Bajia Za Bilingani Na Sosi Ya Kijani
Bajia Za Bilingani Na Sosi Ya Kijani
Vipimo
Bilingani - 2 ya kiasi
Unga mweupe - ½ kikombe
Unga we semolina - ½ kikombe
kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 1 kijiko cha chai
Vitunguu vya majani (spring onions) katakata - ½ kikombe (chopped)
Pilipili manga - ½ cha chai
Haldi (bizari manjano/tumeric) - ½ kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
*Sosi ya kijani ya kikolezo (seasoning) - 1 kijiko cha supu
Maji ya kuchanganyishia - kiasi
Mafuta ya kukaangia - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
- Weka mafuta katika karai
- Osha bilingani kisha kata slesi za duara za kiasi
- Changanya vitu vikavu kwanza katika bakuli kisha tia maji uchanganye vizuri. Mchanganyiko usiwe mwepesi sana.
- Kisha tia vitu vilobakia kama thomu, sosi ya kijani ya kukoleza na endelea kuchanganya vizuri.
- Chovya slesi za bilingani katika mchanganyiko uingia pande zote mbili. Usichovye sana.
- Tia katika mafuta ya moto kisha ukaange na ugeuze pande zote mbili hadi igeuke rangi.
- Chuja katika karatasi ya kuchujia mafuta (Paper towel) kisha panga katika sahani na ikiwa tayari kuliwa na sosi ya ukwaju, au nyinginezo.
Bonyeza kiungo upate sosi za kulia bajia:
*Sosi Ya Kijani Ya Kukoleza (Green Seasoning)
Vipimo:
Vitunguu vya majani (spring onions) - 1 msongo
Figili mwitu (celery) - 2 miche
Kotmiri (coriander) - ½ kikombe
Pilipili mbichi - 3
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha
- Katakata vitu vyote kisha tia katika mashine ya kusagia (blender).
- Tia maji kama ¼ kikombe, saga hadi iwe laini. Ikiwa nzito ongeza maji lakini isiwe nyepesi sana.
- Weka katika chupa kisha hifadhi katika friji au freezer utumie kwa mapishi mengineyo kama mchuzi n.k.