Makosa Katika Ufahamu Wa Hukmu Za Wudhuu
Makosa Katika Ufahamu Wa Hukmu Za Wudhuu
Imetarjumiwa Na: Abu 'Abdir-Rahmaan Sulaymaan
1 – Wapo baadhi ya watu wanasema huwezi kutia Wudhuu huku ukiwa uko uchi.
Mwanachuoni 'Abdul-'Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
"Kufunika tupu (uchi) wako si katika nguzo za Wudhuu [Kwa mfano kuchukua Wudhuu ukiwa bafuni unaoga]."
[Fatawa Ibn Baaz 10/101]
2 – Kuna wanaodhania kwamba kutanguliza kuosha kiungo cha mkono wa kushoto kwanza kabla ya kulia kwa kusahau ni makosa wakati unatia Wudhuu.
Imam An-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
"Wamekubaliana Wanachuoni kuwa kuanza kutia Wudhuu viungo vya mkono wa kulia na kufuatia mkono wa kushoto ni Sunnah, lakini ukianza mkono wa kushoto kabla ya kulia pia Wudhuu huo unakubalika."
[Sharh Swahiyh Muslim 3/10]
3 – Watu wengi hunyanyua kidole wakati wakitamka shahaadah wakati wa kusoma du'aa ya kumaliza kuchukua Wudhuu.
‘Allaamah Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Siijui asli yake kitendo hicho.
[Fataawa Nuwr 'Alaa Ad-Darb 8/117]
4 – Kuna baadhi ya watu wanasema ukigusa najisi itakubidi urudie kutia Wudhuu tena!
‘Allaamah Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
‘Kukanyaga najisi wakati bado kibichi/kimajimaji hakitengui Wudhuu wako, Hata hivyo, mtu anatakiwa kusafisha, na hapa inakusudiwa ni kusafisha pale palipoingia najisi hiyo tu.’
[Fataawa Ibn 'Uthaymiyn 2/119]
6 – Watu wengi huona tabu kupangusa kwenye soksi zenye tundu wakati wanatia Wudhuu.
‘Allaamah Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
"Inajuzu kufuta juu ya soksi hata kama ina matundu na pia kupangusa juu ya Khuff nyepesi (soksi za ngozi), kwa sababu Maswahaba wengi walikuwa maskini, na kwao ni kawaida kukuta wamevaa Khuff zenye matundu."
[Fataawa Ibn 'Uthaymiyn 11/116]
7 – Kuna baadhi ya watu wanapangusa soksi wakati wanachukua wudhuu, soksi hizo zina mapicha ya viumbe vyenye roho.
‘Allaamah Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
‘Haijuzu kupangusa soksi zenye picha ya mnyama, kwani kupangusa juu ya Khuff inajuzu lakini si katika kumuasi Allaah."
[Fataawa Ibn 'Uthaymiyn 11/116]
Na sifa zote Anastahiki Allaah, na Rahmah na amani za Allaah ziwe juu ya Mtume wetu wa mwisho Muhammad, familia yake, na Maswahaba zake na wote watakaomfuata.