Uzazi: Mwenye Kunyonyesha Anaruhusika Kutokufunga? Na Je Inampasa Alipe Deni?
SWALI:
Assalam aleikum,
Samahani kiswahili changu si kizuri so i will ask in english :
Alhamdullilah i had a baby girl two months ago and am breast feeding at the moment,i try to fast one day at a time as am breast feeding, am i exempted from fasting at this time because am breastfeeding and if so,do i have to pay later insh Allah
Jazzaka Allau Kheirah
JIBU:
Sifa zote njema anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shari'ah inakuruhusu kula ikiwa unakhofu kuwa Swawm itakufanya ukose maziwa ya kumnyonyesha mtoto. Kisha unatakiwa ulipe deni lako baada ya Ramadhaan. Na ikiwa utashindwa kulipa hadi Ramadhaan nyingine, Wanachuoni wametofautiana kuhusu kulipa kafara; wako wanaoonelea kuwa utalipa Swawm na kutoa kafara, na wako wanaoonelea kuwa utalipa tu Swawm zako bila kutoa kafara. Na hii rai ya pili ina nguvu zaidi.
Kwa maelezo zaidi tafadhali ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi kuhusu maudhui hiyo:
Na Allaah Anajua zaidi