35-Hadiyth Al-Qudsiy: Mtu Aliyewausia Wanawe Wamuunguze Baada Ya Kufariki Kwa kukhofu Adhabu Ya Allaah
Hadiyth Al-Qudsiy
Hadiyth Ya 35
Mtu Aliyewausia Wanawe Wamuunguze Baada Ya Kufariki Kwa kukhofu Adhabu Ya Allaah
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((كَانَ رَجُلٌ يُسْرِفُ عَلَى نَفْسِهِ فَلَمَّا حَضَرَهُ الْمَوْتُ قَالَ لِبَنِيهِ: إِذَا أَنَا مُتُّ فَأَحْرِقُونِي ثُمَّ اطْحَنُونِي، ثُمَّ ذَرُّونِي فِي الرِّيحِ، فَوَاللَّهِ لَئِنْ قَدَرَ عَلَيَّ رَبِّي لَيُعَذِّبَنِّي عَذَابًا مَا عَذَّبَهُ أَحَدًا. فَلَمَّا مَاتَ فُعِلَ بِهِ ذَلِكَ، فَأَمَرَ اللَّهُ الْأَرْضَ فَقَالَ: اجْمَعِي مَا فِيكِ مِنْهُ فَفَعَلَتْ، فَإِذَا هُوَ قَائِمٌ، فَقَال:َ مَا حَمَلَكَ عَلَى مَا صَنَعْتَ؟ قَالَ: يَا رَبِّ خَشْيَتُكَ. فَغَفَرَ لَهُ)) البخاري، مسلم، النسائي و ابن ماجه
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mtu alifanya maasi makubwa na wakati mauti yalipomfikia aliwausia wanawe akiwaambia: Nitapokufa, nichomeni, munisage na mulitawanye jivu langu baharini kwani, wa-Allaahi, Allaah Atakaponipata, Ataniadhibu adhabu ambayo hajapata kuadhibiwa mtu mwingine. (Wanawe) walifanya walivyousiwa. Kisha Allaah Aliiamrisha ardhi kwamba: “Toa kile ulichokichukua.” Mara hapo akasima. (Allaah) Akamuambia: Kitu gani kilichokufanya ufanye hayo uliyofanya? (Yule mtu) akasema: Yaa Rabb wangu! Ni kukukhofu Wewe. Basi Allaah Akamghufuria)) [Al-Bukhaariy, Muslim, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]