Nikilipa Deni La Benki Kabla Ya Muda Uliowekwa Itakuwa Bado Nimeingia Kwenye Ribaa?

SWALI:

 

Aslam alaykum warhamatulahi wabarakatu, naomba kuuliza kuna baadhi ya mabenki yana kopesha bila riba, lakini wanaweka hela kidago ziada na ukiwauliza je hii siyo riba wanasema sio riba bali ni pesa ya ushuru na wanakupangi miezi ya kulipa miezi wanayo kupangi ni 12 usizidishe ukizidisha inakua na riba, je hela hii inafa kukopa kama mtu ataweza kurudisha kwa miezi 12 naomba jibu. Wasalam mungu wape mema yote na mazuri yote na uhayi mrefu ili mzidi kutuelimisha na makazi yenu yawe janatul-firdausa Amin.

 


 

 

JIBU:

 

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu deni la benki unaloambiwa si ribaa.

 

 

Hakika ni kuwa hakuna benki ya kawaida (conventional) ambayo inakopesha bila ribaa. Ribaa yenyewe inaweza kuwa ndogo au kubwa. Benki inaweza kukuambia lolote kuhusu hilo lakini ukweli ni kuwa hiyo ni ribaa. Hata ikiwa ni ndogo, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:

 

Dirham ya ribaa anayokula mtu naye anajua ni nzito zaidi kuliko zinaa thelathini na sita” (Ahmad)

.

Na amesema vilevile, “Ribaa ina milango sabiini na tatu, iliyo nyepesi zaidi ni mtu kumuingilia mama yake” (al-Haakim).

 

Na Allaah Aliyetukuka Anasema:

 

 

Na kama hamtofanya (kuacha ribaa), basi fahamuni mtakuwa mmetangaza vita na Allaah na Mtume Wake” (al-Baqarah [2]: 279).

Na kauli ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Jiepusheni na maangamivu saba”. Akaulizwa: “Ni yepi ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Kumshirikisha Allaah, uchawi, na kuua nafsi ambayo Allaah Ameharamisha ila kwa haki, kula ribaa, kula mali ya mayatima, kukimbia siku ya mapambano, na kuwasingizia Waumini watoharifu wasiojua maovu” (al-Bukhaariy na Muslim).

 

Ni bora na muhimu sana kujiweka mbali na mikopo aina hiyo isipokuwa ikiwa ni mas-ala ya kifo na uhai.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share