Keki Ya Chokoleti Iliyokoza
Keki Ya Chokoleti Iliyokoza
Vipimo
Maji yaliyochemka - 2 Vikombe vya chai
Unga wa kaukau (cocoa powder) - 1 Kikombe
Unga - 2 ¾ Vikombe
Baking soda - 2 Vijiko vya chai
Baking powder - ½ Kijiko cha chai
Chumvi - ½ Kijiko cha chai
Siagi iliyolainika - 1 Kikombe
Sukari - 2 ¼ Vikombe
Mayai - 4
Vanilla - 1 ½ Kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Washa oveni moto wa 350° F. Kisha paka siagi/mafuta treya ya kuchomea keki.
- Katika bakuli la kiasi, mimina yale maji ya moto yaliyochemka juu ya unga wa kaukau (cocoa powder), na uchanganye (kwa whisking spoon) hadi ilainike, kisha iyache ipoe.
- Kwenye bakuli la kiasi, chunga pamoja unga, baking soda, baking powder na chumvi na uweke kando.
- Katika bakuli la mashine, changanya (cream) siagi na sukari pamoja mpaka ilainike vizuri.
- Kisha tia yai moja baada ya jengine huku unaendelea kuchanganya, halafu tia vanilla, kisha tia mchanganyiko wa unga halafu tia ule mchanganyiko wa kaukau ulouweka kando.
- Mimina kwenye treya ya kuchomea keki na uvumbike (bake) kwenye oveni kwa muda wa dakika 25 – 30.
- Iache ipoe halafu itayarishie malai ya chokoleti (cream chocolate).
Vipimo Vya Malai Ya Chokoleti (cream chocolate)
Siagi - ¼ Kikombe
Sukari laini (icing sugar) - 1 Kikombe
Unga wa kaukau (cocoa powder) - 1 Kijiko cha supu
Maji ya moto - 2 Vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha
- Katika bakuli la mashine, changanya vipimo vyote hadi ilainike vizuri. Unaweza kuongeza maji ikiwa mchanganyiko ni mzito sana.
- Kisha unapaka juu ya keki iliyopoa kwa kutumia kisu cha siagi au mwiko uliobapa (flat).
- Kisha tia mchanganyiko wa malai ya sukari kiasi katika mirija/nozeli (icing tube/icing nozzle) ili itoe usanifu (design) juu ya keki kama ilivo kwenye picha hapo juu au upendavyo. Kata vipande saizi upendayo.