15-Hadiyth Al-Qudsiy: Suwratul Faatihah - Nimeigawa Swalaah Baina Yangu Na Mja Wangu Nusu Mbili
Hadiyth Al-Qudsiy
Hadiyth Ya 15
Suwratul Faatihah - Nimeigawa Swalaah Baina Yangu Na Mja Wangu Nusu Mbili
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَنْ صَلَّى صَلَاةً لَمْ يَقْرَأْ فِيهَا بِأُمِّ الْقُرْآنِ فَهِيَ خِدَاجٌ)) ثَلَاثًا غَيْرُ تَمَامٍ فَقِيلَ لِأَبِي هُرَيْرَةَ إِنَّا نَكُونُ وَرَاءَ الْإِمَامِ فَقَالَ اقْرَأْ بِهَا فِي نَفْسِكَ فَإِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((قَالَ اللَّهُ تَعَالَى قَسَمْتُ الصَّلَاةَ بَيْنِي وَبَيْنَ عَبْدِي نِصْفَيْنِ وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ فَإِذَا قَالَ الْعَبْدُ (الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ) قَالَ اللَّهُ تَعَالَى حَمِدَنِي عَبْدِي وَإِذَا قَالَ (الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ) قَالَ اللَّهُ تَعَالَى أَثْنَى عَلَيَّ عَبْدِي وَإِذَا قَالَ (مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ) قَالَ مَجَّدَنِي عَبْدِي وَقَالَ مَرَّةً فَوَّضَ إِلَيَّ عَبْدِي فَإِذَا قَالَ (إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ) قَالَ هَذَا بَيْنِي وَبَيْنَ عَبْدِي وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ)) مسلم, مالك, الترمذي, أبو داود, النسائي وابن ماجه
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeswali Swalaah bila ya kusoma humo mama wa Qur-aan (Suwratu Al-Faatihah) huwa haikutimia (ina kasoro) [na alikariri mara tatu] haikutimia. Mtu mmoja alimwambia Abuu Hurayrah: (Hata) tukiwa nyuma ya Imaam? Akasema: Isome mwenyewe (kimya kimya) kwani nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Allaah Ta’aalaa Amesema: Nimeigawa Swalah baina Yangu na mja Wangu nusu mbili, mja Wangu atapata yale aliyoyaomba. Mja anaposema (Himidi zote Anastahiki Allaah) Rabb (Mola) wa walimwengu). Allaah Ta’aalaa Husema: Mja Wangu kanihimidi (kanisifu). Na anaposema (Mwingi wa Rahmah – Mwenye kurehemu). Allaah Ta’aalaa Husema: Mja wangu kanitukuza, na anaposema (Mfalme wa siku ya malipo). Allaah Ta’aalaa Husema: Mja wangu kanipa heshima. Na mara moja alisema: Mja wangu kazikubali nguvu Zangu. Na anaposema (Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada) Husema: Hii ni baina Yangu na mja Wangu na mja Wangu atapata kile alichokiomba. Na anaposema: (Tuongoze njia iliyonyooka. Njia ya wale Uliowaneemesha, sio ya walioghadhibikiwa wala waliopotea). Husema: Hii ni ya mja Wangu na mja Wangu atapata kile alichokiomba)) [Muslim, Maalik, At-Tirmidhiy, Abu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]