012-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Dini Ya Kiislamu Ina Daraja Ngapi?

 

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

012-Dini Ya Kiislamu Ina Daraja Ngapi

 

 

 

 

Swali:

 

كم مراتب دين الإسلام

 

Dini ya Kiislamu ina daraja ngapi?

 

 

Jibu:

 

 هو ثلاث مراتب الإسلام والإيمان والإحسان وكل واحد منها إذا أطلق شمل الدين كله.

 

Dini ya Kiislamu ina darajja tatu nazo ni: Uislamu, Iymaan, na Ihsaan na kila fungu katika hayo matatu linapoachwa linakusanya mafungu yote ya Dini.

 

 

Hadiyth inayothibitisha hayo:

 

عَن عُمَر رضي اللهُ عنه:  أبَيْنَما نَحْنُ جُلْوسٌ عِنْدَ رسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ذات يَوْم  إذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَجُلٌ شَدِيدُ بَياضِ الثِّيَاِبِ شَديدُ سَوَادِ الشَّعْرِ، لا يُرَى عليه أَثَرُ السَّفَرِ ولا يَعْرِفُهُ مِنَّا أَحَدٌ، حَتى جَلَسَ إلى النَّبِّي صلى الله عليه وسلم، فأسْنَدَ رُكْبَتَيْهِ إلى رُكْبَتَيْهِ ووَضَعَ كَفَّيْهِ على فَخِذَيْهِ، وقال: يا محمَّدُ أَخْبرني عَن الإسلامِ، فقالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((الإسلامُ أَنْ تَشْهَدَ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمِّداً رسولُ الله، وتُقِيمَ الصَّلاةَ، وتُؤتيَ الزَّكاةَ، وتَصُومَ رَمَضان، وتَحُجَّ الْبَيْتَ إن اسْتَطَعتَ إليه سَبيلاً)). قالَ صَدَقْتَ. فَعَجِبْنا لهُ يَسْأَلُهُ ويُصَدِّقُهُ، قال : فَأَخْبرني عن الإِيمان. قال: ((أَن تُؤمِنَ باللهِ، وملائِكَتِهِ وكُتُبِهِ، ورسُلِهِ، واليَوْمِ الآخِرِ، وتُؤمِنَ بالْقَدَرِ خَيْرِهِ وشَرِّهِ)) قال صدقت. قال : فأخْبرني عَنِ الإحْسانِ. قال:(( أنْ تَعْبُدَ الله كَأَنَّكَ تَرَاهُ فإنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فإنَّهُ يَرَاك)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ  

Kutoka kwa 'Umar (رضي الله عنه)  ambaye amesema: Siku moja tulikuwa tumekaa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) , hapo alitokea  mtu ambaye  nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama  ya machofu ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi aliyemtambua. Alienda akakaa karibu na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaweka magoti yake karibu na magoti yake na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake kisha akasema; Ee Muhammad! Niambie kuhusu Uislamu.  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Uislamu ni kukiri kuwa hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa  Allaah na Muhammad ni Rasuli Wake, kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah, kufunga (Swawm) za Ramadhaan na kutekeleza Hijjah  kwa mwenye uwezo)) Akasema (yule mtu yaani Jibriyl) – “Umesema kweli”. Tulipigwa na mshangao kwa kumuuliza  kwake Nabiy na kumsadikisha.  Na akasema tena: Niambie  kuhusu Iymaan.  Akasema: ((Ni kumwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Rusuli Wake na Siku ya Qiyaamah, na  kuamini ya kuwa kheri na shari zinatoka Kwake)). Akasema: “Umesema kweli”. Akasema: “Hebu nielezee kuhusu Ihsaan”.  Akasema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): (( Ni kumwabudu Allaah kama vile unamuona na kama humuoni basi Yeye Anakuona…)) [Muslim]

 

 

Share