009-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Niyyah Ya Kweli Ni Ipi?
200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
009-Niyyah Ya Kweli Ni Ipi
Swali:
ما هو صدق العزيمة؟
Ni ipi hiyo niyyah ya kweli?
Jibu:
ج: هو ترك التكاسل والتواني وبذل الجهد في أن يصدق قوله بفعله قال الله تعالى (يا أيها الذين آمنوا لم تقولون ما لا تفعلون كبر مقتا عند الله أن تقولوا ما لا تفعلون)
Hayo ni kuacha uvivu na kuakhirisha akhirisha (mambo) na kutoa juhudi katika kusadikisha kauli yake na vitendo vyake. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٢﴾
Enyi walioamini! Kwanini mnasema yale msiyoyafanya?
كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٣﴾
Ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya.
[Asw-Swaff: 2-3]