048-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Faida Muhimu Kuhusu Kumswalia Mtume Wa Ummah ‘Swalaatu 'Alan-Nabbiyy’ - (Faida ya Tatu, Nne, Tano Na Sita)

Faida Ya Tatu

 

Msomaji pia atagundua kuwa katika aina zote hizi za kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), hakuna neno la 'as siyad' (bwana), na kwa sababu hiyo Maulama waliokuja mwisho wamekhitilafiana kuhusu hukmu ya kuingiza neno hili –Sayyidinaa/Bwana wetu- katika Swalah ya Ibraahiymiyyah. Kutokana na upungufu wa nafasi, hatutoingia katika kuchambua kauli wala kutaja waliokataa jambo hili kwa kushikamana na kufuata mafunzo kamili ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Ummah wake alipoulizwa vipi kumswalia (صلى الله عليه وآله وسلم). Akajibu hali kuwa anaamrisha kwa kusema: ((Semeni, Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad…….)). Lakini napenda kuwanukulia wasomaji rai ya Al-Haafidhw bin Hajar Al-'Asqalaaniy katika hayo, tukizingatia kuwa yeye ni mmoja wa Maulamaa wakubwa wa Ki-Shaafi'iy waliokusanya baina ya Hadiyth na Fiqh. Imeenea kwa waliokuja mwisho katika ash-Shaafi'iyyah kwenda kinyume na mafunzo haya ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). 

Al-Haafidhw Muhammad bin Muhammad bin Muhammad Al-Ghuraabiyly (790-835 AH) mwenziwe Ibn Hajr amesema na nimenukuu kutoka mswada wake.([1])

Aliulizwa (Ibn Hajr) - Allaah Atunufaishe kwa maisha yake - kuhusu namna ya kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Swalah au nje ya Swalah, sawa sawa kama imesemwa ni wajibu au inapendekezeka. Je, ni sharti mojawapo kuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) asifiwe kwa ubwana, mfano mtu kusema: 'Allaahumma Swalli 'alaa Sayyidinaa Muhammad...', au 'sayyidil-khalq' (bwana wa viumbe), au 'sayyid walad Aadam' (bwana wa watoto wa Aadam)?" Au mtu afupishe kwa kusema: 'Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad"? Na ni ipi katika mbili hizi ni bora zaidi; kulitamka neno la 'sayyid' kwa vile ni sifa iliyothibiti kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), au kutoitamka kwa vile halijapokewa katika mapokezi?

(Ibn Hajr رضي الله عنه) akajibu:

"Ndio, kushikamana na matamshi yaliyopokewa, ndio ni bora zaidi, na wala pasisemwe kuwa labda Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ameacha hivyo –hakujiita mwenyewe sayyid- kwa sababu ya unyenyekevu wake (صلى الله عليه وآله وسلم), kama alivyoacha  (صلى الله عليه وآله وسلم) kujiswalia (صلى الله عليه وآله وسلم) anapotaja jina lake, ingawa Ummah wake wamehimizwa kufanya hivyo kila anapotajwa (صلى الله عليه وآله وسلم). Kwani sisi tunasema, kama ingelikuwa hivyo ni bora, basi ingelipokelewa kutoka kwa Maswahaba kupitia Mataabi'yna, lakini hatukupata hata kukutana na cho chote kile katika yaliyopokewa kutokana na mmoja miongoni mwa Maswahaba wala Mataabi'yna waliowafuata. Akasema: Juu ya wingi wa hayo yaliyopokewa kutokana na wao kuhusiana na hilo. Na huyu hapa Imaam Ash-Shaafi'iy, Allaah Ampandishe daraja yake, ni miongoni mwa watu wenye kumuheshimu Mtume  (صلى الله عليه وآله وسلم)  zaidi.  Amesema katika utangulizi wa kitabu chake ambacho ni tegemezi kwa watu wa madhehebu yake:  'Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad….' hadi mwisho wa ilipomfikisha juhudi yake, nayo ni kauli yake: 'kila wanapomkumbuka  wanaomkumbuka, na kila wanapoghafilika kumkumbuka wanaoghafilika', kama kwamba ametoa hayo kutokana na Hadiyth Swahiyh ambayo ndani yake kuna: ”Subhaana Allaahi 'adada Khalqihi”. Imethibiti kuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwambia Mama wa Waumini alipomuona amekithirisha at-tasbiyh na akarefusha: ((Umesema maneno ambayo lau yangelipimwa katika mizani kwa hivyo ulivyosema, basi mizani yake itakuwa nzito)). Alikuwa  (صلى الله عليه وآله وسلم)  akipendezwa na kuomba du'aa zilizokuwa fupi lakini zikiwa nzito katika maana.

Al-Qaadhwi 'Iyaadhw ameweka mlango katika namna za kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) katika kitabu chake Ash-Shifaa (Kitabu cha Tiba). Amenukuu ndani yake mapokezi mar-fuu’an -usimulizi wa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) - kutoka kwa kundi la Maswahaba na Mataabi'iyn. Na hakuna katika yote hayo au kutoka kwa yeyote yule miongoni mwa Swahaba na wengineo tamshi la 'sayyidinaa'. Miongoni mwa hayo mapokezi ni:

 

a)                Hadiyth ya 'Aliy kwamba alikuwa akiwafundisha namna ya kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kusema:

 

اللَّهُمَّ دَاحِي الْمَدْحُوَّات وَبَارِئ الْمَسْمُوكَات اِجْعَلْ سوابق صَلَوَاتك وَنَوَامِي بَرَكَاتك زائد تَحَنُّنِك عَلَى مُحَمَّد عَبْدك وَرَسُولِك الْفَاتِح لِمَا أُغْلِقَ

 

Allaahumma Daahiy al-Mad-huwaat, wa Baari al-Masmuukaat, Ij-'Al-Sawaabiq Swalahwaatak, wa Nawaamiy BaRak’ahtak, wa Zaaid Tahiyyaatak 'alaa Muhammad 'Abduka wa Rasuulak, Al-Faatih Limaa Ughliq'

 

“Ee Allaah! Mtandazaji wa ardhi, Mwanzishi wa mbingu, Zijaalie Swalah Zako bora kabisa zilizojaa rutuba ya Baraka Zako na yote mema yaliyozidi, kwa Muhammad, Mja (wako) na Mjumbe (wako), mfunguaji wa yaliyofungwa”.

 

b)                Na kutoka kwa 'Aliy pia, alikuwa akisema:

 

صلواتُ اللهِ البرِّ الرحيمِ والملائكةِ المقرّبين والنبيّينَ والصدّيقينَ والشهداءِ الصَّالحين، وما سبح لك من شيء يا رب العالمين، على محمّدِ بنِ عبدِ الله خاتمِ النبيّينَ وإمامِ المتقين

 

'Swalawaatu-LLaahil-Barrur-Rahiym, wal-Malaaikatil-Muqarrabiyn, wan-Nabiyyiyn was-Swiddiyqiyn was-Shuhadaais-Swaalihiyn, wa Maa Sabaha Laka min shayin Yaa Rabbal-'Aalamiyn, 'alaa Muhammad Ibn 'Abdillaahi Khaatamin-Nabiyyiyn wa Imaamil-Mutaqqiyn…' n.k.

 

“Swalah za Allaah Mhisani Mkunjufu wa rehema, na za Malaika walio karibu Naye, na Mitume na Wasema kweli na Mashahiyd na watu wema, na kila kinachosabbih kwa ajili Yako ewe Mola wa walimwengu wote, juu ya Muhammad bin 'Abdillaah mwisho wa Manabii na kiongozi wa wamchao Mungu”.

 

c)                 Kutoka kwa 'Abdullaah bin Mas'uud ambaye alikuwa akisema:

 

اللَّهُمَّ اجْعَلْ صَلَوَاتِكَ وَبَرَكَاتِكَ وَرَحْمَتَكَ عَلَى مُحَمَّدٍ إمام الخيروَرَسُول الرحمة

 

Allaahummaj-'Al-Swalahwaatika wa BaRak’ahtik, wa Rahmataka 'alaa Muhammad 'Abdika wa Rasuulik, Imaamil-Khayr wa Rasuulir-Rahmah…

 

“Ee Mola zijaalie Swalah Zako na Baraka Zako na Rehma Zako juu ya Muhammad kiongozi wa wema na Mtume wa Rehma”.

 

d)      Kutoka kwa Hasan Al-Baswriy ambaye alikuwa akisema: "Anayetaka kunywa katika kikombe kinachokata kiu kutoka hawdh (chemchem) ya Mustwafaa, aseme:

 

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِهِ وَأَصْحَابِهِ وَأَزْوِاجِهِ وأولاده وَذُرَّيَّاتِهِ وأهل بيته وَأًصْهَارِهِ وَأَنْصَارِهِ وَأَشْيَاعِهِ وَمُحِبِّيهِ

 

'Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aailihi wa Aswhaabihi, wa azwaajihi, wa awlaadihi wa dhurriyaatihi wa ahli baytihi wa aswhaarihi wa answaarihi wa ashyaa'ihi wa muhibbihi'

 

“Ee Mola Mswalie Muhammad na Aali zake na Swahaba zake na Wake zake na Wanawe na Vizazi vyake na Watu wa nyumba yake na Shemeji na wakwe zake na Waliomnusuru na Wenzake na Wapenzi wake”

 

Hivyo ndivyo (Al-Qaadhwiy 'Iyaadhw) alivyoandika katika Ash-Shifaa kuhusu namna ya kumswalia Mtume kutoka kwa Maswahaba na waliowafuatia na akataja mengineyo.

 

Ndio, imesimuliwa katika Hadiyth ya Ibn Mas'uud kwamba kumswalia kwake kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisema:

 

اللَّهُمَّ اجْعَلَ فَضَائِلَ صَلَواتِكَ ورَحْمَتِكَ وَبَرَكَاتِكَ علَّى سَيِّدِ المرْسَلِينَ

 

'Allaahummaj-'Al-fadhwaail Swalahatak wa Rahmatak wa BaRak’ahtak 'alaa Sayyidil-Mursaliyn…

 

Imesimuliwa na Ibn Maajah, lakini isnaad yake ni dhaifu kwa hiyo Hadiyth ya 'Aliy iliyosimuliwa na At-Twabaraaniy ikiwa na isnaad inayokubalika inaongoza. Hadiyth hii ina maneno magumu ambayo nimeyataja na kuelezea katika kitabu Fadhwl An-Nabbiy (Ubora wa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)) cha 'Abdul Hasan Ibn Al-Faaris. Baadhi ya Mashaafi'iy wamesema kwamba mtu akiapa kwa kumswalia Swalah Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) Swalah bora kabisa ili kutekeleza kiapo chake iwe:

 

اللهم صَلَّ الله عَلَى مُحَمَّدٍ كُلَّما ذَكَرَهُ الذَّاكِرُونَ وسها  عَنْ ذِكْرِهِ الْغَافَلُونَ

 

'Allaahuuma Swalli 'alaa Muhammad kullamaa dhakarahudh-dhaakiruun, wa sahaa 'an dhikrihil-ghaafiluun'

 

An-Nawawy kasema: "Inayopasa kutekelezwa ni kusema:

 

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى ‏ ‏مُحَمَّدٍ ‏وعلى َآلِ ‏ ‏مُحَمَّدٍ ‏ ‏كَمَا صَلَّيْتَ عَلَى ‏إِبْرَاهِيمَ.....

 

Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad, kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym …

 

Maulamaa wengi wa mwishoni wamejibu hii, kwa kusema kwamba hakuna dalili inayothibitisha kuhusu aina mbili zilizotajwa kuhusu ubora katika usimulizi. Am kuhusu maana basi ya mwanzo ndio bora.   

Mas-ala haya ni mashuhuri katika vitabu vya Fiqh, na Maulamaa wote wa Fiqh waliozungumzia mas-ala haya kwa pamoja hawajanukuu neno la 'sayyid'. Ingelikuwa neno hili limependekezwa, lisingeliwakwepa wote hata wawe wameghafilika. Mazuri yote ni kufuata waliyosimulia na Allaah Anajua zaidi"

 

Rai ya Ibn Hajar ya kutokukubali kumsifia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa 'usayyid' (ubwana) ni kutokana na amri ya Qur-aan, na hii pia ni rai ya Maulamaa wa Kihanafi. Ni rai ipasayo kufuatwa kwani ndio udhihirisho mkweli wa mapenzi yake  (صلى الله عليه وآله وسلم),

â ö@è% bÎ) óOçFZä. tbq™7Åsè? ©!$# ‘ÏRqãèÎ7¨?$$sù ãNä3ö7Î6ósムª!$# á

((Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Allaah basi nifuateni mimi, Allaah Atakupendeni)) [Aal-I’mraan – 31]

 

Kwa sababu hii, Imaam An-Nawawy amesmea katika Rawdhwatut-Twaalibiyn (1/265): "Swalah iliyo kamilifu kabisa ya kumswaliwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ni:

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى ‏ ‏مُحَمَّدٍ

'Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad…"

 

inayowafikiana aina ya 3 iliyotajwa ambayo haikutajwa sayyid.

 

 

Faida Ya Nne

 

Itambulike kwamba aina ya 1 na ya 4 ndizo Mjumbe wa Allaah  (صلى الله عليه وآله وسلم) alizowafundisha Maswahaba walipomuuliza kuhusu vipi kumswalia, kwa hiyo hii imetumika kama ni dalili kwamba hizi ndizo bora kabisa za kumswalia kwani asingeliwachagulia au kujichagulia mwenyewe isipokuwa kilicho bora na utukufu. Imaam An-Nawawy kama ilivyotajwa, amenukuu (katika Radhwatut-Twaalibiyn) kwamba kama mtu anataka kuapa kwa kumswalia Swalah bora kabisa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), basi haiwezi kutimizwa isipokuwa kwa njia hizi.

 

As-Subkiy ametoa sababu nyingine: "Yeyote anayemswalia kwa Swalah hizi basi amemswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa yakini na atakayemswalia kwa maneno mengine, ameingia katika mashaka au hakutimiza kumswalia kama ipasavyo kwa sababu waliuliza: "Vipi tukuswalie?" Alijibu: "Semeni: …" Hivyo wakiilezea Swalah yao kwake kama kauli yao kadhaa na kadhaa. Hii imetajwa na Al-Haytamiy katika Ad-Darr Al-Mandhwuud (25/2) kisha akasema, (27/1) kwamba lengo linapatikana katika aina zote zilizokuja katika Ahaadiyth Swahiyh.

 

 

Faida Ya Tano

 

Ijulikane kwamba sio shari’ah kuunganisha aina zote hizi kuwa ni aina moja ya Swalah, hali kadhalika Tashahhud zote zilizotolewa kabla, kwani hiyo itakuwa ni bid'ah (uzushi) katika dini; Sunnah ni kusema mara hivi mara vile katika nyakati mbali mbali kama Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah alivyoelezea katika utafiti wake wa Takbiyr za 'Iyd mbili (Majmuu' Al-Fataawa 29/253/1)

 

 

Faida Ya Sita

 

'Allaamah Swiddiyq Hasan Khaan amesema katika kitabu chake Nuzuul Al-Abraar bil 'Ilm Al-Manthuur minal-Ad'iya wAl-Adkhaar, baada ya kutoa Hadiyth nyingi kuhusu fadhila za kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na kukithiri katika kumswalia (Uk. 161):

"Hakuna shaka kwamba wengi miongoni mwa Waislamu wanaomswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Ahlul-Hadiyth (wenye kufuata Hadiyth sahihi) na wasimulizi wa Sunnah iliyotwahirika, kwani ni mojawapo wa kazi yao katika elimu hii sharifu kumswalia kablaa ya kila Hadiyth, kwa hiyo ndimi zao zimerutubika daima kwa kumtaja  (صلى الله عليه وآله وسلم). Hakuna kitabu cha Sunnah au mkusanyo wa Hadiyth; ikiwa ni Jaami', Musnad, Mu'jam, Juz'u n.k ila imekusanya maelfu ya Hadiyth, hata kilichokuwa cha chini yao kabisa kwa uzito; Jaami' As-Saghiyr cha As-Swuyuutiy, kilichokuwa na Hadiyth elifu kumi na hivyo ndivyo ilivyo katika vitabu vyote vya elimu ya hadiyth. Hivyo hawa ni makundi waliookoka, na Jamaa wa Hadiyth ambao watakaokuwa karibu kabisa na Mjumbe wa Allaah  (صلى الله عليه وآله وسلم) siku ya Qiyaamah, na ndio watakaofurahi kwa shifaa (ombolezi) yake   (صلى الله عليه وآله وسلم), mama yangu na baba yangu wawe fidia kwake. Fadhila hii ya watu wa Hadiyth haiwezi kushindwa ya yeyote mwingine ila afanye kama wafanyavyo na zaidi, jambo ambalo takriban haliwezekani. Kwa hiyo Ee mpenda kheri, mtafutaji kuokoka, vyovyote ilivyo, unapaswa uwe Muhaddith au uwe karibu na Muhaddithiyn; usiwe vinginevyo…. Kwani mbali na hivyo hakuna kitakachokunufaisha".

Namuomba Allaah (سبحانه وتعالى)  anifanye miongoni wa watu hawa wa Hadiyth, ambao ni miongoni mwa watu waliokaribu kabisa na Mjumbe wa Allaah  (صلى الله عليه وآله وسلم), na labda kitabu hiki kitakuwa ni ushahidi kwayo. Allaah Amerehemu Imaam Ahmad aliyesema:

Dini ya Muhammad iko katika usimulizi

Kipando bora kwa vijana ni Sunnah athari zake

Usizigeukie nyuma Hadiyth na watu wake

Kwani rai ni usiku na Hadiyth ni mchana

Kijana anaweza kuwa mjinga wa uongofu….

Ingawa jua linang'ara katika mwanga wake!

 



[1] Iliyohifadhiwa katika Maktaba ya Adhw-Dhwaahiriyyah Damascus.

 

Share