Aayah Za Mwisho Katika Suratul Baqarah
SWALI:
Assalam Alaykum warahmatul - llahi wabarakat.
Naomba kujua tofauti ya hadiyth hizi mbili. Amesema Nabiy (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam): Mwenye kusoma aya mbili za mwisho wa suratul-baqarah Mara mbli baaye ya swaalah ya Isha (basi) Zinamtosheleza. kwa ibada ya usiku mzima. Vipi kumtosheleza huko. Na hadiyth myingine inasema pia amesema? Nabiy Swalla Allaahu alayhi wa sallam anayesoma aayah mbili za mwisho wa Suwrah Al-Baqarah usiku zinamtosheleza. Ipi ni sahihi
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Aliyetukuka Rabb wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allahu 'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Qiyaamah.
Hadiyth ya kwanza uliyotaja kuwa ni kusoma Aayah mbili baada ya Swalah ya 'Ishaa hatukuipata katika Hadiyth zinazojulikana kuwa ni Sahiyh. Ama Hadiyth Sahiyh kwa maudhui hii ambayo imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim ni ile iliyosimuliwa na Ibnu Mas'uud Al badry [Radhwiya Allaahu 'anhu]
من قرأ بالآيتين من آخر سورة البقرة في ليلة كفتاه
"Mwenye kusoma aya mbili za mwisho za suratu-Baqarah usiku zinamtosheleza".
Hadiyth hii ina maana kwamba inamtosheleza na shari za kila aina kama kukumbwa na majini, au shari ya aina yoyote nyingine na hubakia katika kinga usiku huo mzima hadi asubuhi.
Vile vile kusoma Aayatul-Kursiy pia ni kinga ya Muislamu pamoja na du'aa nyingine za kusoma kabla ya kulala ambazo ziko katika kitabu cha Hiswnul-Muslim kinachopatikana humu ndani ya Alhidaaya katika viungo vifuatavyo:
Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)
027-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni
028-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Kulala
029-Hiswnul-Muslim: Du’aa Unapojigeuzageuza Usingizini Usiku
030-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Wasiwasi Usingizini Au Kusikia Uoga Na Mfadhaiko
031-Hiswnul-Muslim: Ipasavyo Kufanya Na Kusema Mwenye Kuota Ndoto Njema Au Mbaya
Na Allaah Anajua zaidi