16-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Ukilala Ukiamka Utamke Neno La Tawhiyd
Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd
16-Ukilala Ukiamka Utamke Neno La Tawhiyd
Mafundisho ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yanatujulisha kuwa jambo la kwanza la kufanya unapoamka ni kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa Tawhiyd (kumpwekesha), na kwamba fadhila zake ni kutakabaliwa mtu haja zake:
عَنْ عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنْ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَنْ تَعَارَّ مِنْ اللَّيْلِ فَقَالَ: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوْلَ ولاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ. ثُمَّ قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي أَوْ دَعَا اسْتُجِيبَ لَهُ, فَإِنْ عَزَمَ فَتَوَضَّأَ ثُمَّ صَلَّى قُبِلَتْ صَلَاتُهُ))
Kutoka kwa ‘Ubaadah bin Swaamit (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeamka usiku akasema: “Laa ilaaha illa-Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-Hamdu wa-Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr, wa Subhaana-Allaah wal-HamduliLLaah walaa ilaaha illa-Allaah wa-Allaahu Akbar walaa hawla walaa quwwata illa biLLaah” (Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Pekee Hana mshirika, Ufalme ni Wake na Himdi ni Zake Naye ni Mweza wa kila kitu. Ametakasika Allaah, na Himdi ni za Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Allaah ni Mkubwa kabisa, hapana uwezo wala nguvu ila za Allaah), kisha akasema: “Rabbigh-fir-liy” [ee Allaah, nighufurie] au akaomba, ataitikiwa. Na akiazimia kutawadha na kuswali atatakabaliwa Swalah yake)). [Al-Bukhaariy na wengineo]
Na katika Swalaah ya Sunnah ya Alfajiri ambayo ni rakaa mbili unatakiwa usome, Suwratul-Kaafiruwn (109) na Suwratul-Ikhlaasw (112) na [Suwratul-Baqarah 2: 136], [Suwratul-‘Imraan 3: 84].
Adhkaaar na Nyiradi za asubuhi zote zimetaja Tawhiyd (Rejea Kitabu cha Hiswnul Muslim kinapatikana ndani ya alhidaaya.com), vilevile ndani ya Swalaah tunatamka Tawhiyd ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Kadhaalika unapotaka kulala ni Sunnah usome, Suwratul-Ikhlaasw (112), Al-Mu’awidhataan (113, 114) ambazo zinasomwa pia katika Swalaah ya Witr pamoja na Suwratul-Kaafiruwn (109), Aayatul-Kursiyy 2: 255), na Aayah mbili za mwisho za [Suwratul-Baqarah 2: 285- 286], Suwratul-Mulk (67) Suwratus-Sajdah (32) na pia adhkaar mbali mbali za wakati wa kulala. Baadhi ya hizo adhkaar ni kama zifuatazo:
Hadiyth ya Al-Baraaa bin ‘Aazib (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((إِذَا أَتَيْتَ مَضْجَعَكَ فَتَوَضَّأْ وُضُوءَكَ لِلصَّلَاةِ، ثُمَّ اضْطَجِعْ عَلَى شِقِّكَ الْأَيْمَنِ، ثُمَّ قُلْ: اللّهُـمَّ أَسْـلَمْتُ نَفْـسي إِلَـيْكَ، وَفَوَّضْـتُ أَمْـري إِلَـيْكَ، وَوَجَّـهْتُ وَجْـهي إِلَـيْكَ، وَأَلْـجَـاْتُ ظَهـري إِلَـيْكَ، رَغْبَـةً وَرَهْـبَةً إِلَـيْكَ، لا مَلْجَـأَ وَلا مَنْـجـا مِنْـكَ إِلاّ إِلَـيْكَ، آمَنْـتُ بِكِتـابِكَ الّـذي أَنْزَلْـتَ وَبِنَبِـيِّـكَ الّـذي أَرْسَلْـت. ((فَإِنْ مُتَّ مِنْ لَيْلَتِكَ فَأَنْتَ عَلَى الْفِطْرَةِ، وَاجْعَلْهُنَّ آخِرَ مَا تَتَكَلَّمُ بِهِ))
((Utakapofika kitandani mwako [kutaka kulala] tawadha wudhuu kama wa Swalaah kisha lalia ubavu wako wa kulia kisha sema:
Allaahumma aslamtu nafsiy Ilayka, wa fawwadhwtu amriy Ilayka, wa wajjahtu waj-hiya Ilayka, wa alja-tu dhwahriy Ilayka, raghbatan warahbatan Ilayka. Laa malja-a walaa manjaa Minka illaa Ilayka. Aamantu Bikitaabikal-ladhiy Anzalta wabi Nabiyyikal-lladhiy Arsalta.
Ee Allaah, nimeisalimisha nafsi yangu Kwako, na nimekuachia mambo yangu Wewe na nimeuelekeza uso wangu Kwako na nimeutegemeza mgongo wangu Kwako, kwa matajarajio na kwa kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa ila Kwako. Nimekiamini Kitabu Chako Ulichokiteremsha na Nabii Wako uliyemtuma.
((Ukifariki usiku huo utafariki katika fitwrah [maumbile ya asli ya Tawhiyd], na ifanyeni iwe ya [dhikri] ya mwisho kuisoma)). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Kadhaalika adhkaar ya kulala iliyotajwa katika Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ni:
اللّهُـمَّ رَبَّ السّمـواتِ السَّبْـعِ وَرَبَّ العَـرْشِ العَظـيم، رَبَّنـا وَرَبَّ كُـلِّ شَـيءٍ، فالِـقَ الحَـبِّ وَالنَّـوى، وَمُـنَزِّلَ التَّـوْراةِ وَالإنْجـيلِ والفُـرْقانِ. أَعُـوذُ بِـكَ مِن شَـرِّ كُـلِّ شَـيءٍ أَنْـتَ آخِـذٌ بِنـاصِـيَتِهِ. اللّهُـمَّ أَنْـتَ الأوَّلُ فَلَـيسَ قَبْـلَكَ شَيءٌ، وَأَنْـتَ الآخِـرُ فَلَـيسَ بَعْـدَكَ شَيءٌ، وَأَنْـتَ الظّـاهِـرُ فَلَـيْسَ فَـوْقَـكَ شَيءٌ، وَأَنْـتَ الْبـاطِـنُ فَلَـيْسَ دونَـكَ شَيءٌ، اقـْضِ عَنّـا الـدَّيْـنَ وَأَغْـنِنـا مِنَ الفَـقْرِ
((Allaahumma Rabbas-samawaatis-sab’-i wa Rabbal-’Arshil-’Adhwiym. Rabbanaa wa Rabba kulli shay-in. Faaliqal-habbi wan-nnawaa, wa munzilat-Tawraati wal-Injiyli wal-Furqaan. A’uwdhu Bika minsharri kulli shay-in Anta Aakhidhun binaaswiyatihi. Allaahumma Antal-Awwalu falaysa Qablaka shay-un. Wa Antal-Aakhiru falaysa Ba’-daka shay-un. Wa Antadh-Dhwaahiru falaysa Fawqaka shay-un. Wa Antal-Baatwinu falaysa Duwnaka shay-un. Iqdhwi ‘annad-dayna waghninaa minal-faqri.
Ee Allaah, Rabb wa mbingu saba na Rabb wa ’Arshi Tukufu. Rabb wetu na Rabb wa kila kitu. Mpasuaji wa mbegu na kokwa (zikawa miche) na Aliyeteremsha Tawraati na Injiyl na Qur-aan. Najikinga Kwako kutokana na shari ya kila kitu. Wewe Ndiye Mwenye kukamata utosi wake. Ee Allaah Wewe Ndiye wa Mwanzo hakuna kitu kabla Yako. Nawe Ndiye wa Mwisho hakuna kitu chochote baada Yako. Nawe Ndiye Uliye juu hakuna kitu chochote juu Yako. Nawe Ndiye Uliye karibu hakuna kitu chochote kilicho karibu kuliko Wewe, Tulipie madeni yetu na Utuepushe na ufakiri)) [Muslim]
Na pindi unapokosa usingizi ukawa unajigeuzageuza kitandani, utasoma yaliyomo katika Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa):
لا إِلـهَ إِلاّ اللهُ الـواحِدُ القَهّـار، رَبُّ السَّـمواتِ وَالأرْضِ وَما بَيْـنَهـما، العَزيـزُ الغَـفّار
Laa ilaaha illa-Allaahul-Waahidul-Qahhaar. Rabbus-samawaati wal-ardhwi wamaa baynahuma, Al-’Aziyzul-Ghaffaar.
Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Al-Waahid (Mmoja Pekee) Al-Qahhaar (Mshindi Mwenye kudhibiti na kudhalilisha). Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo kati yake, Al-’Aziyz (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima) Al-Ghaffaar (Mwingi wa kughufuria). [Al-Haakim na ameisahihisha Adh-Dhahabiy (1/540), An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [864] na Ibn As-Sunniy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [757]. Na tazama Swahiyh Al-Jaami’ (4/213) [4693].
Unapoamka kuswali Tahajjud ni Sunnah kusoma Suwratul-’Imraan (3:190-200). Pia adhkaaar zifuatazo:
Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) imetajwa adhkaar ifuatayo:
اللّهُـمَّ رَبَّ جِـبْرائيل، وَميكـائيل، وَإِسْـرافيل، فاطِـرَ السَّمواتِ وَالأَرْض، عالـِمَ الغَيْـبِ وَالشَّهـادَةِ أَنْـتَ تَحْـكمُ بَيْـنَ عِبـادِكَ فيـما كانوا فيهِ يَخْتَلِفـون. اهدِنـي لِمـا اخْتُـلِفَ فيـهِ مِنَ الْحَـقِّ بِإِذْنِك، إِنَّـكَ تَهْـدي مَنْ تَشـاءُ إِلى صِراطٍ مُسْتَقـيم
Allaahumma Rabba Jibraaiyla wa Mikaaiyla wa Israafiyla, faatwiras-samaawaati wal ardhw, ’Aalimal ghaybi wash-shahaadah, Anta Tahkmu bayna ’ibaadika fiymaa kaanuw fiyhi yakhtalifuwn. Ihdiniy limakhtulifa fiyhi minal haqqi bi-idhnika Innaka Tahdiy man Tashaau ilaa swiraatwil-mustaqiym.
Ee Allaah, Rabb wa Jibiriyl na Mikaaiyl na Israafiyl, Mwanzishi wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa mambo ya ghayb na yaliyo wazi, Wewe Unahukumu baina ya waja Wako katika mambo ambayo walikuwa wakitofautiana. Niongoze mimi kwenye haki katika yale ambayo (watu) wametofautiana kwa idhini Yako. Hakika Wewe unamuongoza Umtakae kwenye njia ilionyoka. [Muslim]
Kadhaalika Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) imetajwa adhkaar ifuatayo:
اللّهُـمَّ لَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ نـورُ السَّمـواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فيـهِنَّ، وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ قَـيِّمُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فيـهِنَّ، (وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ رَبُّ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فيـهِنَّ) (وَلَكَ الْحَمْدُ لَكَ مُلْـكُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فيـهِنَّ) (وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ مَلِـكُ السَّـمواتِ وَالأَرْضِ) (وَلَكَ الْحَمْدُ) (أَنْتَ الْحَـقُّ وَوَعْـدُكَ الْحَـقُّ، وَقَوْلُـكَ الْحَـقُّ، وَلِقـاؤُكَ الْحَـقُّ، وَالْجَـنَّةُحَـقُّ، وَالنّـارُ حَقُّ، وَالنَّبِـيّونَ حَـقُّ، وَمـحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم حقُّ، والسَّاعَةُ حَـقُّ) (اللّهُـمَّ لَكَ أَسْلَمتُ، وَعَلَـيْكَ تَوَكَّلْـت، وَبِكَ آمَنْـت، وَإِلَـيْكَ أَنَبْـتُ، وَبِـكَ خاصَمْتُ، وَإِلَـيْكَ حاكَمْـتُ، فاغْفِـرْ لي مـا قَدَّمْتُ، وَما أَخَّـرْتُ، وَما أَسْـرَرْتُ، وَما أَعْلَـنْتُ) (أَنْتَ المُقَـدِّمُ وَأَنْتَ المُـؤَخِّر، لاَ إلَهَ إِلاّ أَنْـت) (أَنْـتَ إِلـهي لا إلَهَ إِلاّ أَنْـت)
Allaahumma Lakal-Hamdu Anta Nuwrus-samaawati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hamdu Anta Qayyimus-samaawaati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hamdu Anta Rabbus-samawaati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hamdu Laka Mulkus-samaawaati wal ardhwi waman fiyhinna. Walakal-Hamdu Antal-Haqqu, wawa’dukal-haqqu, waqawlukal-haqqu, waliqaaukal-haqqu, wal-Jannata haqqun, wannaaru haqqun, wannabiyyuwna haqqun, wa Muhammadun SwallaAllaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam haqqun, was-saa’atu haqqun. Allaahumma Laka aslamtu, wa ’Alayka tawakkaltu, wabika aamantu, wa Ilayka anabtu, wabika khaaswamtu, wa Ilayka haakamtu, faghfir liy maa qaddamtu wamaa akh-khartu, wamaa asrartu, wamaa a’lantu, Antal-Muqaddimu wa Antal-Muakh-khiru laa ilaaha illa Anta. Anta Ilaahiy laa ilaaha illa Anta.
Ee Allaah, Himdi ni Zako, Wewe Ndiye Nuru ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na Himdi ni Zako, Wewe Ndiye sababu ya kusimama kwa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na Himdi ni Zako, Wewe Ndiye Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake; na Himdi ni Zako, Wewe Ndiye Mfalme wa mbingu na ardhi, na Himdi ni Zako, Wewe ni haki [kweli] na ahadi Yako ni ya kweli, na neno Lako ni la kweli, na kukutana na Wewe ni kweli, na Jannah ni kweli, na Moto ni kweli, na Manabii ni kweli, na Muhammad SwallaAllaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam ni kweli, na Qiyaamah ni kweli. Ee Allaah, Kwako nimejisalimisha, na kwako nimetawakali, na Wewe nimekuamini, na Kwako nimerejea kutubia.
Na kwa ajili Yako (au kwa hoja na dalili Zako) nimetetea (maadui Wako). Na nimeelekea Kwako kukufanya Wewe ni Hakimu Wangu (kuhukumu baina yetu). Basi nighufurie niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza; Wewe Ndiye Al-Muqaddimu (Mwenye kutanguliza) na Al-Muakh-khiru (Mwenye kuchelewesha), hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe; Wewe Ndiye Mwabudiwa wangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe. [Al-Bukhaariy]