Kumpa Mtoto Jina La Kikristo Inafaa Au Dhambi?
SWALI
Assalam Alleykum warahmatullah wabarakat
Mimi nimuislam nimetokea kulipenda jina moja zuri la kikristo je ni dhambi?
JIBU
Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Hatuoni kwa nini Muislam kulipenda jina la Kikristo na hali kuna majina mengi mazuri katika Uislam?
Nini hasa kinaweza kumshawishi Muislam hadi kulipenda jina la Kikristo? Je, ni kuwapenda wao? Je, ni kuwa na mtu mwenye jina
Inawezekana ikawa ni moja ya hayo, na zaidi ni Muislam kutofahamu vizuri mafundisho mazuri ya Uislam; vipi Uislam unafundisha kuhusu kuitana, na majina yepi yaliyopendekezwa na Mtume wetu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na yepi majina yanayopendwa zaidi na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) n.k.
Tunakuwekea hapa chini viungo vya kuonyesha mafunzo ya Uislam kuhusu majina, na umuhimu wa kuwa na majina mazuri ya Kiislam
Majina Ya Watoto Na Maana Yake
Jina ni utambulisho wa mtu na utambulisho huo bila shaka unapaswa kuwa unawakilisha kitu au maana nzuri kabisa. Hivyo, pamoja na kuwa haikatazwi kuwa na jina lenye maana nzuri japo si katika majina ya Kiislam, lakini lazima ufahamu kuwa utakapokuwa na jina lisilojulikana katika Uislam na ambalo linajulikana katika dini nyingine, basi tayari utakuwa umejiwekea ugumu mwenyewe kutambulika na kufahamika kwa urahisi katika jamii yako ya Kiislam kama ni Muislam na pia kutopata ushirikiano wa haraka na mwepesi na mzuri kutoka kwa ndugu zako Waislam kwa kudhania au kuamini kuwa wewe si mwenzao.
Pia jina ni heshima na unapokuwa na jina zuri la Kiislam, basi heshima yako katika jamii inakuwa kubwa kuliko kuwa na jina la Kikristo. Isitoshe kujiita jina la Kikristo ni katika kujifananisha nao na
Pia je, umezingatia kuwa mwanao atakapofikia umri wa kutambua kila jambo, akajua kwamba jina ulompa ni la Kikristo naye akachukizwa nalo? Je utamjibu nini? Huoni kwamba hapo itakuleteeni matatizo wote pamoja na mihangaiko ya kubadilisha vyeti vyake vyote pindi akiazimia?
Na Allaah Anajua zaidi