01-Kukata Undugu: Utangulizi
Utangulizi
Shukrani zote njema ni za Allaah rehema na amani zimuendee Mtume wa Allaah na watu wake, Maswahaba na waliomfuata, ama baada:
Kukata undugu ni dhambi kubwa na kosa kubwa inafungua mafungamano inakata vizuizi inaeneza uadui na chuki inahalalisha kukatana na kuhamana.
Kukata undugu kunaondosha mazoea na mapenzi kunaidhinisha laana na kuharakisha adhabu, kunazuia kushuka rehma na kuingia peponi, na kunakufanya uwe mpweke na dhalili, pia inakuvutia huzuni zaidi, ikikutokea balaa unategemea kwa nani kheri na wema inakuzidishia zaidi maumivu.
Dhambi hii Amekemea Allaah katika Kitabu Chake:
“Basi yanayotarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe jamaa zenu?
“Hao ndio Mwenyezi Mungu Aliowalaani, na Akawatia uziwi, na Akawapofoa macho yao.” Muhammad: 22-23
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
“Haingii peponi mkata undugu.”