Crapes Za Blue Berries na Asali
Crapes Za Blue Berries na Asali
Vipimo
Unga - 2 vikombe
Baking Powder - 2 vijiko vya chai
Sukari - ½ kikombe
Yai - 1
Maziwa - 1 ¼ kikombe
Maziwa ya mvuke (evaporated milk) - ¾ kikombe
Siagi - 1 Kijiko cha supu
Mjazo
Blue berries
Asali
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Tia unga, baking powder na sukari katika bakuli.
- Weka yai, maziwa yote na siagi katika bakuli jengine na upige kwa wiski (whisk – mwiko wa kupigia mayai) hadi ichanganyike, kisha changanya katika unga na endelea kupiga kwa wiski hadi uchanganyike vizuri na uwe nyororo.
- Weka motoni kikaango kisichoganda (non-stick frying pan), moto baina ya mdogo na wastani.
- Chota kwa mwiko kiasi nusu 1/3 kikombe (au takriban ½ kikombe) mimina katika kikaango.
- Subiri itoe viputo (bubbles) kisha geuza upike upande wa pili. Pande zote ziive kugeuka rangi ya dhahabu.
- Epua weka kando huku ukimaliza kupika mikate mingine.
- Panga katika sahani na kila juu ya mkate tia blue berries na asali, panga nyigninezo juu yake hivyo hivyo kiasi utakavyotaka kuhudumia.
Kidokezo:
- Unaweza kutumia matunda mengine.
- Kipimo Cha kiasi crapes 15