Kachori Za Spices

Kachori Za Spices

Vipimo

Viazi - 1kg

Ndimu - 2

Rai - 2 vijiko vya chai

Unga wa ngano au wa dengu - 2 vikombe vya chai

Bizari ya majano - 1 Kijiko cha chai

Methi (uwatu) iliyosagwa  1/2 kijiko cha chai

Bizari ya jira (cummin)  1/2 kijiko cha chai

bizari ya mchuzi - 1/2 kijiko cha chai

Chumvi - Kiasi

Pilipili ya unga - Kiasi upendavyo

Mafuta ya kukaangia

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Osha viazi vizuri na viweke katika sufuria
  2. Tia maji ndani ya sufuria iliyokuwa na viazi na hakikisha maji niyakutosha kuweza kuivisha viazi
  3. viweke jikoni vichemke na kuiva baada ya hapo viweke viazi pembeni vipoe kwanza
  4. Kisha menya maganda na uviponde ponde hadi vilainike
  5. Tia chumvi kiasi, ndimu, rai, bizari zote na pilipili  na vichanganye pamoja vizuri.
  6. Kata madonge madonge na yazungushe zungushe katika mikono ili yawe duara
  7. Chukua unga na tia bizari ya majano, chumvi kiasi na maji kiasi
  8. Changanya mchanganyiko huo hadi uchanganyike vizuri uwe mzito mzito
  9. Weka kikaango jikoni na subiri mafuta yapate moto
  10. Kisha chukua donge moja moja na lichovyee lote katika unga ulio tengeneza hakikisha donge hilo limeenea unga huo sehemu yote
  11. Kisha tumbukiza katika kikaango na fanya hivyo kwa madonge mengine yaliyo bakia
  12. Baada ya kumaliza yote tia katika sahani na tayari kwa kuliwa

 

Share