Zipi Ishara Za Kurogwa Au Kufanyiwa Uchawi?
Zipi Ishara Za Kurogwa Au Kufanyiwa Uchawi?
SWALI:
Nashukuru sana kwa majibu mazuri mnayoupa kuhusu masuala yetu mbalimbali. Vipi nitaweza kujua kwamba nimerogwa au nimepatwa na uchawi, naomba mnieleze ishara mbali mbali za kumjua mtu aliyeathirika na uchawi.
Ombi, kama itakuwa vigumu kurushwa kwenye mtandao kwa sasa naomba nijibuni kupiti kwenye e-mail yangu.
JIBU:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho
Hakika zipo ishara nyingi na kila mmoja anapata ishara zake mwenyewe. Ishara moja ni Kufikiria kuwa unafanya kitu ilhali hufanyi na mengineyo. Na njia rahisi ni kusomewa Suwrah na Aayah za Ruqyah, ikiwa mtu huyo kafanyiwa uchawi basi atatoa ishara ambazo mwenye kumsomea atazifahamu na hivyo kumtibu. Mara nyingi inakuwa huyo aliyerogwa anazungumza kwa sauti isiyo ya kawaida na kuelekeza vitu vilivyotumika na mahali vilipowekwa.
Lililo muhimu zaidi ni kila Muislamu awe atasoma sehemu za Qur-aan na nyiradi ambazo zitamuhifadhi yeye na uchawi na kulogwa. Nazo utapata katika maelezo yaliyomo katika viungo vifuatavyo:
Kuhusu Mashaytwaan Na Vipi Kujikinga Nao
Mke Wangu Amevaliwa Na Majini Wa Mahaba? Hapendi Kutenda Kitendo Cha Ndoa Na Mimi
Mke Analalamika Mume Ana Mashetani Yanamfanya Asiweze Kukamilisha Tendo La Ndoa
Pia ingia katika kiungo hiki, upate Du’aa na Adhkaar mbalimbali za kinga na kulogwa:
Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)
Na Allaah Anajua zaidi