Mchuzi Wa Samaki Nguru Na Bilingani Za Kukaanga
Mchuzi Wa Samaki Nguru Na Bilingani Za Kukaanga
Vipimo Vya Samaki
Samaki Nguru 4-5 vipande
Pilipilimbichi ilosagwa 1 kijiko cha supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa 1 kijiko cha supu
Tangawizi mbichi ilosagwa 1 kijiko cha supu
Bizari ya samaki 1 kijiko cha chai
Paprika (pilipili nyekundu ya unga ilokoza) 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Ndimu ¼ kikombe
Vipimo vya mchuzi
Bilingani 2 ya kiasi
Vitunguu (katakata chopped) 2 vikubwa
Nyanya/tungule (katakata chopped) 3
Nyanya kopo (paste) 2 vijiko vya supu
Chumvi kiasi
Ndimu kavu/lumi 1
Mafuta (ya kukaangia) kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Samaki
- Changanya viungo vyote vya samaki upake katika vipande vya samaki, vikolee.
- Weka kwenye treya ya oveni, na choma (grill) huku unageuza samaki hadi wageuka rangi na karibia kuiva.
- Epua samaki weka kando.
- Masalo yatakayobakia katika treya weka katika kibakuli kidogo.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Mchuzi
- Weka mafuta katika karai yapate moto vizuri.
- Katakata bilingani vipande vya mraba (cubes) kisha kaanga katika mafuta hadi vigeuke rangi. Epua katika chujio bilingai zichuje mafuta.
- Weka mafuta kiasi ya vijiko 3 vya supu katika sufuria, tia vitunguu kaanga hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (golden brown).
- Tia nyanya/tungule, nyanya kopo (tomato paste) endelea kukaanga.
- Tia maji kidogo, kisha tia samaki na masala yaliyobakia, tia chumvi.
- Pasua lumu (ndimu kavu) vipande kiasi 3-4 tia na uache mchuzi uchemke kidogo bila ya kuvurugika samaki
- Epua tayari.