057-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Hitimisho

 

 

Hitimisho

 

Yote yaliyotangulizwa humu kuhusu sifa ya Swalah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) yanawahusu wanamume na wanawake, na wala haikuthibiti katika Sunnah kwamba kuna baadhi ya mambo yanamtofautisha (inayomtenga) mwanamke, bali inahikisha kauli ya ujumla ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم):

((Swalini kama mlivyoniona nikiswali)).

 

Hivyo imejumuisha wanawake wote, na kauli ya Ibraahiym An-Nakha'iy amesema: "Mwanamke anafanya kama anavvyofanya mwanamume katika Swalah" [Imetoka kwa Ibn Abi Shaybah (1/75/2) ikiwa na isnaad Swahiyh kutoka kwake]

 

Al-Bukhaariy amesimulia katika At-Tariykh As-Swaghiyr (Uk. 95) ikiwa na isnaad Swahiyh kutoka kwa Umm Ad-Dardaa: "Alikuwa akikaa katika Swalah yake kikao cha wanaume na alikuwa ni Faqihi"

 

Ama Hadiyth inayosema mwanamke ajikunje katika Sujuud na kwamba yeye sio sawa na mwanamume, ni Hadiyth Mursal haina hoja. [Amesimulia Abu Daawuud katika Al-Maraasil] (117/87) kutoka kwa Yaziyd Ibn Abi Habiyb ambaye ametolewa katika Adh-Dwa'iyfah (2652).

Ama ile aliyosimulia Imaam Ahmad katika Masaail (ya mwanawe) Ibn 'Abdullaah kutoka kwake, (Uk.71) kutoka kwa Ibn 'Umar kwamba alikuwa akiwaamrisha wanawake waketi kimarufaa, (Hadiyth hii) haisihi isnaad yake kwa sababu yumo 'Abdullaah bin Al-'Amriy ambaye dhwa’iyf.

 

********

 

 

Haya ndiyo yaliyowezekana kukusanya pamoja katika kuelezea Sifa Ya Swalah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) Kutoka Takbiyr Hadi Tasliym. Natumai kwamba Allaah Ataijaalia iwe yenye ikhlaasw mbele ya Uso Wake Mkarimu na uongofu kwa Sunnah ya Mtume Wake Raufur-Rahiym (…Mpole)

 

سُبْحـانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ سُبْحَانكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْك.  اللّهُـمَّ صَلِّ عَلـى مُحمَّـدٍ وَعَلـى آلِ مُحمَّدٍ. وَبارِكْ عَلـى مُحمَّـدٍ  وَعَلـى آلِ مُحمَّـد  كَمـا صَلَّيْتَ وَبارَكْتَ عَلـى إبْراهيم وَآلِ إبْراهـيمَ إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد

 

Subhaana-Llaahi wa-Bihamdihi, Subhaanaka Llaahumma wa-Bihamdika, ash-hadu an laa ilaaha illa Anta, Astaghfiruka wa atuwbu Ilayka, Allaahumma swalliy ‘alaa Muhammad, wa ‘alaa aali Muhammad, wa Baarik ‘alaa Muhammad, wa ‘alaa aali Muhammad, kama Swallayta wa Baarakta ‘alaa Ibraahiyma, wa aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydum-Majiyd.

 

“Ametakasika Allaah, na sifa njema zote ni zake. Kutakasika ni kwako Ee Allaah, na sifa njema zote ni Zako. Nakiri kwamba hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, nakuomba msamaha na ninarejea Kwako.

Ee Allaah, Mswalie Muhammad na jamaa zake Muhammad, na Mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad kama Ulivyomswalia na Ukambariki Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym hakika Wewe ni mwenye kusifika Mtukufu”([1])

 

 

 

 

 



[1] Du'aa ya mwanzo ni du'aa kamili inayojulikana kama Kaffaaratul-Majlis

(kafara ya kikao): ((Atakayeisema katika mkusanyiko wa kumkumbuka (Allaah) itakuwa kama ni mhuri wa kuchapia, na atakayesema katika mkusanyiko wa maneno ya kipuuzi, itakuwa kama ni kafara yake)) [Imeripotiwa na Al-Al-Haakim na Atw-Twabaaraniy ikiwa Swahiyh]. Du'aa ya pili ni Sunnah kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Du'aa hizi mbili hivyo ni njia bora kabisa katika kutekeleza miongozo ya Kiislamu. ((Hapana watu wowote wale wanaokaa kikao chochote bila ya kumtaja Allaah, wala kumswalia Mtume ila itakuwa dhambi kwao, Allaah Akipenda Atawaadhibu, au Akipenda Atawasamehe)) [Imesimuliwa na At-Tirmidhy, Al-Al-Haakim, Ahmad ikiwa Swahiyh] Taz. Silsilatu Al-Haadiyth As-Swahiyhah cha Shaykh Al-Albaaniy (74/81) kwa maelezo.

Share