyth ilikuwa ni mfululizo wa elimu za hao Swahaabah ambao khofu zao za kuchanganya barua za vyanzo vya maandiko (Nuswuus) ziliwafanya kuwa na hadhari kwa kila upande, hadi kufikia ambapo walikuwa hawawezi kwenda mbali zaidi ya maandiko. Hili lilikuwa ni, na kwa urefu, kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar bin al-Khattwaab, ‘Abdullaah bin ‘Amr bin al-‘Aas, az-Zubayr, na ‘Abdullaah bin ‘Abbaas.
Fikra za Ahl al-Hadiyth zilikuja kuenea zaidi sehemu za Hijaaz kwa sababu zilizo nyingi, na iliyo muhimu mno ilikuwa ni idadi kubwa ya Hadiyth na simulizi nyengine zilizojulikana na watu wa eneo hilo, na ukweli ni kwamba, Wilaya hiyo ilikuwa ni imara zaidi baada ya kiti cha Khilaafah kilipoondoshwa na shughuli nyingi za kisiasa zilipohamishwa, kwanza ni Damascus, baadaye Baghdaad. Imaam wa Madiynah, Sa’iyd bin al-Musayyab (amefariki mwaka 94 H), aliwahi kusimulia kwamba watu wa Makkah na Madiynah hawakupoteza Hadiyth na Fiqh nyingi, kwa sababu walikuwa wazoefu katika Fataawa na masimulizi ya Abuu Bakr, ‘Umar, ‘Uthmaan, ‘Aliy (kabla ya kuwa Khaliyfah), ‘Aaishah, Ibn ‘Abbaas, Ibn ‘Umar, Zayd bin Thaabit na Abuu Hurayrah, na hivyo hawakuona haja ya kutumia Ra-ay kwa lengo la kupata sheria.
Fikra za Ahl ar-Ra-ay, kwa upande mwengine, zilipata sifa nchini
Kuenea kwa utaratibu huu nchini
Pale mapote,
Kwa hivyo, ilikuwa kwa njia hii ambapo ‘Ummah uligawika, kwa wale wasiojihusisha na aidha Shi’ah au Khawaarij, kwenye makundi mawili, Ahl al-Hadiyth na Ahl ar-Ra-ay, na mgongano baina
Hivyo, Ahl ar-Ra-ay kawaida wakiwatoa makosa Ahl al-Hadiyth kwa kuwa na kiwango kidogo cha umakini na uchache wa ufahamu wa Fiqhi, ingawa Ahl al-Hadiyth walidai kwamba mawazo ya Ahl ar-Ra-ay hayakuegemezwa zaidi ila kwenye kubahatisha tu; na kwamba wamejitenga wenyewe kwa kutokuwa na hadhari inayohitajika katika masuala ya Dini yenye umuhimu, ambayo yanaweza tu kuhakikishwa kupitia msaada wa vyanzo vya maandiko.
Hakika, Ahl ar-Ra-ay walikubaliana na Waislamu wote kwamba pale mtu atakapofahamu Sunnah, hatoikataa. Kwa sababu si zaidi ila ni mawazo ya mtu fulani. Udhuru wao kwenye kesi zote hizo ambazo wamelaumiwa kwa kuchanganya Sunnah, si chochote ila kwamba hawakutambua Hadiyth yoyote kuhusiana na suala linalobishaniwa, au kwamba walitambua Hadiyth lakini hawakuikubali kuwa ni yenye maana kwa sifa ya udhaifu kwa wasimuliaji au kasoro nyengine waliyoiona (kasoro ambayo pengine wengine hawakuiona kuwa yenye kuharibu), au kwamba walitambua Hadiyth nyengine ambayo wao waliitambua kuwa yenye maana na ambayo ilipingana na kusudio la sheria ya Hadiyth inayokubalika na wengine.
Juu ya yote hayo, Ahl al-Hadiyth walikubaliana na Ahl ar-Ra-ay katika dharura ya kuwa na msaada wa hoja wakati wowote suala linapotokezea ambapo hakuna maamuzi maalum kwenye vyanzo vya maandiko. Lakini bado, juu ya sehemu hizi za makubaliano, mgogoro na mvutano baina ya makundi haya ulibaki kuwa mkali.
[1] Kwa vile kila dhehebu lilipigana kumzidi mwengine, na kupata wartadi kutoka katika Uislamu, waliamua kuziharibu maana za maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)