Kusoma Baadhi Ya Suwrah Kwa Nia Ya Kuomba Haja Inajuzu?
Kusoma Baadhi Ya Suwrah Kwa Nia Ya Kuomba Haja Inajuzu?
SWALI:
katika baadi ya majibu zenu kumjibu alouliza kuhusu matumizi ya surah yaasiin mukamjibu kua kuna watu wansoma yasin wakisema yaasin inawapawanacho kitaka jee wako watu kama hao na kwani ni yaasiin peke yake sura zinginepia ukisoma na niya kama hiyo sinishirk pia?
kisha natakakujua masala hayo ni ya kifiqhi aw yakiaqidah
JIBU:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako. Jambo hili ni muhimu katika maisha ya Muislamu ambaye anafaa awe na mahusiano mema na Muumba wake. Suala la du’aa ni suala la 'Aqiydah kwani yapo mafungamano ya karibu na Allaah Aliyetukuka.
Kwa kuwa ni hivyo sisi hatutakuwa na uwezo wa kusoma Suwrah au Aayah fulani kwa nia ya kuomba du’aa ila Suwrah na Aayah hizo ziwe zimeelezwa kwetu na ima Allaah Aliyetukuka au Nabiy Wake. Mbali na hayo itakuwa sisi tuwe ni wenye kujikuribisha kwa Allaah Aliyetukuka kwa kusoma Qur-aan na hivyo itakuwa ni kwa kusoma Suwrah yoyote ile.
Ama kwa hakika yale ambayo yametufikia sisi ni kuwa Allaah Aliyetukuka Anatufahamisha:
"Na Allaah ana Majina mazuri basi muombeni kupitia kwayo".
Na Allaah Anajua zaidi