Amemrudia Mke Aliyeritadi Na Ambaye Alikuwa Akimhubiria Aingie Ukiristo
SWALI:
Assalaam aleykum.
Jamaa yangu alimsilimisha mwanamke akamuoa. Bahati mbaya wakaachana na yule mwanamke akasema kwa kutamka kuwa amerudi dini yake ya Ukristo baada ya kuachwa manake yeye alisilimu kwa kutaka kukaa na huyu bwana tu. Akawa anamletea huyu bwana makala za kumhubiria ili nae aingie ukristo. Baadae yule mwanamke akasema hajarudi dini yake ile ilikuwa ni kumfanya huyu bwana amrudie tu. Na huyu bwana amemuoa tena. Jee nini hukumu yake?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kumrudia mke aliyeritadi baada ya kumuacha.
Suala hili la kuoa mke au kuolewa na mume aliyesilimu na baada ya hapo ikafanywa Nikaah huwa yapo matatizo mengine. Tumetahadharisha
Ni nasaha kwa sote tufuate maagizo ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika kuchagua mchumba. Miongoni mwa maagizo ni kutafuta mke aliyeshika Dini na mwenye maadili mema. Mwanamke amesilimu leo na kesho kuolewa Dini yake imejulikana wakati gani? Shida zinazopatikana zinakuwa nyingi zisizokuwa na hesabu ya aina yoyote ile. Inatakiwa tuwe waangalifu
Wengi wanachukua ruhusa iliyotolewa kuwaoa wanawake wa Kiyahudi na Kikristo, lakini hata hivyo Allaah Aliyetukuka Ameweka sharti muhimu
Ikiwa mwanamke huyo baada ya kupatiwa talaka aliritadi hakutakuwa na ndoa baina
Na Allaah Anajua zaidi