Sambusa Za Viazi
Sambusa Za Viazi
Vipimo
Viazi - 4
Vitunguu nyasi vilokatwakatwa - 3 miche
Kitunguu maji kilokatwakatwa - 1
Chumvi - 1 kijiko cha chai
Bizari ya pilau nzima ( jeera) - 1 kijiko cha chai
Mafuta - Nusu kilo
Manda za tayari - 10 - 20
Yai - 1 au 2
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Menya viazi, vioshe vikate slesi kisha vikatekate vipande vidogo vidogo.
- Chemsha maji kidogo ukiwa umeyatia chumvi , kisha vimimine viazi ndani ya maji yawache paka uwone tena yachemka kwa mara ya pili acha kwa dakika 10 - 15, kisha ondoa jikoni.
- Mimina katika chujio uchuje maji .
- Roweka bizari kwenye maji kwa muda wa dakika 20 hivi.
- Chukua bakuli kubwa lenye nafasi mimina viazi, vtunguu nyasi na maji, chumvi, mafuta vijiko 2 – 3 vya supu, na bizari. Changanya vizuri.
- Tandaza manda mezani au kwenye kibao fanya mkunjo wa sambusa kisha paka yai kwa brashi, kunja upate pembe moja . Tazama picha.
- Jaza viazi sehemu ulokunja kisha funga sambusa.
- Tia mafuta katika karai, yakipata moto, tia sambusa ziikaange hadi zigeuke rangi ya dhahabu.
- Zitoe na zichuje mafuta tayari kuliwa kwa Sosi Ya Ukwaju au Chatine Ya Mtindi Na Nanaa