Mwanamke Anasumbuliwa Na Kutokwa Na Ute Kwa Miaka Mingi, Afanyeje?

SWALI:

 

Asalam alaykum,

Napenda kumshukuru mnyezi mungu na kumtakia rehma mtume wake Muhammad (S.W.A) kwa kunipa afya, napenda kuuliza swali kwamba mimi nina mtihani mkubwa sana, kuhusu kujitwaharisha tangia nimekuwa msichana nikiwa na umri wa miaka 14, kila siku mara kwa mara, utukwa na kitu kama mkojo lakini sio mkojo wa kawaida kwani ni kama ute ute ambao ni mzito mzito, hapa nashindwa kuelewa unaponitoka natakiwa kujitwarihirisha kwani ni kila siku mara kwa mara au ni hali ya kawaida kwa mwanamke.


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kusumbuliwa kwako na ute unaokutoka kwa miaka mingi sasa.

Hakika ni kuwa unyevunyevu ambao unawatoka wanawake ni kitu cha kawaida kabisa. Kwa hiyo kutokwa na huo ute hakuna tatizo kabisa isipokuwa ikiwa kinachotoka ni manii au madhii.

 

Ikiwa ni kama ulivyouliza, basi kutakuwa hakuna haja kishari’ah kujitwahirisha kama mtu mwenye janaba. Hivyo jambo kama hilo lisikutie wasiwasi na kukosesha raha. Ukifika wakati wa Swalaah unaweza kujiosha sehemu hizo na kisha ukachukua Wudhuu wako lakini hilo si lazima ila ni bora kufanya hivyo kwa usafi wako na kuchunga usafi wa unayemsimamia mbele yako wakati wa Swalaah zako.

 

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate manufaa zaidi:

 

Tofauti Baina Ya Manii Na Madhii Na Hukumu Zake Za Ghuslu

 

Hukmu Ya Wadii Na Madhii

 

Mwanamke Akitokwa Na Majimaji, Je, Aoge Janaba?

 

Ni Lazima Kujisafisha Sehemu Za Siri Unapotaka Kufanya Wudhuu?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share