Kudanganya Kuogopa Ghadhabu Za Mkewe Kwa Ajili Ya Kuoa Mke Wa Pili Inafaa?
SW
Asalaam alaykum,
Kuna ndugu yangu anataka kuolewa mke wa pili, ila huyo mwanaume kamuapia mkewe hatooa tena baada ya mkewe kujua ila kuzuia ugomvi katika nyumba yake, kwa kifupi kamdanganya maana bado anamwambia ndugu yangu bado anampenda na atamuoa na anamwambia uwongo kama huo unaruhusiwa katika dini maana anataka kufanya jambo la kheir, na mkewe akijua kama bado anataka kuoa tamletea taabu, Je ni sawa kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kuwa hautaoa mke mwingine na wakati mtu anayo nia ya kuoa kafanya hivyo kwa kuepuka matatizo ya nyumbani kwake? Fiamanillah.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho
.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu udanganyifu. Uongo ni jambo ambalo limekatazwa
Uislamu umehimiza
“Mwenye kutudanganya si katika sisi” (Muslim).
Inafaa mtahadhari
Uongo unaruhusiwa tu katika hali maalum kama katika kusuluhisha watu waliokhasimiana au wanandoa wanaotaka kuachana, na si katika suala
Na Allaah Anajua zaidi