Adhkaar Katika Rukuu Na Sujuud

Adhkaar Katika Rukuu Na Sujuwd

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalaam alaykum alaykum alhidaaya, kwanza samahani kwa kuuliza maswali kwani siruhusiki kwa majibu ya maelezo lkn sheikh nakuomba unitowe wasiwasi kama utapata muda ili nijuwe vipi ibada yangu naitekeleza sahihi ama na hasa mwezi huu mtukufu isije ikawa nafanya ibada kumbe nakwenda kinyume. 

 

Moja, ni kuhusu adhkar za rukuu na sujudu nimeona ktk hiswnul muslim wameandika kwa namba, je mie natakiwa nizisome zote kama za sujudu au nichague moja halikadhalika na rukuu.

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Adhkaar za Sunnah katika Swalaah  zinapatikana katika Kitabu cha Hiswnul-Muslim, pamoja na za kurukuu na kusujudu nazo ni katika viungo vifuatavyo:

 

Nazo zinapatikana katika viungo vifuatavyo. Bonyeza usome na usikilize Adhkhaar hizo:

 

017-Hiswnul-Muslim: Du’aa Za Wakati Wa Kurukuu

 

 018-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kuinuka Kutoka Kenye Rukuu

 

 019-Hiswnul-Muslim: Du’aa Za Wakati Wa Kusujudu

 

020-Hiswnul-Muslim: Du’aa Za Kikao Kati Ya Sijdah Mbili

 

Ukiweza kuzihifadhi zote zitakusaidia katika kisimamo cha kuswali usiku ambacho kinapaswa kuwa kirefu katika kila hali.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share