007-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Kwa Yepi Waja Wamejua Yale Anayoyapenda Na Kuyaridhia Allaah?
200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
007-Kwa Yepi Waja Wamejua Yale Anayoyapenda Na Kuyaridhia Allaah?
Swali:
بماذا عرف العباد ما يحبه الله ويرضاه ؟
Kwa yepi waja wamejua yale Anayoyapenda Allaah (سبحانه وتعالى) na kuyaridhia?
Jibu:
ج: عرفوه بإرسال الله تعالى الرسل وإنزاله الكتب آمرا بما يحبه الله ويرضاه ناهيا عما يكرهه ويأباه وبذلك قامت عليهم حجته الدامغة, وظهرت حكمته البالغة قال الله تعالى (رسلا مبشرين ومنذرين لئلا يكون للناس على الله حجة بعد الرسل) وقال تعالى (قل إن كنتم تحبون الله فاتبعوني يحببكم الله ويغفر لكم ذنوبكم والله غفور رحيم )
Wamejua kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kuleta Rusuli na kuteremsha Vitabu Akiamrisha Anayopenda Allaah, kuyaridhia, kukataza Asiyoyapenda na kuyachukia. Na kwa sababu hiyo, hoja zenye nguvu zilisimama juu yao, na hikmah Yake Allaah (سبحانه وتعالى) ikadhihirika kwa kusema:
رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿١٦٥﴾
Rusuli ni wabashiriaji na waonyaji ili pasikuweko kutoka kwa watu hoja yoyote juu ya Allaah baada ya (kuletwa) Rusuli. Na Allaah daima ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [An-Nisaa: 165]
Pia Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾
Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Aal-‘Imraan: 31]