03-Kwa Ajili Ya Allaah Kisha Historia: Uhakika wa Kujinasibisha Na Ahlul Bait

 

Inavyofahamika kwetu sisi  mashia nikwamba tunajihusisha sana na Ahlul-Bayt, na madhehebu ya kishia yamejengeka katika misingi ya kuwapenda Ahlul-Bayt -kwa mawazo yetu-, kwa hiyo kupendana kwetu au kuchukiana na watu wengine (AHLUS SUNNAHH) ni kwa sababu ya Ahlul Bayt, na kuwachukia maswahaba hasa makhalifa watatu akiwemo Bi Aisha binti Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambae ni mke wake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na fikra za mashia wote wakubwa kwa wadogo wanawake kwa wanaume wasomi wao na wajinga wao wanaitakidi kwamba maswahaba wamewadhulumu Ahlul Bayt pia wakawauwa na wakawavunjia heshima zao .

 

Na fikra za mashia nikwamba Ahlus Sunnah ndio walio pandikiza fikra za uadui kwa Ahlul-Bayt kutokana na fikra hizo, hakuna anae sita katika sisi (mashia) kuwaita Ahlus Sunnah maadui, na siku zote tutaikumbuka damu ya shahidi Hussein (‘Alayhi salaam) lakini vitabu vyetu tunavyovitegemea sisi (mashia) vinatueleza ukweli wa mambo tofauti na itikadi yetu, kwani vitabu vyetu vinatufahamisha jinsi gani Ahlul-Bayt wenyewe walivyokuwa wakiwachukia wafuasi wao(mashia) vitabu hivyo pia vinatufahamisha maovu waliyo yafanya mashia waliotangulia kwa Ahlul-Bayt, pia vinatufahamisha ni kina nani walio mwaga damu za Ahlul-Bayt, na ni kina nani walio sababisha vifo vyao na nikina nani walio vunja heshima zao.

 

Amesema Amirul muuminina (‘Alayhi salaam) {Lau kama utawachunguza mashia (wapambe) wangu basi hutawakuta isipokuwa ni wakunisifia tu, na kama utawapa mtihani mtihani (wakupima imani zao) basi hutowakuta isipokuwa ni murtad wote (wametoka katika dini) na lau kama utawachuja hungempata hata mmoja katika elfu} (ALKAFY/ALRAUDHA 8/833).    

 

Na akasema Amirul muuminina (‘Alayhi salaam) {Enyi wenye kufanana na wanaumme na wala si wanaume, wenye  fikra za kitoto na akili za kike  natamani nisingewaona  wala nisingewajua, jambo ambalo limenisababishia majuto na tabu kubwa, Mwenyezimungu awalaani, hakika mmeujaza moyo wangu uchafu na kifua changu mmekijaza chuki, na mmenijengea tuhuma na mmeniharibia mawazo yangu kwa kuniasi na kunidhalilisha, mpaka maquraish wakasema kuwa mtoto wa Abii Twalib ni mtu shujaa lakini hajui vita. Lakini nitafanyaje wakati hakuna  mtu anaetii amri yangu} NAHJUL BALAGHA  70-71.

 

Na akawaambia wao kwa kuwakemea:- nimepewa mtihani kwa ajili yenu kwa mambo  matatu, na mawili: (viziwi wenye masikio, na mabubu wenye kutamka, na vipofu wenye macho, sina marafiki wa kweli wakati wa kukutana na maadui na sina ndugu wa uhakika wakati  wa matatizo.mumemfedhehesha  mtoto wa Abuu  Twalib kama mwamke asie na nguo) NAHJUL BALAGHA  142.

Aliwaeleza hayo kwa sababu ya kumfedhehesha kwao na kumuhadaa kwao Amiril muuminina (‘Alayhi salaam) na anazo(amiril-muuminina) lawama nyingi zinazowahusu wao (mashia).

 

Na imam Husain (‘Alayhi salaam) amesema katika kuwaombea vibaya mashia ( wapambe) wake: { Ewe Mwenyezi Mungu ukiwastarehesha kwa muda wowote ule basi wagawe makundi, na uwafanye kuwa mapande mapande yenye kukhtalifiana  nyendo zao, na wla usiridhie wao kuwa viongozi daima (milele)  kwani wao walituita sisi ili watusaidie, kisha wakatufanyia uadui na wakatuua} ALIRSHADLIL MUFID uk 241.                                          

 

Na  aliwasemesha mara nyengine na akawaombea vibaya, katika maneno aliyo yasema: {lakini mlifanya haraka  kutuunga mkono, kama ndege wanao kimbilia mzoga, kisha  mkapukutika kama vile popo wanao tumbukia motoni,  kisha mkaivunja ahadi yenu  kwa upumbavu na kujiweka mbali na rehema na kujitumbukiza kwa matwaghuti wa umma huu, na  makundi mengine maovu na walioacha kitabu cha Allah, kisha ninyi ndio mnaotudhalilisha  na kutuua fahamuni yakua laana ya Mwenyezi Mungu itawashukia  madhalimu} AL-IHTIJAJU 2/24

 

Na maelezo haya yanatuwekea wazi ni akina nani waliomuua Hussein, Nao siwengine bali ni  mashia wake (wapambe) watu wa “Kuufa”, ni mababu zetu basi kwanini tunawabebesha Ahlus Sunnah majukumu ya mauaji ya Husein (‘Alayhi salaam)?

 

Na kwa ajili hii amesema  bwana  Muhsin Al Amin ( watu wa Iraq wapatao ishirini elfu walimuunga mkono Husein, kisha wakamsaliti, na wakamuasi ingawa walimuahidi  kutii, na kisha wakamuua) A’YANU- SHIA 1/32. 

 

Hasan (‘Alayhi salaam) amesema: (Naapa kwa Mwenyezi Mungu ninamuona muawiya ni m’bora kwangu kuliko hawa  wanaodai kwamba wao ni kundi langu, walitaka kuniua na walichukua mali zangu, naapa kwa Mwenyezi Mungu kuchukua kutoka  kwa muawiya kile ambacho kitazuia kumwagika  daamu yangu na nikapata amani kwa watu wangu hilo ni bora  kuliko kuniua na kuwapoteza Ahlul Bayt (jamaa zangu) naapa kwa Mwenyezi Mungu kama ningepigana na muawiya, wagenikamata na kunipeleka kwa  muawiya kwa kutaka amani,   naapa kwa Mwenyezi Mungu kuingia  mkataba wa amani na muawiya katika hali ya heshima na utukufu  ni bora kwangu kuliko kuniuwa nikiwa mateka, AL-IHTIJAJU 2/10.

   

Imam Zayinul- Abidin (‘Alayhi salaam) aliwaambia watu wa kuufa: {Je mnajua kwamba mlimuandikia baba yangu na kumhadaa, na mkampa ninyi wenye ahadi, kisha mkampiga vita na kumfedhehesha basi ni kwa jicho gani mtamuangalia bwana Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake? Wakati akiwaambieni mmemuua mjukuu wangu na mmeivunja heshima  yangu basi ninyi si katika uma wangu} AL-IHTIJAJU2/32.

 

Pia aliwazungumzia akisema:(Ikiwa hawa wanatulilia sisi basi ni akinanani waliotuua wasio kuwa wao?} AL-IHTIJAJU 2/29.

 

 Na Albaqir (‘Alayhi salaam) amesema {lau wangalikuwa watu wote kwetu sisi ni mashia ingelikua robo tatu yao  ni wenye shaka na sisi na robo nyingine wangekuwa ni wapumbavu} RIJALUL KUSHY uk 79.

 

Na amesema Asadiq (‘Alayhi salaam){ni naapa  kwa Mwenyezi Mungu lau kama ningewapata  miongoni mwenu waumini watatu wanaoficha mazungumzo yangu  nisingeona halali kuwaficha mazungumzo} USULUL ALKAFI 1/496.

 

Na amesema  Fatma mdogo (‘Alayhi salaam) katika khutba aliyoitowa kwa watu wa kuufa: {Enyi watu wa (mji) wa kufa  enyi watu wa hiana na vitimbi na majivuno. Hakika, Ahlul Bayt Mwenyezi Mungu ametupa mtihani kwenu, na amekupeni mtihani kwetu, lakini akaufanya mtihani wetu kuwa ni mzuri, mkatukufurisha na mkatukadhibisha  na mkaona halali kutupiga vita  na mkaona ni halali kuiba mali zetu, kama mlivyo muua babu yetu juzi, na panga zenu bado zinadondosha damu zetu sisi Ahlul Bayt, mmepata hasara, basi  subirini laana na adhabu  kama vile tayari  imeshawashukia, na waonje baadhi yenu uchungu wa adhabu kwa vile mtakavyokaa milele katika adhabu yenye kuumiza siku ya kiyama kwa vile mlivyotudhulumu, basi jueni laana ya Mwenyezi Mungu  huwafikia madhalimu, hakika mnastahiki hasara ni yenu enyi watu wa kuufa, nimangapi nimeyasoma kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake kabla yenu kisha mkamfanyia hadaa ya kumuua ndugu yake  Ali bin Abii Talib na babu yangu na watoto wake na wajukuu wake wema.

Mmoja katika watu wa kuufa akatujibu kwa kujifakharisha akasema  {sisi ndio tulie muua Ali na watoto wake, kwa panga za india na mikuki,  Na tukawateka wanawake  wao kama  inavyo tekwa mali iliyoachwa na wenyewe, na tukawapiga pigo takatifu } AL IHTIJAJU2/28.

Na amesema Zainab mtoto wa Amirul muuminina (‘Alayhi salaam) kwa watu wa kuufa  kwa kuwakemea : (baada ya hayo, (utangulizi)Enyi watu wa kuufa, enyi watu hadaa na hiana, na wasaliti  Hakika ya mfano wenu  ni kama mfano wa mwanamke  alieukata uzi wake vipande vipande baada ya kuusokota,   hamna lolote zaidi ya kujisifu kwa mambo msiyokuwa nayo  na kujiona  na uongo! mnamlilia  ndugu yangu? Basi lieni sana na chekeni kidogo,  ni hakika kuwa mmefanyiwa mtihani, kwa kumuaibisha, vipi mliona rahisi kukiua kizazi cha Mtume wa mwisho (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) AL IHTIJAJU, juzuu ya 2 ukurasa wa  29-30.

 

Tunafaidika kutoka na hoja  hizi- na tumeziacha nyingi zisizokua hizo-  faida zifuatazo:

  1. Kuchoka na kukereka kwa  Amirul muuminin  na watoto wake juu ya wafuasi wao watu wa kuufa kwa hadaa zao na vitimbi vyao na usaliti wao.

 

  1. Usaliti wa watu wa kufa  na vitimbi vyao  vilivyopelekea  mauaji ya Ahlul Bayt na  kuvunjwa heshima yao.

 

  1. Kuwa watu wa Ahlul Bayt (‘Alayhi salaam) wamewabebesha  watu wao (mashia) majukumu ya kumuua Husain (‘Alayhi salaam) na waliopamoja nae.na amekiri mmoja wao kwa kumjibu kwake Fatuma mdogo kuwa wao ndio  waliomuua Ali na watoto wake, na kuwateka wake zao kama tulivyo kutangulizia .

 

  1. Hakika Ahlul Bayt (‘Alayhi salaam) waliwaombea vibaya wafuasi wao (mashia) na kuwa sifu kwamba  wao ni mataaghuti wa uma huu, na makundi  mengine  yaliyo bakia na waliokitupa kitabu, kisha wakaongeza juu ya hayo kwa usemi wao:- kuwa laana ya Mwenyezi Mungu itakua juu ya madhalimu. Na kwa sababu hiyo walimjia Abii Abdillah (‘Alayhi salaam) wakamwambia:- { hakika sisi tumepewa jina baya limeelemeza migongo yetu na limeua mioyo yetu  na viongozi wamehalalisha damu zetu kwa ajil yake, katika maelezo waliyo yapokea kwa wanazuoni wao.akasema  Abu Abdillah (‘Alayhi salaam):(jina lenyewe ni) Arrafidha?  Wakasema ndio, akasema : hapana si wao walio waita hivyo  lakini Mwenyezi Mungu ndie aliewaita hivyo} (ALKAAFI  JUZUUYA ‘5 ‘UKURASA WA ‘34.) Abuu  Abdallah akabainisha kuwa Mwenyezi Mungu ndie aliewaita hivyo (Arrafidha) na wala sio Ahlus Ssnnah walio waita jina hilo.

 

Kwa kweli  nimeyasoma maelezo haya  mara nyingi na nikayafikiria sana, nani kayaandika sehemu maalum, na nikakesha masiku mengi nikiyachunguza na kuyatafakari kwa makini maelezo haya –na mengineyo ambayo ni mengi kuliko niliyo yaandika – sikuzinduka katika fikra hizo ila nilijikuta nikisema kwa sauti kubwa sana “mwenye zimungu awe pamoja nanyi Ahlul-Bayt hakika mmekutana na misukosuko mingi kutoka kwa hawa wanaodai kuwa ni wafuasi wenu (mashia)” 

 

Sisi tunajua sote maudhi  yaliyowapata manabii wa Mwenyezi Mungu na Mitume wake (‘Alayhi salaam) kutoka kwa watu wao na yale yaliyo mpata Nabii wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake, lakini nimestaajabika na mambo mawili kutoka kwa Musa (‘Alayhi salaam) na subira yake juu ya wana wa israil, kwa sababu tunaona jinsi gani qur-an ilivyo muelezea mussa kuliko mtu mwengine na ikaeleza wazi jinsi alivyo vumiliya maudhi ya wana wa israel, na hadaa zao na vitimbi vyao na uadui wao.

Pia  ninawashangaa  Ahlul Bayt (‘Alayhi salaam) kwa kuvumilia kwao maudhi mengi waliyo yapata kutoka kwa watu wa kufa kitovu cha mashia, waliwa fanyia hiana wakawasaliti na kuwaua na kupora mali zao hata hivyo Ahll-Bayt waliyavumilia yote hayo, pamoja na hayo yote sisi bado tunawatupia lawama Ahlul-sunnah na tunawabebesha mzigo wote!

 

Na tunaposoma  vitabu vyetu vya kutegemewa tunapata mshangao, hawezi kuamini mmoja wetu tunaposema kuwa vitabu vyetu sisi mashia vinawakashifu Ahlul Bayt (‘Alayhi salaam) na kumkashifu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake,  kwa uthibitosha wa hayo soma maelezo yafuatayo:imepokewa  kutoka kwa Amirul muuminina (‘Alayhi salaam)  kwamba  punda wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aitwae Ghufayr alisema kumuambia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) : namtoa fidia  baba yangu na mamam yangu kwako ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, baba yangu alinisimulia kutoka kwa baba yake na babu yake, kua baba yake : alikuwa pamoja na nuhu katika safina akasimama akapangusa katika kiuno chake kisha akasema: katika mgongo huu atatoka punda ambae atapandwa na bwana wa Mitume na wa mwisho wao, namshukuru Mwenyezi Mungu ambae amenijaalia kua mimi ndie punda huyo. USUULUL KAFI 1/237.

Riwaya hii inatufundisha haya yafuatayo:

  1. Punda anazungumza!

  2. Punda anamsemesha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake kwa kumuambia  namtoa fidia kwako baba yangu na mama yangu  pamoja na kuwa waislamu ndio ambao  wanajitoa muhanga, kumuhami Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), kwa baba zao na mama zao sio punda.

  3. Punda anasema : {amenieleza baba yangu kutoka kwa babu yangu mapaka kufikia babu yake wa nne } ingawa  yakua kati ya Nhu na Mohamed  kuna miaka mingi sana, lakini punda huyu  anasema  kuwa babu yake wa nne  alikuwa pamoja na Nuh, katika safina (jahazi).

Siku moja  tulikuwa tunasoma kitabu kimoja kiitwacho Usuulul- kafi, pamoja na badhi ya wanafunzi wa chuo cha  cha Annajaf  kwa imam ALKHUUIY, akajibu imam ALKHUUIY kwa kusema : uangalieni muujiza huu, Nuhu(‘Alayhi salaam) anatoa khabari za Mohamad na unabii wake kabla ya kuzaliwa kwake kwa miaka mingi.

Yakabakia maneno ya  imam ALKHUUIY yana gonga gonga katika masikio yangu kwa muda mrefu huku nikijisemea katika nafsi yangu: itawezekana vipi jambo hili liwe muujiza?  na ndani yake kuna punda anamwambia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake, namatoa fidia kwako wewe baba yangu na mama yangu?!! Na vipi inawezekana kwa amiril-muminina (‘Alayhi salaam)(kiongozi wa waislamu) kunakili maneno kama haya? Lakini nikanyamaza kama walivyo nyamaza wasikilizaji wengine.

Na Sudduqu amenakili maelezo  kutoka kwa Aridhaa(‘Alayhi salaam) katika kuyayatafsiri maneno ya  Mwenyezi Mungu yasemayo

      (وإذ تقول للذي أنعم الله عليه وأنعمت عليه أمسك عليك زوجك واتق الله وتخفي في نفسك ما الله مبديه)

 سورة الأحزاب:37 "

{Na (wakumbeshe) ulipo mwambia yule ambae Mwenyezi Mungu amemneemesha( kwakumwaafikia uislamu) na wewe ukamneemesha kwa kuumpa ungwana, nae ni bwana Zaid bin Haritha (ulipomwambia) ‘Shikamana na mkeo na umche Mwenyezi Mungu(usimuache)’na ukaficha katika nafsi yako aliyotaka Mwenyezi Mungu kuyatoa.} ALAHZAB/37,

Amesema Arridha mfasiri wa aya hii {hakika ya Mtume (‘Alayhi salaam) na wtu wake alikwenda nyumbani kwa  Zaid bin Harith kwa haja fulani, basi akamuona mke zaid ambae ni Zainab akioga akamwambia: ametakasika aliye kuumba} UYUNU AKHBARU ARRIDHA uk 113.

Je  inawezekana kwa Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kumuangalia  mke wa mtu  muislamu, na kumtamani na kumshangaa? kisha amwambia ametakasika aliye kuumba?! Je hivi sikumtukana Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)?!

 

Imepokewa kutoka kwa Amirul muuminin kuwa alimuendea Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake na akiwa pamoja na Abu bakar na Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema {Nikakaa kati yake na Aisha, akasema Aisha hukuona chochote isipokua pajalangu na paja la Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)? akasema Mtume:nyamaza ewe Aisha }AL BURHAN FII TAFSIRL QUR-AN uk 4/225.

 

Na mara nyingine alikuja  bila kupata sehemu ya kukaa, akamuashiria Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kuwa njoo hapa akimaanisha nyuma yake, wakati huo  Aisha akiwa amesimama nyuma yake akiwa amejistiri:akaja Ali(‘Alayhi salaam)akakaa kati ya Mtume na Aisha, akasema Aisha kwa hasira: {hukupata sehemu ya kuweka matako yako isipokua paja langu? Akakasirika Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na akasema: Ewe kipunda usiniudhi kwa ndugu yangu)  KITABU SULAIM BIN QAIS 179.

Na imepokewa na Al-majlisy  kuwa Amirul muumini amesema:{nilisafiri pamoja na Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake, akiwa hana mtumishi isipokuwa mimi na alikuwa na shuka moja hana nyengine isipokuwa hiyo  na alikuwa nae Aisha katika safari hiyo, na alikuwa Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na watu wake analala kati yangu na Aisha, hakuna mtu  kati yetu aliekuwa na shuka zaidi ya shuka hiyo ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)

Basi ikawa  anaposimama kwa ajili ya sala za asiku hujifunua shuka kwa mkono wake katika sehemu yake ya katikatii kati yangu na Aisha mpaka shuka hugusa shuka la  tandiko ambalo liko chini yetu} BIHAARUL ANWARI 40/2.

 

Hivi kweli  Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ataridhika ‘Ali  akae katika mapaja ya bibi Aisha mkewe? Hivi Mtume hamuonei wivu mkewe itakuaje amuache kwenye godoro moja  na mtoto wa  Ami yake ambae hazingatiwi kuwa muharimu wake? Kisha ataridhika vipi  Amiril-Muminina juu ya hayo?!

 

Amesema bwana ‘ALI  GHURWIYU mmoja  kati ya wanazuoni wakubwa wa hapa chuoni {hakika  Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ni lazima utupu wake ukaingie motoni  kwa sababu yeye aliwaingilia wanawake washirikina akikusudia hivyo mke wake Aisha na Hafsa, na kusema maneno haya ni kumkosea heshima Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kwasababu lau itaingia tupu ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ndani ya moto hakuna atakae ingia peponi kamwe.

 

Natosheka na mapokezi haya sita yaliyomuhusu Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)na ali zake  Ili niende katika maudhui nyingine.

 

Pia wametoa maelezo mengi yamhusuyo Amirul muuminin (‘Alayhi salaam) yafuatayo ni sehemu ndogo katika hayo:

  1. Kutoka kwa Abu Abdillah (‘Alayhi salaam) amesema { aliletwa  mwanamke mmoja kwa ‘Umar akiwa amemng’ang’ania mtu mmoja  ambae alikuwa akimpenda akiwa amejimwagia weupe wa yai katika nguo zake na mapaja yake, akasimama ‘Ali akamuangalia yule mwana mke akamtuhumu na zinaa.BIHARUL-AL-ANWAR 4/303.

Na sisi tuna jiuliza: Je anawezaje Amirul muuminin kuangalia mapaja ya mwanamke ajnabi (anaeweza kumuoa) Na je inaingia akilini kwa  immu ASSAADIQ  kunakili habari kama hii, au inawezekanaje kwa mtu anaeipenda familia ya Mtume kusema maneno kama haya?

 

  1. Anasimulia Abii Abdillah(‘Alayhi salaam) alisimama mwanamke muovu kwa amirul muuminin akiwa juu ya  mimbari, akasema huyu ni muuaji wa wapenzi, akamuangalia, akasema kumwabia{ewe mwanamke usie jieshimu mwenye maneno machafu usie na haya unaejifanya mwana mme ambae huingii katika siku zako kama wanawake wengine, ewe ambae ninazifahamu habari zako vizuri }A-BIHARU 41/293.

 

Hivi inawezekana kwa Amirul muuminin kutamka maneno machafu kama haya?

Je inawezekana kwa Amiril- muminina kumuambia mwanamke kuwa ninazifahamu habari zako vizuri?

Na je anaweza Asadiq (‘Alayhi salaam) kunukuu maneno mabaya kama haya?, Lau kama habari hizi zingekua katika vitabu vya Ahlus Sunnah  dunia ingewaka moto wala isinge kalika na tungeli wafedhehesha vibaya, lakini yamo katika vitabu vyetu sisi mashia!

 

  1. Na  katika kitabu cha TABRISIY   kiitwacho Al-ihtijaaj, kuna maneno yasemayo  kuwa Fatma (‘Alayha salaam) alisema kumwambia Amirul muuminin (‘Alayhi salaam) {Ewe mtoo wa Abii Talib...}

 

  1. Amepokea ATABRASIY katika kitabu  AL IHTIJAJU  maelezo yanayoonyesha namna gani  ‘Umar  pamoja  na watu wengine aliokuwa nao walivyokuwa wakimkokota Amirul muuminin (‘Alayhi salaam) huku akiwa amefungwa kamba ya shingo wakamvuta nayo mpaka wakafika nae kwa Abu Bakr, kisha akaita  akisema  :Ewe mtoo wa mama, hakika watu wamenidhlilisha na wamekaribia kuniua!!

 

Nasisi tunauliza  jamani  hivi kweli  Amirul muuminin alikuwa muoga kiasi hiki?.

Hebu angalia jinsi walivyo msifu  Amirul muuminin(‘Alayhi salaam) aliposema Fatma kuhusu yeye:{Hakika wamawake wa kikuraishi walinizungumzia kuwa yeye ni mtu mwenyetumbo kubwa, mwenye mikono mirefu, mwenye miguu minene, na upara, macho makubwa, mwenye mabega mapana kama ya   ngamia, meno nje, tena faqiri (masikini)} TAFSIRUL-QUMMIYU  2/336.

Imepokewa kutoka kwa Abu Is’haq kuwa alisema:

Baba yangu aliniingiza msikitini siku ya ijumaa, akaninyanyua nikamuona Ali akikhutubu juu ya mimbari hali ya kuwa ni mzee, mwenye kipara, pajilauso limekunjana mwenye mabega mapana mwenye machokulegea} MUQATILU-TALIBINA.

        

Je  kweli hizi ndizo sifa alizo kuwa nazo Amirul muuminin   (‘Alayhi salaam)?

Mpaka hapa naona tutosheke na maelezo haya ili tuweze kuleta maelezo mengine yanayomhusu Fatma (‘Alayha salaam):

  1. Amepokea Abuu Jaafar Al-kulaiyniy katika kitabu kiitwacho Usuulul- kaafi, kuwa Fatma alimshika tai (ukosi wa shati) ‘Umar  na kumvutia, pia imeelezwa katika kitabu cha Sulaim bin Qais {kwamba fatuma (‘Alayhi salaam) alienda kwa Abu Bakar na ‘Umar kufuatilia mirathi yake wakagombana nae, nae akazugumza katikati ya watu na kupiga kelele mpaka wakakusanyika watu} uk 253.

Basi Fatma  alikua ni mlevi mpaka afanye hivi?

 

  1. Na amepokea Al Kulainiy katika kitabu kiitwacho: Alfuruui, akisema kwamba Fatma  salamu za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, hakua radhi kuolewa na ‘Ali (‘Alayhi salaam) kwa sababu baba yake siku moja aliingia nyumbani kwake na akamkuta analia, akamuuliza ni jambo gani linamliza,   Naapa kwa Mwenyezi Mungu lau angekuwepo katika jamaa zangu mtu mbora kuliko yeye nisingekuozesha kwa huyu, na mimi sie niliekuozesha lakini Mwenyezi Mungu ndie alie kuozesha. Alipoingia nyumbani kwake baba yake Fatma (yaani Mtume) akiwa ameongozana na Buraida (Fatma) alipomuona tu baba yake akatokwa na machozi, akasema (Mtume), “ni kipi  kinacho kuliza mwanangu?” Akasema {ni uchache wa chakula, na uwingi wa matatizo na huzuni}, na inasemakana kuwa Fatma alisema  katika maelezo mengine {Naapa kwa jina la Allah imezidi huzuni yangu, na kuzidi ufakiri wangu, na ugonjwa wangu umezidi kuendelea} KASHFUL-GHUMMA 1/149-150.

 

Na wamemsifu Ali (‘Alayhi salaam) sifa nyingi wakasema: {Alikuwa mweusi wa  rangi  mwenye kimo cha wastani hakuwa mfupi wala mrefu, alikuwa na tumbo kubwa, vidole vyembamba, mikono iliyojaa, miundi iliyojaa, macho malegevu, ndevu nyingi, kipara, na uso uliokunjana} MAQATILU ALTALIBINA  27.

 

Ikiwa sifa hizi ni za Amirul muuminin kama wanavyo sema inawezekana vipi mtu kuzikubali sifa kama hizi?  Basi tutosheke na maelezo haya  kwa  kutaka kufupisha, ingawa tulikuwa na hamu ya kunukuu  maelezo yaliyo pokewa kutoka kwakila mmoja miongoni mwa viongozi wetu (wa kishia)

Lakini badala yake  tukaonelea kutosheka na mapokezi matano tu yaliyo pokewa kwa kila mmoja, pia  tukaonelea maelezo yatakuwa marefu sana endapo tutanukuu mapokezi aina tano yanayomhusu Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na matano mengine yanayomhusu Amirul muuminin(‘Ali), na matano yanayomhusu Fatma tuliona maelezo hayo yatahitaji  kurasa nyingi kwa hivyo tutajitahidi kupunguza zaidi tukijaribu kuweke wazi mengi yaliyo fichika.

 

Aliandika  AL KULAINIY katika kitabu AL-USUL akinakili  kutoka katika kitabu AL KAFI: maneno yasemayo: hakika Jibrilu alimteremkia Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)  akamwambia ewe Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria mtoto atakae zaliwa na Fatma, atauliwa na umma wako baada ya  kuondoka wewe, akasema “Ewe Jibril, mpelekee mwenyezimungu salamu zangu na umuambie, sioni haja ya mtoto atakaezaliwa na Fatma kisha auliwe na umma wangu baada yangu” jibril akapanda mbinguni  kisha akashuka akasema yaleyale: “Ewe Jibrilu mpelekee mola wangu salamu na umwambie sina haja na mtoto atakaeuliwa na umma wangu baada ya kuondoka kwangu, ” akaapa Jibrilu mbinguni akateremka nakusema: Ewe Muhammad mola wako amekutolea salamu na kukubashiria kua amejaalia katika kizazi cha mtoto huyo uongozi na  wasia,  akasema (Mtume) nimeridhika, kisha Mtume akatuma mtu kwa Fatma na kumuambia kuwa Mwenyezi Mungu amenibashiria mtoto, utakaemzaa wewe kisha atauliwa na umma wangu baada ya kuondoka (kufa) kwangu, na Fatma nae akatuma mtu kwa Mtume akimwambia sina haja na mtoto atakaeuliwa na umma wako baada ya kufa kwako, Mtume akatuma tena mtu kwa Fatma akimwambia kuwa mwenyezimungu amejaalia katika kizazi chake uongozi na wasia, Fatma nae akatuma mtu akisema nimeridhika, Fatuma akabeba mimba (ya Husain) kwa taabu, na akazaa kwa taabu, na  Husain hakunyonya  kwa (mama yake) Fatma (‘Alayha salaam) wala kwa mwanamke mwingine bali  alikuwa akiletwa kwa Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)  na kumuekea kidole chake cha gumba katika mdomo wake na kunyonya kiasi kinachomtosha kwa siku mbili au tatu.

 

Hapa tunjiuliza maswali  je ni sahihi kuwa Mtume  alikuwa anaweza kukataa jambo alilobashiriwa na mwenyezimungu? Na je Fatma nae alikuwa anaweza kukataa jambo lilopitishwa na mwenyezi Mungu na  kumbashiria, kweli anaweza kufanya hivyo kwa kusema sina haja nalo?na je alibeba mimba ya Husein akiwa amemchukia, na kumzaa huku amemchukia, na je alikataa kumnyonyosha  mpaka ikafikia  aletwe kwa Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kumyonyesha kwa kidole chake cha gumba kiasi cha kumtosha siku mbili ua tatu?.

Hakika bwana wetu shahidi Husain (‘Alayhi salaam) kwa upande wake yeye haifai kusemwa maneno kama haya wala kwa upande wa mama yake kusemwa kuwa yeye alichukia kubeba mimba yake na kumzaa..kwani  wanawake wote wa dunia hii wanatamani lau kila mmoja wao angezaa  watoto kumi mfano wa  imam Al Husein(‘Alayhi salaam), vipi itawezekana kwa Bi Fatma kuchukia kubeba mimba ya  Husein na kuchukia kumzaa, na kuacha kumnyonyesha.

Katika kikao kilicho kusanya idadi kubwa ya waheshimiwa na wanafunzi wa hapa chuoni imamu ALKHUIY alizungumzia mauudhui mbalimbali kisha akamaliza maneno yake: kwa kusema Mwenyezi Mungu awalaani makafiri, tukasema ni akina nani hao? Akasema: ni wale maadui zetu (AHLUS SUNNAH), wanamtukana Husein(‘Alayhi salaam) vilevile wanawatukana Ahlu Bayt!!

Nitasema nini kumwambia imam AL KHUIY!

 

Alipo muozesha Amirul muuminin binti Yake Ummu Kulthum  kwa ‘Umar bin Al Khatwaab, alisema Abuu Jaafar al khulainiy akimnukuu Abii Abdillah(‘Alayhi salaam) kuwa ‘Umar alisema kuhusu ndoa hiyo:{hakika huo ni utupu tulio upora!!!!} FURU’UL- KAFIY 2/141.

Hapa tumuulize msemaji wa maneno haya: je ‘Umar alimuoa Ummukulthum ndoa ya kisheria au alimchukua kwa nguvu ? Maneno aliyonasibishwa kwa Assaadiq (‘Alayhi salaam) yapo wazi je anawezaje Abuu Abdillah kusema  maneno kama  yakimuhusu  mtoto wa ‘Ali (‘Alayhi salaam).

Lau ingekua kweli  ’Umar alimpora  Ummu Kulthum basi ingewezekana vipi baba yake  simba wa Mwenyezi Mungu, na mwenye ukali pia ni kijana wa kiquraishi kuridhia unyonge huu?!

 

Basi tunaposoma  kitabu kiitwacho ARRAUDHA -MINAL KAFI 8/101. katika mazungumzo  ya Abii Basyr  pamoja na mwanamke ambae alikuja kwa Abii Abdillah akiuliza juu ya (Abu Bakr na ‘Umar) akasema kumwabia unawapenda, akasema:nikikutana na mola wangu nimwambie kuwa wewe unaniamrisha kuwapenda (Umar na Abu Bakr)akasema ndio.

 

Basi mtu anaeamrisha kumpenda ‘Umar vipi atamtuhumu kuwa alimpora mwanamke katika Ahlul-Bayt?

Nilipomuuliza imam Al khuiyu kuhusu maneno ya Abii Abdillah aliyomuambia yule mwanamke kuhusu kuwapenda Abibakar na ‘Umar, akajibu kwa kusema: hakika alimuambia vile kwa  Taqiya!! (kutamka au kufanya tafauti na unavyo amini kwa kuogopa)

 

Basi na mimi namwambia Al imam Khuiy: hakika yule mwanamke ni katika mshia wa Ahlul Bayt, na Abu Basiyr ni katika jamaa wa karibu waAssadiq (‘Alayhi salaam)(kiongozi mkubwa wa kishia) kwa hiyo hapakuwa na haja yakutumia taqiyya, kama ingekuwa sahihi kufanya hivyo, lakini maneno haya ya Abul-qassim Alkhuuiy, ni kujitetea kusiko sahihi,

Kuhusu  Hassan  ameeleza  Al Mufidi katika kitabu  kiitwacho AL- irshad akiwaelezea watu wa kuufa kuwa:{waliizingira nyumba yake na wakamkamata kwa nguvu na wakamnyang’nya mswala wake aliokua amekalia akabaki ameshika upanga wake akiwa uchi (kwa maana kua walimvuwa nguo) uk190. Je atabakije Hasan(‘Alayhi salaam) akiwa hana nguo mbele ya watu?Je kusema maneno haya ndio mapenzi kwa Hassan au kashfa?

 

Na aliingia Sufian bin Abii laila kwa Hasan (‘Alayhi salaam) nae akiwa ndani mwake na kumwambia imam Hasan:{Amani iwe juu yako ewe mdhalilishaji wa waumini!akasema “una ushahidi gani juu ya

hilo”? akasema: umekabidhiwa jukumu la kuongoza umma ukajivuwa na kumuachia huyu muovo anawahukumu watu kwa sheria isiyo ya mwenyezi mungu!} RIJALUL KUSHIY uk 103.

 

Je kweli Hasan (‘Alayhi salaam)alikuwa ni mdhalilishaji wa waumini?au alikuwa ni mwenye kuwatukuza kwa kuzihifadhi damu zao, na kuwaunganisha  kwa  hekima zake, na kwa mtazamo wake ulio madhubuti?

Lau kama Hasan (‘Alayhi salaam) agepigana na  Muawiya  kwa kugombea  ukhalifa(uongozi)  basi Ingemwagika damu nyingi  ya waislamu, na wangelikufa watu wengi isinge weza Kuijuwa idadi yao, isipokua Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) na ungegawanyika umma makundi makundi, na usingeweza kusimamisha jambo lolote  wakati huo.

 

Na masikitiko makubwa ni kua maneno haya yamenasibisha kwa Abii Abdillah (‘Alayhi salaam) nina apa kwa Mwenyezi Mungu kuwa yeye yuko mbali na maneno haya na mfano wake.

 

Ama imam Assaadiq yameshampata kutoka kwa mashia maudhui mengi na kumsingizia kila aina ya uovu, tunasoma pamoja maelezo haya yafuatayo:

Imepokewa kutoka kwa Zurara kuwa  alisema:{nilimuuliza Abaa Abdillah(‘Alayhi salaam) kuhusu  Tashahhud  nikasema “Attahiyyaatu wa ssalawaatu” nae aksema kama nilivyo sema mimi basi nilipo toka nikamjambia kwenye ndevu zake, na kusema hatofaulu milele} RIJALUL KUSHIYI uk 142.

 

Ni haki yetu kumlilia kwa machozi ya damu  Imam Asadiq, anawezaje mtu kutoa maneno machafu  kama haya kwa kiongozi mkubwa kama  imam Abii Abdillah??Je inawezekana je kwa Zurara kumjambia  Abii Abdillah (‘Alayhi salaam) katika ndevu zake?! na kumwabia kuwa hatofaulu milele?

 

Hakika zimepita karne kumi toka kuandikwa kitabu cha ALKUSHIYI, na kimepita katika mikono ya wanazuoni wa mkundi mbalimbali ya kishia, sikuona yoyote kuyarudi maneno haya au kuyapinga  Mpaka  imamu Alkhuuiy wakati alipo kuwa akiandika kitabu chake kikubwa (MUUJAMU RIJALUL-HADITH) na mimi nilikua mmoja  wa waliomsaiidia  kuandika kitabu hiki, na katika kukusanya riwaya mbalimbali kutoka katika vitabu vikubwa, na tulipomsomea riwaya hii alinyamaza  kidogo, kisha akasema:kila kizuri kina kasoro na kila mjuzi anamakosa, hakuzidisha zaidi ya maneno  hayo, lakini sisi tunabaki tukijiuliza  ewe imam mtukufu, hakika  makosa huja     kwa kughafilika, au kukosea bila kukusudia, lakini kwa sababu ya uhusiano uliopo kati yangu mimi na wewe kiasi nimekuwa kama mtoto wako na umekuwa kama baba yangu, nalazimika kuyachukua maneno yako kwa nia njema lau si hivyo nisingeridhia kunyamaza kwako juu ya  udhalilishaji huu aliofanyiwa imamu Assaadiq (‘Alayhi salaam)

.

Na amesema sheikh  AL KULAINIY (amenieleza Hisham bin hakami na Hammadu kutoka kwa Zurara kuwa alisema: Nikajisemea nafsini mwangu: sheikh hajuwi  ugomvi-akimkusudia  imam wake-)

Na wameandika katika sherhe ya hadith hii: Hakika sheikh huyu ni mzee asie na akili, wala hawezi kuzungumza na maadui.   Basi je imam Al Sadiq(hana akili?)

Hakika moyo wangu umepata uchungu na huzuni kwa  sababu ya matusi haya na shutma hizi.

Na uovu huu haustahiki kwa Ahlul Bayt, inatakiwa kuwaheshimu.

 

Ama Al-Abbaas na mtoto wake Abdillah, na mtoto wake mwingine Ubaidillah na Aqiil (‘Alayhi salaam) wote hawakusalimika na matusi  na kubezwa na kusengenywa, soma nami maelezo haya: ameeleza  AL-kushiyi kuwa aya isemayo(لبئس المولى ولبئس العشير):{Ni rafiki mbaya alioje na jamaa mbaya alioje} imeteremka kumlaumu  AbasI (Radhiya Allaahu ‘anhu).( RIJALUL KUSHIYI)54,  na neno lake Mwenyezi Mungu lisemalo:

 (ومن كان في هذه أعمى فهو في الآخرة أعمى وأضل سبيلا)

{Na mwenyekua kipofu katika dunia hii na akhera atakua kipofu na mwenye kupotea njia}

Na neno lake Mwenyezi Mungu mtukufu lisemalo:

 (ولا ينفعكم نصحي إن أردت أن أنصح لكم

){Nawala hazitowafaa nasaha zangu nitapo wanasihi}zimeteremka kwake(52-53).

 

Na pia amepokea Al Kushiy kwamba Amirul muuminin(‘Alayhi salaam) aliwaombea dua mbaya  Abdillah bin Abbaas na ndugu yake Ubaidullah  akisema: (Ewe Mwenyezi Mungu walaani watoto wawili wa Fulani akikusudia  Abdullahi na Ubaydullah, na wapofoe macho yao kama ulivyo pofoa nyoyo Zao, na ujaalie kupofoka macho yao kuwa ni ushahidi wa kupofoka nyoyo zao) 52.

 

Na amepokea tegemeo la uislamu Abuu Jafar Al Kulainiy katika  kitabu cha  Alfurui kutoka Kwa  imam Al- baqir kuwa  aliesema kuhusu  Amirul muuminin: (akabakia pamoja nae watu wawili Wanyonge madhalili wageni katika uislamu, Abasu na Aqiilu)

 

Hakika aya tatu ambazo Al kushiyi amedai kuwa zimeteremka kwa ajili ya  Abbas maana yake Nikua anamuhukumu kua ni kafiri  na atakaa milele motoni siku ya Qiyama, na kama si hivyo nini basi maana ya neon lake Allah (فهو في الآخرة أعمى وأضل سبيلا)‘atakua katika akhera kipofu na mwenye  kupotea njia’?

 

Ama kuhusu Amirulul muuminin (‘Alayhi salaam) kwamba  aliwaombea vibaya watoto wawili wa  Abasi-Abdillah na Ubaydullah, kwa kuwaombea laani na upofu wa macho na moyo basi hii inatosha kuwa ni kuwakufurisha pia.

Hakika ya Abdillahi bin Abbas, Ahlu-ssunna wamembandika jina la: mafasiri wa Qur-an na mwanachuoni wa ummah, iweje sisi mashia tumlaani na huku tukidai kuwapenda Ahlul –Bayt?(jamaa zake Mtume).

Na ama Aqiilu (‘Alayhi salaam) yeye ni ndugu wa amirul muuminin (‘Alayhi salaam), Je yeye ni mdhalilifu, na ni mgeni Katika uislam?

 

Ama kuhusu  imam Ziyyinul abidina Ali bin  Husein amepokea Al Kulainiyi kwamba yazidu mtoto wa muawiya alimuomba kua mtumwa wake, akaridhika (zaynul-abidin) (‘Alayhi salaam) kuwa mtumwa wa Yazidu  alipomuambia (nimekubali uliyo yaomba, mimi ni mtumwa nilie lazimishwa kuwa mtumwa ukipenda nitumie au niuze) AL RAUDHA MINAL KAFI –8/235.

 

Angalia neno lake (zainul-abidina) na maana yake: {Nimekubali kuwa mimi ni mtumwa  kwako, na mimi ni mtumwa alie lazimishwa kuwa mtumwa kwa hiyo  ukipenda nibakishe niwe mtumwa wako, na ukitaka kuniuza niuze}hivi inawezekana imam zainul-abidina (‘Alayhi salaam) kuwa mtumwa wa Yazidu amuuze anavyotaka au amtumie anavyo taka?

 

Tukitaka kueleza maneno yote yaliyosemwa kuhusu  Ahlul Bayt basi maneno yatakua marefu kwa sababu hakuna alie salimka na maneno makali na machafu au vitendo viovu wamesingiziwa  vitendo vingi vichafu, na hayo yanapatikana  katika vitabu vyetu vinavyo tegemewa, tutakuletea baadhi ya mneno hayo katika sehemu ijao.

 

Soma nami riwaya hii ifuatayo:

 

Imeokewa kutoka kwa Abi bdillah (‘Alayhi salaam) (Kwamba Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikuwa halali mpaka aubusu uso wa Fatma) BIHAARUL-ANWAR 42/44

Na imepokewa kuwa: (Alikua (Mtume) anaweka uso wake mtukufu katikati ya chuchu mbili za Fatma) BIHARUL-ANWAR  43/78.

 

Hakika  Fatma (‘Alayha salaam) ni mwanamke aliye balehe-kufikia umri wa ukubwa- (wakati huo) basi je inaingia akilini kuweka Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) uso wake kati ya chuchu zake? Na ikiwa Mtume na mwanawe (Aaisha) wamefikiswha hapa na watu hawa (mashia) je mtu mwengine watamfikishwapi?piawamemtilia shaka imamu  Mohammad Al Qaani, Je yeye ni mtoto wa imamu Ridha au ni mtoto wa (…)             

Soma nami maelezo haya:

Imepokewa kutoka kwa Ali bin Jafar Al Baaqir kuwa aliulizwa imamu Ridhwaa (‘Alayhi salaam) 153.

{Hatujawahi kua na imamu mwenye mbadiliko ya rangi iliyochanganyika na weusi akawaambia imamu Aridhaa(‘Alayhi salaam) Je ni mtoto wangu, wakasema: hakika  Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipitisha  hukumu kwa kutumia mtaalamu wa kufuatilia nyayo na koo za watu basi  na sisi tumtumie mtaalamu huyo akasema imamu Ridhwaa nendeni mkamwite nyinyi lakini mimi hapana, na wala msiwafahamishe mnalo waitia na iwe mjumbani kwenu.

Walipokuja walitukalisha bustanini na wakawapanga mstari shangazi zake na ndugu zake wa kiume na wa kike,  kisha wakamchukuwa  Arridhwaa (‘Alayhi salaam) wakamvisha  juba la sufi na kofia yake, kisha wakamuekea kwanye shingo yake futi za kupimia kisha wakamuambia ingia kwenye bustani ujifanye kama unafanya kazi, kisha wakamleta Abu jaafari (‘Alayhi salaam) wakamuambia mkutanishe huyu mtoto na baba yake, akasema hayupo hapa babayake isipokuwa huyu ni ammi wa baba yake, (ammi ni ndugu yake baba)na huyu ni ammi yake na huyu ni shangazi yake, na kama kutakuwa na baba yake hapa basi ni huyu mwenye bustani, kwa sababu miguu yao inafanana, alipo rudi ABUL-HASSAN wakasema huyu ndie baba yake. USUULUL KAF1/322.

 

Hii ina maana kuwa walikuwa na wasiwasi yakuwa Muhammad Al Qaaniu (AMANI YA MUNGU IMSHUKIE) alikuwa ni mtoto wa Arridhwa, wakati wa kuwa Arridhwa mwenyewe anasisitiza kuwa ni mtoto wake, lakini watu wengine wanalipinga hilo na kwa sababu hiyo walisema (hatujawahi kuwa kiongozi mwenye mchanganyiko wa rangi) bila shaka hii ni kumtukana na kumvunjia heshima Arridhwa (‘Alayhi salaam) na kumtuhumu mkewe na zinaa na kuutilia mashaka uaminifu wake kwa sababu hiyo walikwenda kumleta mtaalamu wa kufananisha na kufuatilia nyayo na kutambua koo za watu, lakini mtaalamu huyo alihukumu kuwa Muhammad Al-qaaniu ni mtoto wa Arridhwa wa kumzaa, hapo waliridhika na wakanyamaza.

 

Inawezekana kutuhumiwa watu wengine mfano wa tuhuma hizi na hayo wanaweza wakayaamini watu, ama kuwatuhumu Ahlul Bayt(‘Alayhi salaam), hilo ni miongoni mwa maovu makubwa, lakusikitisha  ni kuwa vitabu vyetu vikubwa ambavyo tunadai kuwa vimenakili elimu ya Ahlul Bayt, vimejaa upotevu mfano wa upotevu huu, -hakuna ujanja wala nguvu isipokuwa kwa msada wa Mwenyezi mungu- tuliposoma maelezo haya wakati tukiendelea na masomo chuoni, wanazuoni wetu waliyapitia harakaharaka, bado nakumbuka sababu alizozitowa imamu Al-khuuiy pale alipo yapitia maelezo haya, alisema akimnukuu bwana Al-kaashiful-ghitwai: walifanya hivyo kwa kutaka kuubakisha ukoo wao ukiwa safi.

Pia walimtuhumu Arridhwa(‘Alayhi salaam) kua alikuwa akimpenda binti ya ammi yake maamuni nae pia alikua akimpenda.(angalia UYUNI AKHBAR ARIDHA) Uk

Wakambandika Ja’far, nakumuita Ja’far muongo, wakamtukana na kumtusi  pamoja na kuwa ni Ndugu yake  Al hassanil- askariyi, amesema Al kulainiyi:(jaafari ni mwenye kudhihirisha matendo maovu, mlevi, ndie mwanamme duni kuliko wote nilio waona, ni mwenye kujivunjia heshima pia ni mtu duni sana. (USUULU LKAFI)1/504

 

Basi tujiulize ni kweli katika Ahlul-Bayt kuna walevi, au mafasiqi au watu waovu?

Na tunapotaka kupata ufafanuzi zaidi,  ni juu yetu kusoma vitabu vinavyo tegemewa na Sisi (Mashia) ili tueze kujua nini kilicho semwa  kuhusu Ahlul-Bayt  wengine walio bakia amani ya mungu iwashukie, ili  tujue ni vipi waliuawa watoto wao walio twaharika na wapi waliuliwa?na ni akina nani waliowaua?

 

Wengi wao waliuawa  ndani ya miji ya Fursi kwa  mikono ya watu walio katika miji hiyo lau kama  siogopi kurefusha zaidi ya hapa basi ningetaja majina ya watu nilio wahifadhi miongonimwao na majina ya watu walio waua, lakini ninamuomba  msomaji mtukufu kukiendea  kitabu kiitwacho:  MAQATILU ATALIBYNA cha  AL-ASFAHANI, kwani kinatosha kubainisha hayo. 

 

Na ujue kuwa walio kumbana na matusi mengi zaidi na kubezwa na kusengenywa ni maimamu wawili: Muhammadul- baagir na mtoto wake Jaafar Asadiq amani ya mungu iwashukie wao na baba zao, hakika wameegemezewa mambo mengi, kutumia taqiyyah, kufanya mut’a kuwalawiti wana wake, kuazimana wanawake, na mengi mengine. Ingawa wenyewe wako mbali na hayo yote.

 

 

 

 

Share