Steki Nyama Kondoo Ya Sosi Tamu/Kali Ya Nanaa, Ukwaju Na Jamu Ya Marmalade (Machungwa)
Steki Nyama Kondoo Ya Sosi Tamu/Kali Ya Nanaa, Ukwaju Na Jamu Ya Marmalade (Machungwa)
Vipimo
Steki ya nyama ya kondoo (Lamb steak) - 3- 4 LB
Vitunguu vya majani (spring onions) - 5 miche
Kitunguu saumu (thomu/galic) - 7 chembe
Pilipili mbichi - 5-6
*Sosi ya nanaa ya tayari - 2 vijiko vya supu
Jam ya marmalade (machungwa) - 2 vijiko vya supu
Ukwaju ulokamuliwa - 1 kikombe cha chai
Jiyra/cummin/bizari ya pilau - 1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Safisha nyama iache ichuje maji weka kando.
- Weka katika mashine ya kusagia, vitunguu vya majani, pilipili mbichi, kitunguu thomu, chumvi na nusu ya ukwaju, kisha saga hadi ilainike .
- Mimina katika kibakuli, kisha changanya na sosi ya nanaa, jam ya marmalade, ukwaju ulobakia na jiyra/cummin/bizari ya pilau ya unga.
- Weka kando sosi kiasi ya ¼ kikombe. Changanya ilobakia katika nyama vizuri, kisha iache ikolee kwa muda wa kiasi masaa 3 nje au zaidi ya masaa katika friji.
- Weka katika treya ya oveni kisha uoke (bake) kwa moto wa 430° - 450° kwa muda wa saa 1 takriban hadi nyama iwive. (muda na moto inategemea na aina ya nyama).
- Epua kisha pakaza sosi ilobakia kisha rudisha katika oveni moto wa kuchomea (grill) na iache ichomeke kwa muda wa dakika 2 tu takriban huku unaigeuza.
- Epua ikiwa tayari kuliwa na mkate au wali.
Kidokezo:
Ikiwa hupati sosi ya nanaa ya tayari dukani, unaweza kutumia majani ya nanaa kiasi ya misongo 3 (bunches). Saga pamoja na viungo katika mashine ya kusagia na uongeze ukwaju kidogo.