Dada Anayetaka Kusilimu, Watoto Awafanye Nini Ili Wasichukuliwe Na Baba Yao Asiyetaka Wawe Na Mama Yao?

SWALI:

 

Asalamu Aleikum Warahmatullah Wabarakatu,

Kwa hakika nina furaha sana kwa mtandao wenu na kwa kadri munavyo yajibu mswali kwa ustadi na umakinifu, Inshalla Mungu atawawezesha muwe na moyo huo huo kwani sikazi ndogo munayo ifanya kuwaelisha umaa. Allaha bariq fee.

Suala langu ni, Kuna dada mmoja mkristo alijaaliwa kuwa na toto wa 3 na alikua akiishi na mumu wake Mkristo, kwa sasa hivyo wame kosana na mumuwe kwa matatizo yao yakinyumbani, mke amempeleka mume kortini ili amuachie watoto na ampe talaka, Sasa dada kama huyu ana sema yeye sasa anataka kusilimu na aolewe na muislamu kinacho msumbua zaidi ni watoto kwa sababu yeye akisilimu je watoto itakuaje? Kwa sababu anaogop baba ya watoto anaweza kuja kuchuka watoto na awapeleke kwa familia yake (Baba) ili waepukane na mama yao kwa sababu amesilimu, je jambo kama hili utampa dada huyu Ushauri gani? Naomba jibu kadri ya uwezo wenu.

Shukran.


 

JIBU: 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. 

Shukrani kwa swali lako kuhusu dada anayetaka kusilimu.

Mwanzo jambo la kusilimu halifai kucheleweshwa kabisa, inafaa mumsilimishe mwanzo na auweke Uislamu wake kuwa ni siri huku akingojea uamuzi wa mahakama ili umkabidhi yeye watoto.

Akishakabidhiwa watoto, afanye juhudi ya kuwapeleka kwa haraka katika Madrasah nzuri au amuite mwalimu nyumbani kuwafundisha. Watoto hao wakipata elimu ya Uislamu pamoja na kuingiwa na Imani itakuwa si rahisi kwa baba kuweza kuwachukua kwani watoto wenyewe hawatokubali kabisa jambo hilo.

Na hata baba akiweza kuwachukua watoto wake, hilo halitakuwa katika uwezo wake yey huyo dada na hivyo hatoadhibiwa na Allaah kwa hilo bali atapata thawabu kwa juhudi zake. 

Fanyeni hima katika hilo na kwa ajili ya Niyah yenu na yake njema Allaah Aliyetukuka Atakuwa pamoja naye.

 

Na Allaah najua zaidi

 

Share