Katlesi Za Kuku Mviringo Wa Yai
Katlesi Za Kuku Mviringo Wa Yai
Vipimo na namna ya kutayarisha
Mbatata/viazi Chemsha - 2 Kilo
Kuku safisha, osha katakata vipande - ½
Mayai Piga kwa uma (fork katika kibakuli) - 3
Vitunguu maji katakata vidogodogo (chopped) - 2
Pilipili shamba/mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha chai
Ndimu/limau Kamua - 1 au mbili
Pilipili manga - ½ kijiko cha chai
Tangawizi mbichi Saga - 1 kipande
Kitunguu thomu (saumu) Saga - 7 – 10 chembe
Uzile/bizari nyembamba/ya pilau/cumin Saga - 2 vijiko vya chai
Bizari ya mchuzi ukipenda = 1 kijiko cha chai
Kotmiri majani osha, katakata (chop) = 1 kikombe
Chenga za mkate (Bread crumbs) Weka katika sahani ya chali - 1 kikombe
Namna Ya Kupika:
- Menya mbatata/viazi
- Chemsha kuku kwa tangawizi na kitunguu thomu, ndimu, au limau mpaka akauke
- mchambue kuku mtoe mifupa
- Ziponde mbatata katika bakuli mpaka zivurugike.
- Changanya vizrui na mbatata/viazi, kuku na viungo vyote vinginevyo isipokuwa chenga za mkate na mafuta, na mayai
- Fanya madonge uviringe kama shepu ya yai.
- Chomva katlesi ndani ya mayai halafu karagiza kwenye bread crumbs.
- Weka mafuta yashike moto, zitie katelsi mpaka zigeuke rangi ya dhahabu zitowe tayari kwa kuliwa.