11-Hadiyth Al-Qudsiy: Watu Wa Mwanzo Kuulizwa Qiyaamah: Shahidi, ‘Aalim Na Mtoaji Mali

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 11

Watu Wa Mwanzo Kuulizwa Qiyaamah: Shahidi, ‘Aalim Na Mtoaji Mali

  

عَنْ أبي هريرة رضي الله عنه قال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهم عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ ((إِنَّ أَوَّلَ النَّاسِ يُقْضَى يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَيْهِ رَجُلٌ اسْتُشْهِدَ فَأُتِيَ بِهِ فَعَرَّفَهُ نِعَمَهُ فَعَرَفَهَا قَالَ: فَمَا عَمِلْتَ فِيهَا؟ قَالَ: قَاتَلْتُ فِيكَ حَتَّى اسْتُشْهِدْتُ، قَالَ: كَذَبْتَ وَلَكِنَّكَ قَاتَلْتَ لِأَنْ يُقَالَ جَرِيءٌ فَقَدْ قِيلَ ثُمَّ أُمِرَ بِهِ فَسُحِبَ عَلَى وَجْهِهِ حَتَّى أُلْقِيَ فِي النَّارِ، وَرَجُلٌ تَعَلَّمَ الْعِلْمَ وَعَلَّمَهُ وَقَرَأَ الْقُرْآنَ فَأُتِيَ بِهِ فَعَرَّفَهُ نِعَمَهُ فَعَرَفَهَا قَالَ: فَمَا عَمِلْتَ فِيهَا؟ قَالَ: تَعَلَّمْتُ الْعِلْمَ وَعَلَّمْتُهُ وَقَرَأْتُ فِيكَ الْقُرْآنَ، قَالَ: كَذَبْتَ وَلَكِنَّكَ تَعَلَّمْتَ الْعِلْمَ لِيُقَالَ عَالِمٌ وَقَرَأْتَ الْقُرْآنَ لِيُقَالَ هُوَ قَارِئٌ فَقَدْ قِيلَ ثُمَّ أُمِرَ بِهِ فَسُحِبَ عَلَى وَجْهِهِ حَتَّى أُلْقِيَ فِي النَّارِ، وَرَجُلٌ وَسَّعَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَأَعْطَاهُ مِنْ أَصْنَافِ الْمَالِ كُلِّهِ فَأُتِيَ بِهِ فَعَرَّفَهُ نِعَمَهُ فَعَرَفَهَا قَالَ: فَمَا عَمِلْتَ فِيهَا؟ قَالَ: مَا تَرَكْتُ مِنْ سَبِيلٍ تُحِبُّ أَنْ يُنْفَقَ فِيهَا إِلَّا أَنْفَقْتُ فِيهَا لَكَ قَالَ كَذَبْتَ وَلَكِنَّكَ فَعَلْتَ لِيُقَالَ هُوَ جَوَادٌ فَقَدْ قِيلَ ثُمَّ أُمِرَ بِهِ فَـسُحِبَ عَـلَى وَجْهِهِ ثُمَّ أُلْقِيَ فِي النَّارِ ))

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi sallam) akisema: ((Wa mwanzo kuhesabiwa Siku ya Qiyaamah ni mtu aliyekufa shahidi katika vita, ataletwa na kujulishwa neema alizoneemeshwa na baada ya kuzijua ataulizwa (na Allaah): “Umezifanyia kazi gani neema hizi?” Atasema: “Nimepigana jihaad kwa ajili Yako mpaka nikafa shahidi.” Ataambiwa: “Umesema uongo, bali ulipigana ili isemwe kuwa wewe ni jasiri na imeshasemwa.” Kisha itaamrishwa abururwe kwa uso wake na kuingizwa Motoni. Na mtu (mwengine) 'Aalim aliyejifundisha Dini akaijua vizuri, akasoma na Qur-aan, ataletwa na kujulishwa neema alizoneemeshwa, kisha ataulizwa; “Umezifanyia kazi gani neema hizi?” Atasema: “Nimejifunza elimu nikafundisha na kwa ajili Yako nikasoma Qur-aan.” Ataambiwa: “Umesema uongo, bali ulijifunza elimu ili isemwe kuwa wewe ni ‘Aalim. Ukasoma Qur-aan ili isemwe kuwa wewe ni msomaji (mzuri), na imeshasemwa.” Kisha itaamrishwa abururwe kwa uso wake na kuingizwa Motoni. Na mtu (mwengine) Allaah Amempa wasaa, akampa kila aina ya mali, ataletwa na kujulishwa juu ya neema alizoneemeshwa, kisha ataulizwa: “Umezifanyia kazi gani neema hizi?” Atasema: “Sijaacha njia Unayopenda mtu atoe katika mali yake ila mimi nimetoa kwa ajili Yako.” Ataambiwa: “Umesema uongo, bali umetoa ili isemwe kuwa wewe ni mkarimu na imeshasemwa. Kisha itaamrishwa abururwe kwa uso wake na kuingizwa Motoni”. [Muslim] 

 

 

Share