Kuku Wa Karai Na Viazi (Pakistani)
Kuku Wa Karai Na Viazi (Pakistani)
Vipimo
Kuku - 1 mkubwa
Mafuta ya kukaangia viazi - kiasi
Kotmiri iliyokatwakatwa- 2 misongo (bunches)
Methi/fenugreek seeds/uwatu - ¼ kijiko cha chai
Haldi/tumeric/bizari ya manjano - ½ kijiko cha chai
Jiyra/cummin/uzile/bizari ya pilau - 1 kijiko cha chai
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7 chembe
Viazi/mbatata - 3
Nyanya/tungule- 6 - 7
Tangawizi mbichi - 1 kipande kiasi
Pilipili mbichi iliyosagwa- 1 kijiko cha chai
Ndimu - 1
Chumvi - kiasi
Mafuta ya kupikia - ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Mkate kuku vipande vipande vya kiasi. Mwoshe vizuri kwa chumvi na siki atoke harufu mbayaa.
- Menya viazi/mbatata kisha katakata vipande vipande vya mraba (cubes)
- Katakata nyanya ndogondogo (chopped), Chuna tangawizi mbichi na kitunguu thomu, katakata kotimiri (chopped) weka kando.
- Weka mafuta katika karai, kaanga viazi/mbatata hadi viive kisha epua vichuje mafuta. Weka mafuta kando.
- Weka mafuta ¼ kikombe katika karai weka katika moto yashike moto. Kisha tia tangawizi mbichi, kitunguu thomu, bizari zote. Kakaanga haraka kidogo tu.
- Tia vipande vya kuku na kakaanga achanganyike na masala.
- Tia nyanya/tungule, chumvi, pilipili mbichi iliyosagwa endelea kukaanga na kufunika hadi kuku aive na itokee sosi ya nyanya.
- Tia ndimu, changanya, kisha mwagia viazi, changanya.
- Mwagia kotmiri ikiwa tayarii kuliwa kwa wali mweupe au aina yoyote ya mikate.