Saladi Ya Vitunguu Na Pilipili Mboga Tofauti
Saladi Ya Vitunguu Na Pilipili Mboga Tofauti
Vipimo
Saladi la duara - 1
Tango - 1
Pilipili mboga jekundu - ½
Pilipili mboga kijani - ½
Pilipili mboga manjano - ½
Karoti - 1
Kitunguu cha zambarau (red onion) - ½
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katakata saladi la duara lioshe, lichuje na lipange katikati kwenye sahani.
- Katakata matango slesi yapange kuzunguka sahani.
- Kuna (grate) karoti kisha mwagia juu ya saladi kisha katakata mapilipili mboga tupia tupia juu ya karoti.
- Kata kitunguu slesi kisha tupia tupia juu.
Kidokezo:
Ukipenda changanya ndimu , mafuta ya alizeti (olive oil) na chumvi mwagia juu.