Kashata Za Njugu-Karanga
Kashata Za Njugu-Karanga
Vipimo:
Karanga - Kilo
Sukari - 5 vikombe
Maji - 2 vikombe
Maziwa ya unga - 2 vijiko vya chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
- Saga karanga zilizokaangwa na kumenywa mpaka zilainike kiasi.
- Kisha changanya maji na sukari weka jikoni yachemke mpaka yanate kidogo kama shira. Changanya unga wa karanga na maziwa ya unga kisha mimina kwenye hiyo shira.
- Koroga taratibu kwa moto mdogo mpaka uone imeshikana na inanata.
- Paka mafuta treya kisha mimina na utandaze upesi upesi.
- Acha ipoe kidogo tu kisha katakata vipande na acha ipoe kabisa.
- Panga kwenye sahani tayari kwa kuliwa pamoja na kahawa.
Kidokezo:
Kama maziwa ya unga huna si lazima.