Chapati -2
Chapati -2
Vipimo
Unga wa ngano mweupe - 1 Kilo
Samli - 150gm
Chumvi - 3 vya chai
Maji ya moto yasichemke lakini - Kiasi
Mafuta Ya Zaituni (olive oil)- 4 vijiko vya supu
Samli tena - 200 gms
Iliki iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Tia unga kwenye sinia au bakuli kubwa lilo na nafasi, changanya na chumvi, mafuta ya zaituni, samli 150g, iliki, mimina maji ya moto kwa kipimo cha kikombe kila unapovuruga unga.
- Uunga uwe mwepesi unapoganda kuwa donge moja kubwa. Uwache kwa muda wa dakika 60 (saa moja hivi) ukiwa umeufinika ili unga ulainike.
- Katakata madonge makubwa yenye ukubwa wa chungwa ili uweze kutoa kila donge chapati mbili. Ukimaliza hapa weka madonge kwa muda wa nusu saa ukiwa umefinika bila ya kuingia upepo ndani.
- Sukuma donge ukiwa umelimwagia unga mkavu juu, liwe mviringo. Unaweza kutumia kifimbo hata chupa kusukumia madonge ikiwa huna kifimbo juu ya meza au kwenye kibao maalumu cha chapati.
- Yayusha samli nyingine ya 200gm kisha itumie kwa kupaka kwenye kila donge ukilisukuma duara itakayobakia weka kando utachomea chapatti.
- Likate katikati kwa kidole chako au kijiko upate mgawanyo wa sehemu mbili sasa kila sehemu utakunja kwanzia ncha moja hadi ikutane na ncha nyengine kama mkeka, donge lake linakuwa na sampuli, huuitwa tabaki mkunjo huu kama ilivyo katika picha.
- Weka chuma cha kuchomea chapati jikoni moto mdogomdogo.
- Sukuma kila donge kisha mara nyengine mviringo huu utakuwa mviringo wa kuchoma weka chapati kwenye chuma kavu bila samli iache muda wa dakika tatu igeuze upande mwengine kisha vilevile , ukiona ina mabapa ya kuchomeka tia samli ile uloyeyusha kwa kijiko kikubwa kimoja huku unaizungusha zungusha.
- Geuza upande wa pili vile vile mpaka iwive.
- Zipange kwenye sahani huku unazifinika, hapa tayari kuliwa kwa mchuzi au mboga yoyote.
Kidokezo:
Ukipenda kuzichambua kidogo chapati baada ya kumaliza hii unazishika zote kwa pamoja ikiwa umezikunja, unakunja ngumi au kifimbo kupiga tu mara moja tosha.