Nini Sababu Ya Kuteremshwa Suwrah At-Takaathur?

 

Nini Sababu Ya Kuteremshwa Suwrah At-Takaathur?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Naomba mnitumie tafsiri ya suratul alhaakum' takathuru pamoja na kisa chake.

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Surwah At-Takaathur imeteremshwa Makkah kulingana na Mufassiriyn wengi. Hii ni Suwrah ambayo ina Aayah nane na katika Suwrah zilizoteremshwa mwanzoni katika kipindi cha Makkah.  

 

Hatukuipata sababu ya kuteremshwa kwake katika Swahiyh Asbaab An-Nuzuwl.

 

Ila Ibn Abiy Haatim amenukuu kuwa Abuu Buraydah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Suwrah hii imeteremshwa kuhusiana na makabila mawili, Bani Haarithah na Bani al-Harth ambao walijifakharisha utukufu na matendo mazuri ya watu wao walio hai; bado ya hapo walikwenda makaburini na kujifakharisha na ‘amali tukufu na nzuri za waliofariki. Hapo ndipo Suwrah hii iliteremshwa.

 

At-Tirmidhiy, Ibn Jariyr na Ibn al-Mundhir wamepokea rai hii ya ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliyesema: “Tulikuwa na shaka kuhusu adhabu ya kaburi mpaka Alhaakumut Takaathur ilipoteremshwa”.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share