Keki Ya Jibini Ya Matunda Ya Peach
Keki Ya Jibini Ya Matunda Ya Peach
Vipimo
Malai ya jibini (cream cheese) - 2 Pakiti za 450g
Sukari - ½ Kikombe cha chai
Mayai - 2
Unga wa ngano - 1 Kijiko cha chai
Mtindi (yogurt) - ½ Kikombe cha chai
Ukoko wa tayari (ready crust) - 2
Matunda ya Peach ya kopo - 1
Unga wa kastadi - 1 Kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Washa oveni moto wa 350°F.
- Katika bakuli la mashine, changanya vizuri malai ya jibini, sukari, mtindi na halafu kijiko cha unga.
- Kisha tia mayai na uendele kuchanganya.
- Halafu mimina juu ya ule ukoko (crust) na utandaze vizuri hadi pembeni.
- Vumbika (bake) kwenye oveni kwa muda wa dakika 15, Kisha badilisha moto kwa kuweka 300°F na uendele kuchoma kwa muda wa saa moja.
- Ikishaiva iache ipoe na huku tayarisha sosi yake.
- Katika sufuria, tia juisi ya peach utakayoitoa kwenye kopo pamoja na kastadi na uweke moto mdogo huku unakoroga mpaka iwe nzito kiasi.
- Kisha mimina juu ya ile jibini iliyopoa na upange peach kwa mpango mzuri.
- Iweke kwenye firiji ipate ubaridi na kisha itakuwa tayari kwa kuliwa - kata vipande upendavyo.