Slesi Za Mkate Za Jibini Na Kitunguu Saumu (Thomu) Na Oregano (Italian)
Slesi Za Mkate Za Jibini Na Kitunguu Saumu (Thomu) Na Oregano (Italian)
Vipimo
Slesi za mkate- 15 – 20
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 3 vijiko vya supu
Jibini ya malai (cream cheese) - ½ kikombe
Siagi (butter) - 2 kijiko vya supu
Mafuta ya zaytuni (olive oil) - 1 kijiko cha supu
*Oregano (Italian herb) - ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Saga kitunguu thomu kiwe laini kabisa.
- Katika bakuli dogo, changanya kitunguu thomu, siagi, jibini na mafuta. Koroga ichanganyike vizuri.
- Pakaza kwenye slesi za mkate
- Nyunyizia oregano juu ya slesi
- Choma (grill) katika moto mdogo mdogo hadi slesi ziegueke rangi kidogo. Kisha epua zikiwa tayari
Kidokezo:
- Kiasi ya vipimo inategemea upendavyo kujaza slesi za mkate . Ikiwa utapenda kujaza kwa wingi, unaweza kuongeza kila kipimo kidogo zaidi.
- Oregano inauzwa tayari madukani
- Slesi nzuri zikiliwa moto moto na chai.