014-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Dalili Ipi Inayojulisha Kujumuisha Mojawapo Ya Nguzo Za Kiislamu

 

  200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

014-Dalili Ipi Inayojulisha Kujumuisha Mojawapo Ya Nguzo Za Kiislamu

 

 

 

 

Swali:

 

   ما الدليل على شموله الدين كله عند الإطلاق

Ni ipi dalili inayojulisha kujumuisha mojawapo ya mafungu hayo (ya Dini Ya Kiislamu) kuwa ndio Dini yote?

 

 

Jibu:

 

 

ج: قال الله تعالى  (إن الدين عند الله الإسلام) وقال النبي صلى الله عليه وسلم  (بدأ الإسلام غريبا وسيعود غريبا كما بدأ) وقال صلى الله عليه وسلم   (أفضل الإسلام إيمان بالله) وغير ذلك كثير.

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

 

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ ۗ

Hakika Dini mbele ya Allaah ni Uislamu [Aal-‘Imraan: 19]

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

 

 ((بَدَأَ الإِسْلامُ غَرِيبًا ، وَسَيَعُودُ كَمَا بَدَأَ غَرِيبًا...))

((Uislamu ulianza ukiwa mgeni na utaondoka ukiwa ni mgeni kama ulivyoanza)). [Muslim, Kitaabul-Iymaan Juz 145]

 

Na akasema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

((أفضل الإسلام إيمان بالله))

((Uislamu bora kwa mtu ni kumwamini Allaah)) [Ahmad 4/114, Atw-Twabaraniy katika Al-Kabiyr kutoka katika Hadiyth ya ‘Amru bin ‘Absa, al-Haythamiy katika kitabu chake ‘Al-Mujma’ (1/63) kuwa watu waliopokea ni thiqah (waaminifu)]

 

 

Share