Itakuwa Ni Nadhiri Akisema Moyoni Kuwa Atampa Mtoto Jina La Aliyefariki Kisha Asimpe?

SWALI:

 

Assalamu alaikum, nina suali langu ambalo nataka kuliza, hivi karibuni tulitoewa na msiba wa mtoto mdogo wa miaka sita. baada ya siku mbili tatu hivi, nikafikiria tu mimi mwenyewe kuwa nikipata mtoto nitamwita jina lake, ikiwa mpaka hapo hakuna yeyote ambaye ashalita jina hilo. lakini sikumwambiya mtu yoyote. je, kwa mfano ikiwa nimepata mtoto na mimi nataka kuita jina lengine inafaa? tafadhali ni jibu. Ahsantum.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako la kumpatia mtoto wako jina.

Hakika suala la kufikiria kitu au kukipanga ni suala la kawaida kabisa ambalo humtokea kila mmoja wetu.

 

 

Hiyo si nadhiri, kwani nadhiri unaielekeza kwa Allaah Aliyetukuka kwa kumwambia nikipata mtoto, nitafanya jambo kadhaa. Ikiwa hukuweka Niyah hiyo kutakuwa hakuna tatizo la kubadilisha jina lake atakapo zaliwa au kumuita jina hilo hilo.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share