Jimai: Ameota Yuko Na Mke Wake Akatokwa Na Madhii Katika Ramadhwaan Nini Hukmu Yake?
SWALI:
asalam alaikum
swali langu ni kwamba mimi nilivo kuwa kitandani usubuhi nikawa namfikiria
demu wangu mpaka nikatokwa na manii aina ya maji ila mazito ila sio manii
ya kawaida nai yale ya kutamani je nimefungua na hukmu yake ninini na timeile nilikuwa macho.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Tunashukuru kwa swali lako
Tunakunasihi utumie Lugha nzuri ya heshima unapouliza maswali, hii ni tovuti ya dini na si kijiwe cha kupiga soga za kidunia na mambo machafu.
Ama kuhusu swali lako, inadhihirika kwanza wazi kuwa una rafiki wa kike (Girl Friend) na hiyo ni hatari kubwa kwa Muislam. Uislam umeharamisha mahusiano yoyote yasiyo ya kisheria baina ya jinsia mbili hadi watu watakapooana. Unayofanya ni mambo ya haraam na unapaswa uyaache haraka
Allaah (Subhanaahu wa T'ala) Amekataza japo kuikaribia zinaa, Aliposema:
(( وَلاَ تَقْرَبُواْ الزِّنَى إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاء سَبِيلاً))
((Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya)) [Israa : 3]
Na vile vile tambua kuwa mahusiano hayo hayaruhusiwi si mwezi wa Ramadhaan tu, bali hata miezi mingine yote iliyobaki. Na adhabu ya mzinifu ni kali
Adhabu za Zinaa katika sheria ya Kiislamu ni kali mno na lau
Mzinzi ambaye hajaoa au kuolewa anafaa apigwe mijeledi mia moja hadharani
((الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا مِئَةَ جَلْدَةٍ وَلَا تَأْخُذْكُم بِهِمَا رَأْفَةٌ فِي دِينِ اللَّهِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلْيَشْهَدْ عَذَابَهُمَا طَائِفَةٌ مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ))
((Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma kwa ajili
Na ikiwa ameoa au ameolewa basi wapigwe mawe hadi kufa
فِي الصَّحِيحَيْنِ مِنْ رِوَايَة الزُّهْرِيّ عَنْ عُبَيْد اللَّه بْن عَبْد اللَّه بْن عُتْبَة بْن مَسْعُود عَنْ أَبِي هُرَيْرَة وَزَيْد بْن خَالِد الْجُهَنِيّ فِي الْأَعْرَابِيَّيْنِ اللَّذَيْنِ أَتَيَا رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ أَحَدهمَا : يَا رَسُول اللَّه إِنَّ اِبْنِي هَذَا كَانَ عَسِيفًا - يَعْنِي أَجِيرًا - عَلَى هَذَا فَزَنَى بِامْرَأَتِهِ فَافْتَدَيْت اِبْنِي مِنْهُ بِمِائَةِ شَاة وَوَلِيدَة فَسَأَلْت أَهْل الْعِلْم فَأَخْبَرُونِي أَنَّ عَلَى اِبْنِي جَلْد مِائَة وَتَغْرِيب عَام وَأَنَّ عَلَى اِمْرَأَة هَذَا : الرَّجْم فَقَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ((وَاَلَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَأَقْضِيَنَّ بَيْنكُمَا بِكِتَابِ اللَّه تَعَالَى الْوَلِيدَة وَالْغَنَم رَدّ عَلَيْك وَعَلَى اِبْنك مِائَة جَلْدَة وَتَغْرِيب عَام . وَاغْدُ يَا أُنَيْس - لِرَجُلٍ مِنْ أَسْلَم - إِلَى اِمْرَأَة هَذَا فَإِنْ اِعْتَرَفَتْ فَارْجُمْهَا)) فَغَدَا عَلَيْهَا فَاعْتَرَفَتْ فَرَجَمَهَا البخاري و مسلم
Katika Swahiyhayn kutoka kwa Abu Hurayrah na Zayd bin Khaalid Al-Juhaniy (Radhiya Allaahu 'anhum) katika kisa cha Mabedui wawili waliokuja kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Mmoja alisema: "Ewe Mjume wa Allaah, mwanangu (wa kiume) aliajiriwa na bwana huyu kisha akafanya zinaa na mke wake. Nimemlipa fidia kwa ajili ya mwanangu kwa kumpa kondoo mia moja na mtumwa mwanamke. Lakini nilipowauliza watu wenye elimu, wamesema kwamba mwanangu apigwe mijeledi mia na ahamishwe mji kwa muda wa mwaka na mke wa huyu bwana apigwe mawe hadi afariki". Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, nitahukumu baina yenu wawili kutokana na Kitabu cha Allaah. Rudisha mtumwa mwanamke na kondoo na mwanao apigwe bakora mia kisha mwanao ahamishwe mbali kwa muda wa mwaka. Nenda Ewe Unays!)) Alimwambia mtu katika kabila la Aslam, ((Nenda kwa mke wa huyu bwana na akikiri makosa yake, basi mpige mawe hadi mauti [yamfike])) Unays akamuendea na akakiri makosa yake, kwa hiyo akampiga mawe hadi mauti. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Pia tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo kuhusu Madhara ya Zinaa na Adhabu Zake
Nini Hukumu Ya Mwenye Kuzini Kwa Siri?
Kufanya Mapenzi Bila Ya Kitendo Cha Ndoa Kwa Ambaye Hajaolewa?
Kuwa kwako na mahusiano ya haraam kumekupelekea hadi kumuota huyo mwanamke kwenye ndoto zako katika mwezi huu mtukufu. Tunamuomba Allaah Akusamehe na Akuongoze, na fanya toba ya kikweli kweli. Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate makala za Tawbah.
Ikiwa ushaacha mahusiano hayo ya haraam. Na ikiwa bado hujaacha mahusiano hayo ya haraam, basi hii ni fursa kubwa katika mwezi huu kuacha na kurudi kwa Mola wako Aliyekuumba na Akakupa pumzi na uhai na rizki na afya njema ambayo wewe hivi sasa unaitumia katika kumuudhi na kumuasi huyo Aliyekuruzuku vitu hivyo.
Ama kuhusu swali lako, ikiwa hayo yaliyotoka si manii halisi
Na haifai kukaa kujiwazisha na kujifikirisha mambo machafu na maovu
Na Allaah Anajua zaidi