Du'aa Ya Tashahhud Katika Swalaah Ipi Sahihi?
Duaa Ya Tashahhud Katika Swalaah Ni Ipi Sahihi?
SWALI:
Assalamu alykum,
tulifundishwa madrasa kusema (attahiyatu, almubarakatu, aswalawatu,
atwayibathu lillah....) je hivi ni makosa, maana maagizo yanasema
(atahiyatu lillah, waswalawatu, watwayibatu..)
JIBU:
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
At-Tashahhud katika Swalaah ziko aina kadhaa. Hivyo ulivyotaja huenda umekosea katika kuzitamka kwa hiyo ingia katika viungo vifuatavyo upate maelezo yake kwa maandishi na kwa kusikiliza ili uweze kujifunza kuzitamka kwa usahihi:
022-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Tashahhud
023-Hiswnul-Muslim :Kumswalia Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Baada Ya Tashahhud
Zimetajwa pia katika Swiffatusw-Swalaah ya Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu-Allaah) ambazo zinapatikana katika viuongo vifuatavyo:
Pia bonyeza kiungo kifuatacho:
Na Allaah Anajua zaidi