Kulipa Kodi Kwa Pesa Za Ribaa Inafaa?
Kulipa Kodi Kwa Pesa Za Ribaa Inafaa?
SWALI:
Assalam aleikum warahmatullahi wabarakatu. Ama baada ya salamu namshukuru Allah kwa neema hii yote alio tupa kwa mtandao huu adhimu na Awaezashe ni wenye kuiendeleza mpaka apendapo Yeye Jalali.
Ama kwa swali langu ni kuwa katika nchi hizi za kikafiri huwa mabenki mengi hutoa na kupokea riba na vile vile serikali za kikafiri pia hutoza ushuru kwa raia wake je ni sawa kulipa ushuru kwa pesa za riba? Allah awajazi kila la kheri.
JIBU:
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Haifai kwako kulipa kodi kwa kutumia ribaa ambayo si haki yako wala si mali yako. Hivyo hivyo, serikali ina haki kuchukua kutoka kwa wananchi kodi ili iweze kutekeleza miradi yao pamoja na kuwasaidia raia wake kwa njia moja au nyingine.
Usaidizi huo unafanya hata wakimbizi wengine wakiwa ni waongo kupata usaidizi kutoka kwa serikali kuwawezesha kuishi bila matatizo. Na huenda wewe au mwengine ambaye anaishi katika nchi hiyo ya kikafiri mumenufaika katika hilo.
Kwa hiyo fanya hima kujiepusha na mas-ala ya ribaa.
Na Allaah Anajua zaidi