Anajitahidi Kuwa Katika Taqwa Lakini Bado Anapenda Kutazama Machafu

 

 

Anajitahidi Kuwa Katika Taqwa Lakini Bado Anapenda Kutazama Machafu

 

Alhidaaya.com

 

Swali:

 

A/alikum mimi ni kijana wakiume na penda kusali,kusoma quran na dua kwa wingi ila yangu na penda kuangali machafu kila sapuli, naomba mnisaidie niwe katika mja mwema. 

 

Shukuran

 

Jibu: 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho. 

 

Moyo wako una maradhi sugu na dawa unayo lakini huitumii kama inavyotakiwa, kwani dawa yako kubwa ni hizo Swalah zako na kusoma Qur-aan; Swalah unazotakiwa uzitumie mara tano kwa siku yawezekana unazitumia lakini bila ya kutimiza vipimo vyake, kwa maana kuwa unaondosha jukumu au kwa maana kuwa unainama na kuinuka bila ya Swalah kukuathiri au bila ya wewe kuathirika na Swalah zako.

 

Swalah umeifanya kama ni moja kati ya desturi au mazoezi ambayo ni ya kila siku na sio ‘Ibaadah yenye kutegemewa kukukurubisha kwa Allaah na yenye kukupelekea kujikataza na maovu yako na machafu ya kila sampuli unayopenda kuangalia. 

 

Ndugu yetu unapenda kuswali –kama ulivyosema- au unaswali, unasoma Qur-aan na kadhalika lakini tulichoamrishwa Waislamu sio kuswali tu bali ni kusimamisha Swalah, tulichoamrishwa si kusoma Qur-aan tu bali tabia zetu ziwe Qur-aan na hicho ndio ambacho huna kwani kama ulikuwa unasimamisha Swalah kama tulivyoamrishwa basi Allaah Anatuambia:

 

اتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ وَأَقِمِ الصَّلَاةَ ۖ إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ ۗ وَلَذِكْرُ اللَّـهِ أَكْبَرُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ ﴿٤٥﴾

Soma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uliyoletewa Wahy katika Kitabu na simamisha Swalaah, hakika Swalaah inazuia machafu na munkari. Na bila shaka kumdhukuru Allaah ni kubwa zaidi. Na Allaah Anajua yale mnayoyatenda. [Ankabuwt:45]

 

Hivyo, tunakushauri usimamishe Swalah kikamilifu na kwa kufanya hivyo bila shaka utajikuta unayaogopa na kujitenga na maasi, kadhalika, isome Qur-aan kwa kuifahamu na kwa mazingatio, na kwa kufanya hivyo utaweza kujua yaliyokatazwa katika maasi na utakuwa unayakimbia kila yanapokusogelea. Jitahidi kusikiliza mawaidha ya Dini kila mara na jiepushe na kuwa na faragha ambazo hakuna la maana unalofanya ndani yake. Hayo yote In shaa Allaah kwa idhini ya Allaah, yataweza kukusaidia kuwa mja mwema na kuwa mbali na machafu.

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi: 

 

Nataka Kutubu Lakini Shaytwaan Kanivaa Nifanye Nini?

 

Hatari Ya Kuchelewa Kuomba Maghfira Na Tawbah

 

Anaomba Toba Kisha Anarudia Tena Kufanya Kosa Kila Mara. Vipi Aweze Kuimarika Bila Kurudi Makosani?

 

Inaruhusiwa Kutazama Picha Za Uchafu Kwa Ajili Ya Kujitayarisha Na Ndoa? 

 

Kijana Anaishi Nchi Zenye Maasi Mengi, Anajaribu Kujizuia Anaomba Toba Kila Mara Anasumbuliwa Na Khofu Aliyonayo

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share