Kumuoa Mtoto Wa Kambo Inafaa?
SWALI:
Asallam allaikum je ni makosa kuishi na mtoto wa kambo nae mue mumeelewana na kukubaliana baina yako na mkeo au mumeo kisha ukamuoa na mkawa jamii moja, ni sawa.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kumuoa mtoto wa kambo.
Ama kuhusu suala
“Mmeharimishwa kuoa mama zenu … na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu, waliozaliwa na wake zenu mliowaingilia” (4: 23).
Kwa hiyo, mtoto wa kambo ambaye tayari umemuingilia mama yake huwa hufai tena kumuoa binti hiyo kisheria. Na hata ukimuacha mama yake, hutoweza kumuoa mtoto huyo wa kambo.
Na Allaah Anajua zaidi