Mavazi Ya Maaskari Wa Kike. Je Wanaruhusika Kuvaa Hivyo Kama Ni Udhuru?
Mavazi Ya Maaskari Wa Kike. Je Wanaruhusika Kuvaa Hivyo Kama Ni Udhuru?
SWALI:
Assalamu alaykum,
Kwanza niwapongeze kwa juhudi kubwa mnayoifanya katika kuielimisha jamii hasa ya kiislamu kwa njia ya mtandao.
Uislamu unaelezeaje juu ya mavazi ya ndugu zetu wanawake wa kiislamu ambao ni maaskari? I mean wanao udhuru wa kuvaa hivyo? Maana ni wazi hawako katika sitara inayokubalika kiislamu na kishari’ah!
JIBU:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Uislamu umeweka shari’ah kuhusiana na kivazi cha mwanamke Muislamu kwa kumuweka katika hali ya muruwa na heshima. Kwa ajili hiyo, Uislamu unataka mwanamke Muislamu awe atavaa vazi la heshima anapotoka nyumbani kwake. Hakuna udhuru kabisa kwa mwanamke Muislamu awe ni askari au anafanya kazi nyingine yoyote kuvaa kivazi ambacho hakiendi sambamba na shari’ah ya Kiislamu.
Na pia hakuna dharura yoyote kwa mwanamke kuingia katika kazi ya uaskari au nyingine yoyote ambayo haitompatia ruhusa kuvaa vazi lake la heshima. Kwa hiyo, kazi hiyo si dharura kwa mwanamke kutovaa kishari’ah.
Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:
Kuvaa Niqaab Ni Fardhi? Nini Hukmu Ya Mwanamke Kuvaa Suruwali?
Mwanamke Anavaa Hijaab Lakini Anavaa Suruwali Ya Kubana Anaposwali, Inakubaliwa Swalah Yake?
Na Allaah Anajua zaidi