Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan
Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan
Jina Lake Na Kuzaliwa Kwake:
Jina lake ni Swaalih bin Fawzaan bin 'Abdillaah Al-Fawzaan na kazaliwa 1354 (1933) H.
Malezi Yake Na Masomo:
Baba yake alifariki wakati bado yu mdogo, kwa hivyo alikulia katika familia ya baba yake na kujifunza Qur-aan na kusoma na kuandika na ‘Ulamaa katika mji wake. Ndipo akaanza kusoma katika Madrasah ya serikali katika mji wake mwaka 1379 H. Baadaye aliendelea na masomo yake katika Madrasah ya Buraydah katika mwaka wa 1371 H. Kisha akasoma katika kituo cha kujifunza Buraydah kilichoanza kati ya 1373 H hadi 1377 H. Kisha akaendelea na masomo yake katika fani ya Shariy´ah Riyaadh na akahitimu mwaka 1381 H.
Baada ya hapo akaendelea kusoma shahada ya pili kisha ya tatu ya udaktari katika Fiqh.
Waalimu Wake:
1) Shaykh 'Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz, Muftiy wa Saudi Arabia aliotangulia. Shaykh Ibn Baaz alikuwa na uaminifu sana na Shaykh Al-Fawzaan na alikuwa akimpa vitabu mbalimbali avipitie na kmtaka rai yake.
2) Shaykh 'Abdullaah bin Humayd, mkuu wa mahakama ya juu kabisa katika Baraza la Saudi Arabia huko nyuma. Alikuwa akihudhuria katika darsa zake nyingi alipokuwa akisoma Buraydah.
3) Shaykh Muhammad Amiyn Ash-Shanqiytwiy, mfasiri bingwa wa Qur-aan wa zama zetu.
4) Shaykh 'Abdur-Razzaaq Al-'Afifiy Mwanachuoni kutoka Misri aliyekuwa katika Baraza la Kudumu la Kutoa Fatwa Saudi Arabia chini ya Muftiy wa wakati huo, Imaam Ibn Baaz.
Kazi Zake:
1) Alikuwa mwalimu katika Madrasah ya Buraydah na Riyaadh, baada ya hapo akaajiriwa kama mwalimu katika kitivo cha Shariy´ah.
2) Alikuwa Mudiyr wa Chuo kikuu cha U-Qaadhiy Riyaadh mwaka 1396 H.
3) Amekuwa mjumbe wa baraza la ‘Ulamaa wakubwa katika mwaka 1407 H Saudi Arabia.
4) Amekuwa mjumbe wa baraza la Fatwa Saudi Arabia katika mwaka wa 1411 H.
5) Ni mjumbe wa baraza la Fatwa Makkah la Raabitwat-ul-´Aalam Al-Islaamiy.
6) Ni Imaam, mwalimu na Khatwiyb wa Ijumaa katika msikiti wa Amiyr Mutw'ib bin 'Abdil-´Aziyz, huko Riyaadh.
7) Anajibu maswali katika kipindi cha Radio cha ‘Nuwr 'Alaa Ad-Darb’ katika kituo cha Saudi cha Redio.
8) Alikuwa mshauri na msimamizi katika mitihani mingi ya kitaaluma katika ngazi za shahada ya pili na udaktari.
Vitabu Vyake:
Shaykh ameandika vitabu vingi na wanafunzi wake huwa wanaandika mihadhara yake ya sauti. Miongoni mwa vitabu hivyo ni:
1) I'aanat ul-Mustafiyd sharh kitaab At-Tawhiyd. Maelezo ya kina ya Kitaab-ut-Tawhiyd, mijalada miwili.
2) Al-Mulakhasw-ul-Fiqhi. Kitabu kifupi na maarufu cha Fiqh kinachofundishwa duniani kote.
3) At-Tahqiyqaat Al-Mardiyyah fiyl-Mabaahith Al-Fardiyyah fiyl-Mawaariyth. Moja ya vitabu maarufu katika Shariy´ah ya Kiislamu cha Miyraath katika zama hizi kinachofundishwa katika Chuo kikuu cha Kiislamu.
Chanzo: Mukhtasari utangulizi wa kitabu cha Al-Ajwibah Al-Mufiydah ´an As-ilatil-Manaahij Al-Jadiydah (ukurasa 14-18) na Jamaal bin Fur.