012 - Yuwsuf

 

  يُوسُفْ

 

012-Yuwsuf

 

012-Yuwsuf: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿١﴾

1. Alif Laam Raa.[1] Hizi ni Aayaat za Kitabu kinachobainisha.

 

 

 

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٢﴾

2. Hakika Sisi Tumekiteremsha kikisomeka kwa (lugha ya) Kiarabu ili mufahamu.

 

 

 

نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ بِمَا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ هَـٰذَا الْقُرْآنَ وَإِن كُنتَ مِن قَبْلِهِ لَمِنَ الْغَافِلِينَ ﴿٣﴾

3. Sisi Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) simulizi nzuri kabisa katika Tuliyokufunulia Wahy hii Qur-aan. Na japokuwa kabla yake ulikuwa miongoni mwa wasiojua.[2]

 

 

 

إِذْ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ إِنِّي رَأَيْتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوْكَبًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ رَأَيْتُهُمْ لِي سَاجِدِينَ ﴿٤﴾

4. Pale Yuwsuf[3] alipomwambia baba yake: Ee baba yangu kipenzi! Hakika mimi nimeona (njozini)[4] nyota kumi na moja na jua na mwezi,[5] nimeziona zikinisujudia.

 

 

 

قَالَ يَا بُنَيَّ لَا تَقْصُصْ رُؤْيَاكَ عَلَىٰ إِخْوَتِكَ فَيَكِيدُوا لَكَ كَيْدًا ۖ إِنَّ الشَّيْطَانَ لِلْإِنسَانِ عَدُوٌّ مُّبِينٌ﴿٥﴾

5. Akasema: Ee mwanangu! Usisimulie njozi yako kwa kaka zako watakupangia njama. Hakika shaytwaan kwa mwanaadam ni adui bayana.

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ يَجْتَبِيكَ رَبُّكَ وَيُعَلِّمُكَ مِن تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ وَيُتِمُّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَعَلَىٰ آلِ يَعْقُوبَ كَمَا أَتَمَّهَا عَلَىٰ أَبَوَيْكَ مِن قَبْلُ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٦﴾

6. Na hivyo ndivyo Atakavyokuteua Rabb wako na Atakufunza tafsiri ya khabari (kuhusu ndoto na matukio) na Atakutimizia Neema Yake juu yako, na juu ya kizazi cha Ya’quwb, kama Alivyoitimiza kabla juu ya baba zako wawili; Ibraahiym na Is-haaq. Hakika Rabb wako Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

لَّقَدْ كَانَ فِي يُوسُفَ وَإِخْوَتِهِ آيَاتٌ لِّلسَّائِلِينَ﴿٧﴾

7. Kwa yakini kuna Aayaat (Mazingatio, Dalili, Mawaidha) katika (kisa cha) Yuwsuf na kaka zake kwa waulizao.

 

 

إِذْ قَالُوا لَيُوسُفُ وَأَخُوهُ أَحَبُّ إِلَىٰ أَبِينَا مِنَّا وَنَحْنُ عُصْبَةٌ إِنَّ أَبَانَا لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٨﴾

8. Pale waliposema: Bila shaka Yuwsuf na ndugu yake (shakiki Binyaamiyn)[6] ni vipenzi zaidi kwa baba yetu kuliko sisi, na hali sisi ni kundi (lenye idadi kubwa), hakika baba yetu yumo katika makosa ya bayana.

 

 

 

اقْتُلُوا يُوسُفَ أَوِ اطْرَحُوهُ أَرْضًا يَخْلُ لَكُمْ وَجْهُ أَبِيكُمْ وَتَكُونُوا مِن بَعْدِهِ قَوْمًا صَالِحِينَ﴿٩﴾

9. Muueni Yuwsuf, au mtupilieni mbali katika ardhi (ya mbali) ili uso wa baba yenu ukuelekeeni nyinyi na muwe baada ya hapo watu Swalihina.

 

 

 

قَالَ قَائِلٌ مِّنْهُمْ لَا تَقْتُلُوا يُوسُفَ وَأَلْقُوهُ فِي غَيَابَتِ الْجُبِّ يَلْتَقِطْهُ بَعْضُ السَّيَّارَةِ إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ﴿١٠﴾

10. Akasema msemaji miongoni mwao: Msimuue Yuwsuf, bali mtumbukizeni katika kisima kirefu watamwokota baadhi ya wasafiri, ikiwa nyinyi ni wenye (kuazimia) kufanya.

 

 

 

قَالُوا يَا أَبَانَا مَا لَكَ لَا تَأْمَنَّا عَلَىٰ يُوسُفَ وَإِنَّا لَهُ لَنَاصِحُونَ﴿١١﴾

11. Wakasema: Ee baba yetu! Una nini hata hutuamini kwa Yuwsuf, wakati sisi tunampendelea kila jema? 

 

 

 

أَرْسِلْهُ مَعَنَا غَدًا يَرْتَعْ وَيَلْعَبْ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ﴿١٢﴾

12. Mwache atoke pamoja nasi kesho, ale atakacho na acheze, na hakika sisi tutamhifadhi. 

 

 

 

قَالَ إِنِّي لَيَحْزُنُنِي أَن تَذْهَبُوا بِهِ وَأَخَافُ أَن يَأْكُلَهُ الذِّئْبُ وَأَنتُمْ عَنْهُ غَافِلُونَ﴿١٣﴾

13. Akasema: Hakika mimi inanihuzunisha kwamba nyinyi mwende naye, na nakhofu asije kuliwa na mbwa mwitu, nanyi muwe mmeghafilika naye. 

 

 

 

قَالُوا لَئِنْ أَكَلَهُ الذِّئْبُ وَنَحْنُ عُصْبَةٌ إِنَّا إِذًا لَّخَاسِرُونَ﴿١٤﴾

14. Wakasema: Ikiwa mbwa mwitu atamla na hali sisi ni kikundi (cha idadi kubwa na nguvu) hakika sisi hapo bila shaka tutakuwa watu wasiofaa kwa lolote.

 

 

 

فَلَمَّا ذَهَبُوا بِهِ وَأَجْمَعُوا أَن يَجْعَلُوهُ فِي غَيَابَتِ الْجُبِّ ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِ لَتُنَبِّئَنَّهُم بِأَمْرِهِمْ هَـٰذَا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ﴿١٥﴾

15. Basi walipokwenda naye, na wakakubaliana wamtie katika kisima kirefu, Tulimtia ilhamu (Yuwsuf) kwamba bila shaka utakuja kuwajulisha jambo lao hili wala wao hawahisi.

 

 

 

وَجَاءُوا أَبَاهُمْ عِشَاءً يَبْكُونَ﴿١٦﴾

16.  Wakaja kwa baba yao usiku wanalia.

 

 

 

قَالُوا يَا أَبَانَا إِنَّا ذَهَبْنَا نَسْتَبِقُ وَتَرَكْنَا يُوسُفَ عِندَ مَتَاعِنَا فَأَكَلَهُ الذِّئْبُ ۖ وَمَا أَنتَ بِمُؤْمِنٍ لَّنَا وَلَوْ كُنَّا صَادِقِينَ﴿١٧﴾

17. Wakasema: Ee baba yetu! Hakika sisi tulikwenda kushindana mbio na tulimwacha Yuwsuf kwenye vitu vyetu, basi mbwa mwitu akamla. Nawe hutotuamini japo ni wakweli.

 

 

 

وَجَاءُوا عَلَىٰ قَمِيصِهِ بِدَمٍ كَذِبٍ ۚ قَالَ بَلْ سَوَّلَتْ لَكُمْ أَنفُسُكُمْ أَمْرًا ۖ فَصَبْرٌ جَمِيلٌ ۖ وَاللَّـهُ الْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ﴿١٨﴾

18. Wakaja na kanzu yake ikiwa na damu ya uongo. (Baba yao) akasema: Bali nafsi zenu zimekushawishini jambo. Basi subira njema, na Allaah Ni Mwenye kuombwa msaada juu ya mnayoyaeleza.

 

 

 

وَجَاءَتْ سَيَّارَةٌ فَأَرْسَلُوا وَارِدَهُمْ فَأَدْلَىٰ دَلْوَهُ ۖ قَالَ يَا بُشْرَىٰ هَـٰذَا غُلَامٌ ۚ وَأَسَرُّوهُ بِضَاعَةً ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِمَا يَعْمَلُونَ﴿١٩﴾

19. Ukaja msafara, wakamtuma mtekaji maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake. Akasema: Eh, bishara nzuri hii! Huyu ni ghulamu! Na wakamficha kumfanya bidhaa. Na Allaah Ni Mjuzi kwa yale wanayoyatenda. 

 

 

 

وَشَرَوْهُ بِثَمَنٍ بَخْسٍ دَرَاهِمَ مَعْدُودَةٍ وَكَانُوا فِيهِ مِنَ الزَّاهِدِينَ﴿٢٠﴾

20. Wakamuuza kwa thamani ndogo mno ya dirham za kuhesabika, na walikuwa hawana hamu ya kubaki naye.

 

 

 

وَقَالَ الَّذِي اشْتَرَاهُ مِن مِّصْرَ لِامْرَأَتِهِ أَكْرِمِي مَثْوَاهُ عَسَىٰ أَن يَنفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا ۚ وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي الْأَرْضِ وَلِنُعَلِّمَهُ مِن تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ ۚ وَاللَّـهُ غَالِبٌ عَلَىٰ أَمْرِهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٢١﴾

21. Na yule (kigogo au waziri)[7] aliyemnunua huko Misri alimwambia mke wake: Mkirimu makazi yake, asaa akatufaa au tutamchukua kama ni mwanetu. Na hivyo ndivyo Tulivyommakinisha Yuwsuf katika ardhi na ili Tumfunze tafsiri za khabari (za ndoto na matukio). Na Allaah Ni Mwenye Kushinda juu ya Jambo Lake, lakini watu wengi hawajui.

 

     

 

 

وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ﴿٢٢﴾

22. Na (Yuwsuf) alipofikia umri wa kupevuka, Tulimpa hikmah na ilimu. Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.

 

 

 

 

وَرَاوَدَتْهُ الَّتِي هُوَ فِي بَيْتِهَا عَن نَّفْسِهِ وَغَلَّقَتِ الْأَبْوَابَ وَقَالَتْ هَيْتَ لَكَ ۚ قَالَ مَعَاذَ اللَّـهِ ۖ إِنَّهُ رَبِّي أَحْسَنَ مَثْوَايَ ۖ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ﴿٢٣﴾

23. Na yule mwanamke ambaye yeye (Yuwsuf) alikuwa katika nyumba yake alimtongoza kinyume na nafsi yake, na akafunga milango na kumwambia: Haya njoo! (Yuwsuf) akasema: Najikinga kwa Allaah! Hakika yeye bwana wangu[8] amenifanyia makazi mazuri. Hakika madhalimu hawafaulu.

 

 

 

وَلَقَدْ هَمَّتْ بِهِ ۖ وَهَمَّ بِهَا لَوْلَا أَن رَّأَىٰ بُرْهَانَ رَبِّهِ ۚ كَذَٰلِكَ لِنَصْرِفَ عَنْهُ السُّوءَ وَالْفَحْشَاءَ ۚ إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُخْلَصِينَ﴿٢٤﴾

24. Na kwa yakini alimtamani (Yuwsuf) (kwa ari na azima) na (Yuwsuf) angelimtamani (kwa maumbile ya kibinaadam) lau kwamba asingeliona buruhani (ishara) kutoka kwa Rabb wake.  Tumefanya hayo ili Tumwepushe na uovu na machafu. Hakika yeye ni miongoni mwa Waja Wetu waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.

 

 

 

وَاسْتَبَقَا الْبَابَ وَقَدَّتْ قَمِيصَهُ مِن دُبُرٍ وَأَلْفَيَا سَيِّدَهَا لَدَى الْبَابِ ۚ قَالَتْ مَا جَزَاءُ مَنْ أَرَادَ بِأَهْلِكَ سُوءًا إِلَّا أَن يُسْجَنَ أَوْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٢٥﴾

25. Wakakimbilia mlangoni wote wawili (Yuwsuf awahi kutoka nje na yeye awahi kumzuia), akairarua kanzu yake (Yuwsuf) kwa nyuma (katika patashika hiyo), na wakamkuta bwana (mume) wake mlangoni. (Mke wa ‘aziyz) akasema: Hakuna jazaa ya anayetaka kufanya uovu na ahli wako isipokuwa kufungwa jela au adhabu iumizayo.

 

 

 

قَالَ هِيَ رَاوَدَتْنِي عَن نَّفْسِي ۚ وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِّنْ أَهْلِهَا إِن كَانَ قَمِيصُهُ قُدَّ مِن قُبُلٍ فَصَدَقَتْ وَهُوَ مِنَ الْكَاذِبِينَ﴿٢٦﴾

26. (Yuwsuf) akasema: Yeye ndiye aliyenitongoza kinyume na nafsi yangu. Na akashuhudia shahidi miongoni mwa ahli zake mwanamke (akasema): Ikiwa kanzu yake imechanwa mbele, basi mwanamke amesema kweli, naye (Yuwsuf) ni miongoni mwa waongo.

 

 

 

وَإِن كَانَ قَمِيصُهُ قُدَّ مِن دُبُرٍ فَكَذَبَتْ وَهُوَ مِنَ الصَّادِقِينَ﴿٢٧﴾

27. Na ikiwa kanzu yake imechanwa nyuma, basi mwanamke amesema uongo, naye (Yuwsuf) ni miongoni mwa wakweli.

 

 

 

فَلَمَّا رَأَىٰ قَمِيصَهُ قُدَّ مِن دُبُرٍ قَالَ إِنَّهُ مِن كَيْدِكُنَّ ۖ إِنَّ كَيْدَكُنَّ عَظِيمٌ﴿٢٨﴾

28. Basi (mumewe) alipoona kanzu yake imechanwa nyuma, alisema: Hakika hii ni katika vitimbi vyenu wanawake. Hakika vitimbi vyenu wanawake ni vikubwa mno.

 

 

 

 

يُوسُفُ أَعْرِضْ عَنْ هَـٰذَا ۚ وَاسْتَغْفِرِي لِذَنبِكِ ۖ إِنَّكِ كُنتِ مِنَ الْخَاطِئِينَ﴿٢٩﴾

29. (Ee) Yuwsuf yaachilie mbali haya. Na (wewe) mwanamke omba maghfirah kwa ajili ya dhambi yako. Hakika wewe ulikuwa miongoni mwa wenye hatia.

 

 

 

وَقَالَ نِسْوَةٌ فِي الْمَدِينَةِ امْرَأَتُ الْعَزِيزِ تُرَاوِدُ فَتَاهَا عَن نَّفْسِهِ ۖ قَدْ شَغَفَهَا حُبًّا ۖ إِنَّا لَنَرَاهَا فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٣٠﴾

30. Na wanawake katika mji ule wakasema: Mke wa ‘aziyz anamtongoza kijana wake kinyume na nafsi yake. Kijana kashammaliza kwa mapenzi, haoni hasikii. Hakika sisi tunamuona yumo katika upotofu bayana.

 

 

 

فَلَمَّا سَمِعَتْ بِمَكْرِهِنَّ أَرْسَلَتْ إِلَيْهِنَّ وَأَعْتَدَتْ لَهُنَّ مُتَّكَأً وَآتَتْ كُلَّ وَاحِدَةٍ مِّنْهُنَّ سِكِّينًا وَقَالَتِ اخْرُجْ عَلَيْهِنَّ ۖ فَلَمَّا رَأَيْنَهُ أَكْبَرْنَهُ وَقَطَّعْنَ أَيْدِيَهُنَّ وَقُلْنَ حَاشَ لِلَّـهِ مَا هَـٰذَا بَشَرًا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا مَلَكٌ كَرِيمٌ﴿٣١﴾

31. (Mke wa ‘aziyz) aliposikia hila zao (za kumchafulia jina zaidi), aliwaalika na akawaandalia hafla (na matakia), na akampa kila mmoja wao kisu. Kisha akasema: Tokeza mbele yao. Basi walipomuona (Yuwsuf) walimpa haiba na utukuzo, wakajikatakata mikono yao, na wakasema: Haasha li-LLaah! (Ametakasika Allaah Mkamilifu wa Kuumba).   Huyu si mtu! Hakuwa huyu ila ni Malaika mtukufu.  

 

 

 

قَالَتْ فَذَٰلِكُنَّ الَّذِي لُمْتُنَّنِي فِيهِ ۖ وَلَقَدْ رَاوَدتُّهُ عَن نَّفْسِهِ فَاسْتَعْصَمَ ۖ وَلَئِن لَّمْ يَفْعَلْ مَا آمُرُهُ لَيُسْجَنَنَّ وَلَيَكُونًا مِّنَ الصَّاغِرِينَ﴿٣٢﴾

32. Akasema: Basi huyo ndiye mliyekuwa mkinilaumia. Na kwa yakini nilimtamani kinyume na nafsi yake, akajilinda. Na kama hatofanya ninalomuamrisha, basi bila shaka atafungwa jela, na bila shaka atakuwa miongoni mwa waliodhalilishwa.

 

 

 

قَالَ رَبِّ السِّجْنُ أَحَبُّ إِلَيَّ مِمَّا يَدْعُونَنِي إِلَيْهِ ۖ وَإِلَّا تَصْرِفْ عَنِّي كَيْدَهُنَّ أَصْبُ إِلَيْهِنَّ وَأَكُن مِّنَ الْجَاهِلِينَ﴿٣٣﴾

33. (Yuwsuf) akasema: Ee Rabb wangu! Nastahabu zaidi jela kuliko yale wanayoniitia. Na Usiponiepusha na vitimbi vyao nitaelemea kwao na nitakuwa miongoni mwa majahili.

 

 

 

فَاسْتَجَابَ لَهُ رَبُّهُ فَصَرَفَ عَنْهُ كَيْدَهُنَّ ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿٣٤﴾

34. Basi Rabb wake Akamuitikia na Akamuepusha na vitimbi vyao. Hakika Yeye Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

ثُمَّ بَدَا لَهُم مِّن بَعْدِ مَا رَأَوُا الْآيَاتِ لَيَسْجُنُنَّهُ حَتَّى حِينٍ﴿٣٥﴾

35. Kisha ikawadhihirikia baada ya kuona Aayaat (Dalili, Vielelezo) [vya kumtoa hatiani] kuwa wamfunge jela kwa muda fulani.

 

 

 

وَدَخَلَ مَعَهُ السِّجْنَ فَتَيَانِ ۖ قَالَ أَحَدُهُمَا إِنِّي أَرَانِي أَعْصِرُ خَمْرًا ۖ وَقَالَ الْآخَرُ إِنِّي أَرَانِي أَحْ  مِلُ فَوْقَ رَأْسِي خُبْزًا تَأْكُلُ الطَّيْرُ مِنْهُ ۖ نَبِّئْنَا بِتَأْوِيلِهِ ۖ إِنَّا نَرَاكَ مِنَ الْمُحْسِنِينَ﴿٣٦﴾

36.  Wakaingia pamoja naye jela vijana wawili.  Mmoja wao akasema: Hakika mimi nimeona ndotoni kuwa nakamua (zabibu ziwe) mvinyo. Na mwengine akasema: Hakika mimi nimeona ndotoni nabeba juu ya kichwa changu (kapu la) mikate wanaila ndege humo. Tujulishe tafsiri yake, hakika sisi tunakuona ni miongoni mwa wafanyao ihsaan.

 

 

 

قَالَ لَا يَأْتِيكُمَا طَعَامٌ تُرْزَقَانِهِ إِلَّا نَبَّأْتُكُمَا بِتَأْوِيلِهِ قَبْلَ أَن يَأْتِيَكُمَا ۚ ذَٰلِكُمَا مِمَّا عَلَّمَنِي رَبِّي ۚ إِنِّي تَرَكْتُ مِلَّةَ قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ﴿٣٧﴾

37. (Yuwsuf) akasema: Hakitokufikieni chakula chochote mtakachopewa kula isipokuwa nitakujulisheni wasifu wake kabla hakijakufikieni. Hayo nitakayowafasiria ni katika Aliyonifunza Rabb wangu. Hakika mimi nimeacha mila ya watu wasiomwamini Allaah na wao ni wenye kuikanusha Aakhirah. 

 

 

 

وَاتَّبَعْتُ مِلَّةَ آبَائِي إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ مَا كَانَ لَنَا أَن نُّشْرِكَ بِاللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۚ ذَٰلِكَ مِن فَضْلِ اللَّـهِ عَلَيْنَا وَعَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ﴿٣٨﴾

38. Na nimefuata Dini ya baba zangu Ibraahiym, na Is-haaq na Ya’quwb. Haikutupasa kumshirikisha Allaah na kitu chochote. Hilo (la kutomshirikisha) ni katika Fadhila za Allaah juu yetu na juu ya watu, lakini watu wengi hawashukuru.

 

 

 

يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ أَأَرْبَابٌ مُّتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ أَمِ اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ﴿٣٩﴾

39. Enyi masahibu wangu wawili wa jela! Je, miola wengi wanaofarakana ni bora au Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika?

 

 

 

مَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا أَسْمَاءً سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ ۚ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۚ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٤٠﴾

40. Hamuabudu pasi Naye (Allaah) isipokuwa majina tu mmeyaita nyinyi na baba zenu, Hakuyateremshia Allaah mamlaka yoyote. Hakuna hukumu isipokuwa ya Allaah. Ameamrisha kwamba msiabudu chochote isipokuwa Yeye Pekee. Hiyo ndio Dini iliyonyooka, lakini watu wengi hawajui.

 

 

 

يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ أَمَّا أَحَدُكُمَا فَيَسْقِي رَبَّهُ خَمْرًا ۖ وَأَمَّا الْآخَرُ فَيُصْلَبُ فَتَأْكُلُ الطَّيْرُ مِن رَّأْسِهِ ۚ قُضِيَ الْأَمْرُ الَّذِي فِيهِ تَسْتَفْتِيَانِ﴿٤١﴾

41. Enyi masahibu wangu wawili wa jela! Ama mmoja wenu atamnywesha bwana wake mvinyo. Na ama mwengine atasulubiwa, na ndege watakula kichwani mwake. Limeshahukumiwa jambo ambalo mnaliulizia.

 

 

 

 

وَقَالَ لِلَّذِي ظَنَّ أَنَّهُ نَاجٍ مِّنْهُمَا اذْكُرْنِي عِندَ رَبِّكَ فَأَنسَاهُ الشَّيْطَانُ ذِكْرَ رَبِّهِ فَلَبِثَ فِي السِّجْنِ بِضْعَ سِنِينَ﴿٤٢﴾

42. (Yuwsuf) akasema kumwambia yule aliyejua kuwa ataokoka miongoni mwa wale wawili: Nikumbuke mbele ya bwana wako. Lakini shaytwaan alimsahaulisha kumkumbuka kwa bwana wake. Basi akabakia jela miaka kadhaa.

 

 

 

وَقَالَ الْمَلِكُ إِنِّي أَرَىٰ سَبْعَ بَقَرَاتٍ سِمَانٍ يَأْكُلُهُنَّ سَبْعٌ عِجَافٌ وَسَبْعَ سُنبُلَاتٍ خُضْرٍ وَأُخَرَ يَابِسَاتٍ ۖ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ أَفْتُونِي فِي رُؤْيَايَ إِن كُنتُمْ لِلرُّؤْيَا تَعْبُرُونَ﴿٤٣﴾

43. (Kisha) na mfalme akasema: Hakika mimi naona ndotoni ng’ombe saba wanene wanaliwa na ng’ombe saba waliokonda, na mashuke saba ya kijani na mengineyo (saba) yabisi. Enyi wakuu! Nifutuni kuhusu ndoto yangu, mkiwa ni wenye kuagua ndoto.

 

 

 

قَالُوا أَضْغَاثُ أَحْلَامٍ ۖ وَمَا نَحْنُ بِتَأْوِيلِ الْأَحْلَامِ بِعَالِمِينَ﴿٤٤﴾

44.  Wakasema: Mkorogano wa ndoto! Nasi si wenye kujua kufasiri ndoto.

 

 

 

وَقَالَ الَّذِي نَجَا مِنْهُمَا وَادَّكَرَ بَعْدَ أُمَّةٍ أَنَا أُنَبِّئُكُم بِتَأْوِيلِهِ فَأَرْسِلُونِ﴿٤٥﴾

45.  Akasema yule aliyeokoka kati ya wale wawili na akakumbuka baada ya muda: Mimi nitakujulisheni kuhusu tafsiri yake. Basi, nitumeni (kwa Yuwsuf nikamuulize).

 

 

 

يُوسُفُ أَيُّهَا الصِّدِّيقُ أَفْتِنَا فِي سَبْعِ بَقَرَاتٍ سِمَانٍ يَأْكُلُهُنَّ سَبْعٌ عِجَافٌ وَسَبْعِ سُنبُلَاتٍ خُضْرٍ وَأُخَرَ يَابِسَاتٍ لَّعَلِّي أَرْجِعُ إِلَى النَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَعْلَمُونَ﴿٤٦﴾

46. Yuwsuf! Ee mkweli wa dhati! Tufutu kuhusiana na ng’ombe saba wanene wanaliwa na ng’ombe saba waliokonda, na mashuke saba ya kijani na mengineyo (saba) yabisi, ili nirejee kwa watu ili wapate kujua.

 

 

 

قَالَ تَزْرَعُونَ سَبْعَ سِنِينَ دَأَبًا فَمَا حَصَدتُّمْ فَذَرُوهُ فِي سُنبُلِهِ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّا تَأْكُلُونَ﴿٤٧﴾

47. Akasema: Mtalima miaka saba mfululizo bila kusita. Mtakachokivuna kiacheni katika mashuke yake isipokuwa kichache mtakachokula.

 

 

 

ثُمَّ يَأْتِي مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ سَبْعٌ شِدَادٌ يَأْكُلْنَ مَا قَدَّمْتُمْ لَهُنَّ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّا تُحْصِنُونَ﴿٤٨﴾

48. Kisha itakuja baada ya hapo (miaka) saba ya shida itakayokula vile mlivyovitanguliza kuviweka kwa ajili yao isipokuwa kidogo katika vile mtakavyoweka akiba.

 

 

 

ثُمَّ يَأْتِي مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ عَامٌ فِيهِ يُغَاثُ النَّاسُ وَفِيهِ يَعْصِرُونَ﴿٤٩﴾

49. Kisha utakuja baada ya hapo mwaka humo watu watasaidiwa kwa kunyweshewa mvua na humo watakamua (vya kukamuliwa).

 

 

 

وَقَالَ الْمَلِكُ ائْتُونِي بِهِ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُ الرَّسُولُ قَالَ ارْجِعْ إِلَىٰ رَبِّكَ فَاسْأَلْهُ مَا بَالُ النِّسْوَةِ اللَّاتِي قَطَّعْنَ أَيْدِيَهُنَّ ۚ إِنَّ رَبِّي بِكَيْدِهِنَّ عَلِيمٌ﴿٥٠﴾

50.  Mfalme akasema:  Nileteeni (Yuwsuf). Basi (Yuwsuf) alipojiwa na mjumbe alisema: Rejea kwa bwana wako umuulize nini mkasa wa wanawake waliojikata mikono yao. Hakika Rabb wangu kwa vitimbi vyao Ni Mjuzi.

 

 

 

قَالَ مَا خَطْبُكُنَّ إِذْ رَاوَدتُّنَّ يُوسُفَ عَن نَّفْسِهِ ۚ قُلْنَ حَاشَ لِلَّـهِ مَا عَلِمْنَا عَلَيْهِ مِن سُوءٍ ۚ قَالَتِ امْرَأَتُ الْعَزِيزِ الْآنَ حَصْحَصَ الْحَقُّ أَنَا رَاوَدتُّهُ عَن نَّفْسِهِ وَإِنَّهُ لَمِنَ الصَّادِقِينَ﴿٥١﴾

51. (Mfalme) akasema: Mlikuwa na jambo gani kubwa mlipomtongoza Yuwsuf kinyume na nafsi yake? Wakasema: Haasha liLlaah! (Ametakasika Allaah Mkamilifu wa Kuumba). Hatukuona uovu wowote kwake. Mke wa ‘aziyz akasema: Hivi sasa umefichuka ukweli! Mimi nilimtongoza kinyume na nafsi yake. Na hakika yeye bila shaka ni miongoni mwa wakweli.  

 

 

ذَٰلِكَ لِيَعْلَمَ أَنِّي لَمْ أَخُنْهُ بِالْغَيْبِ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي كَيْدَ الْخَائِنِينَ﴿٥٢﴾

52. (Yuwsuf akasema:) Nimekiri hilo ili (‘aziyz) apate kujua kwamba mimi sikumfanyia khiyana kwa siri, na kwamba Allaah Haongozi hila za makhaini.

 

 

 

وَمَا أُبَرِّئُ نَفْسِي ۚ إِنَّ النَّفْسَ لَأَمَّارَةٌ بِالسُّوءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّي ۚ إِنَّ رَبِّي غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٥٣﴾

53. Nami siitoi hatiani nafsi yangu. Hakika nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu[9] isipokuwa ambayo Rabb wangu Ameirehemu.  Hakika Rabb wangu Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

وَقَالَ الْمَلِكُ ائْتُونِي بِهِ أَسْتَخْلِصْهُ لِنَفْسِي ۖ فَلَمَّا كَلَّمَهُ قَالَ إِنَّكَ الْيَوْمَ لَدَيْنَا مَكِينٌ أَمِينٌ ﴿٥٤﴾

54. Na mfalme akasema: Nileteeni (Yuwsuf) nimteue makhsusi kwangu. Basi aliposema naye, akasema: Hakika wewe leo kwetu umetamakani kwa cheo na umekuwa muaminiwa.

 

 

 

قَالَ اجْعَلْنِي عَلَىٰ خَزَائِنِ الْأَرْضِ ۖ إِنِّي حَفِيظٌ عَلِيمٌ ﴿٥٥﴾

55. (Yuwsuf) akasema: Niteue niwe msimamizi wa mapato ya ardhi, hakika mimi ni mhifadhi mjuzi.

 

 

 

وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي الْأَرْضِ يَتَبَوَّأُ مِنْهَا حَيْثُ يَشَاءُ ۚ نُصِيبُ بِرَحْمَتِنَا مَن نَّشَاءُ ۖ وَلَا نُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٦﴾

56. Na hivyo ndivyo Tulivyommakinisha Yuwsuf katika ardhi, anakaa humo popote atakapo. Tunamfikishia Rehma Yetu Tumtakaye, na wala Hatupotezi ujira wa watendao ihsaan.

 

 

وَلَأَجْرُ الْآخِرَةِ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ ﴿٥٧﴾

57. Na bila shaka ujira wa Aakhirah ni bora zaidi kwa wale walioamini na wakawa na taqwa.

 

 

 

وَجَاءَ إِخْوَةُ يُوسُفَ فَدَخَلُوا عَلَيْهِ فَعَرَفَهُمْ وَهُمْ لَهُ مُنكِرُونَ ﴿٥٨﴾

58. Wakaja kaka zake Yuwsuf wakaingia kwake, yeye akawatambua, lakini wao hawakumtambua.

 

 

 

وَلَمَّا جَهَّزَهُم بِجَهَازِهِمْ قَالَ ائْتُونِي بِأَخٍ لَّكُم مِّنْ أَبِيكُمْ ۚ أَلَا تَرَوْنَ أَنِّي أُوفِي الْكَيْلَ وَأَنَا خَيْرُ الْمُنزِلِينَ﴿٥٩﴾

59. Na alipowatayarishia mizigo yao akasema: Nileteeni ndugu yenu kwa baba yenu. Je, hamuoni kwamba mimi natimiza kikamilifu kipimo nami ni mbora wa wenye kukirimu?

 

 

 

فَإِن لَّمْ تَأْتُونِي بِهِ فَلَا كَيْلَ لَكُمْ عِندِي وَلَا تَقْرَبُونِ ﴿٦٠﴾

60. Msiponijia naye, basi hamtokuwa na kipimo kwangu wala msinikurubie.

 

 

 

قَالُوا سَنُرَاوِدُ عَنْهُ أَبَاهُ وَإِنَّا لَفَاعِلُونَ ﴿٦١﴾

61.  Wakasema: Tutamrairai baba yake aturuhusu tutoke naye na bila shaka tutafanya.

 

 

 

وَقَالَ لِفِتْيَانِهِ اجْعَلُوا بِضَاعَتَهُمْ فِي رِحَالِهِمْ لَعَلَّهُمْ يَعْرِفُونَهَا إِذَا انقَلَبُوا إِلَىٰ أَهْلِهِمْ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٦٢﴾

62. (Yuwsuf) akawaambia watumishi wake: Wekeni bidhaa zao katika mizigo yao, watapata kuzitambua watakaporudi kwa ahli zao, huenda wakarejea.

 

 

 

فَلَمَّا رَجَعُوا إِلَىٰ أَبِيهِمْ قَالُوا يَا أَبَانَا مُنِعَ مِنَّا الْكَيْلُ فَأَرْسِلْ مَعَنَا أَخَانَا نَكْتَلْ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ﴿٦٣﴾

63. Waliporejea kwa baba yao, walisema: Ee baba yetu! Tumenyimwa kipimo, basi mwachie ndugu yetu atoke pamoja nasi tupate kupimiwa, na sisi bila shaka tutamhifadhi.

 

 

 

قَالَ هَلْ آمَنُكُمْ عَلَيْهِ إِلَّا كَمَا أَمِنتُكُمْ عَلَىٰ أَخِيهِ مِن قَبْلُ ۖ فَاللَّـهُ خَيْرٌ حَافِظًا ۖ وَهُوَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ ﴿٦٤﴾

64. Akasema: Vipi nimwaminishe kwenu kama nilivyokuaminini kwa kaka yake kabla? Basi Allaah ni Ni Mbora wa wenye kuhifadhi. Naye Ni Mbora zaidi wa Kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu.

 

 

 

وَلَمَّا فَتَحُوا مَتَاعَهُمْ وَجَدُوا بِضَاعَتَهُمْ رُدَّتْ إِلَيْهِمْ ۖ قَالُوا يَا أَبَانَا مَا نَبْغِي ۖ هَـٰذِهِ بِضَاعَتُنَا رُدَّتْ إِلَيْنَا ۖ وَنَمِيرُ أَهْلَنَا وَنَحْفَظُ أَخَانَا وَنَزْدَادُ كَيْلَ بَعِيرٍ ۖ ذَٰلِكَ كَيْلٌ يَسِيرٌ ﴿٦٥﴾

65. Walipofungua mizigo yao, walikuta bidhaa zao zimerudishwa kwao. Wakasema: Ee baba yetu! Tunataka nini zaidi? Hizi bidhaa zetu tumerejeshewa, nasi tutawaletea chakula ahli zetu, na tutamhifadhi ndugu yetu, na tutapata ziada ya shehena ya ngamia. Hicho ni kipimo chepesi.

 

 

 

قَالَ لَنْ أُرْسِلَهُ مَعَكُمْ حَتَّىٰ تُؤْتُونِ مَوْثِقًا مِّنَ اللَّـهِ لَتَأْتُنَّنِي بِهِ إِلَّا أَن يُحَاطَ بِكُمْ ۖ فَلَمَّا آتَوْهُ مَوْثِقَهُمْ قَالَ اللَّـهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٌ ﴿٦٦﴾

66. Akasema: Sitompeleka pamoja nanyi mpaka mnipe Ahadi ya Allaah kwamba lazima nyinyi mtamrudisha kwangu isipokuwa ikiwa mmezungukwa. Basi walipompa ahadi yao, akasema: Allaah kwa tuyasemayo Ni Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.

 

 

 

وَقَالَ يَا بَنِيَّ لَا تَدْخُلُوا مِن بَابٍ وَاحِدٍ وَادْخُلُوا مِنْ أَبْوَابٍ مُّتَفَرِّقَةٍ ۖ وَمَا أُغْنِي عَنكُم مِّنَ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۖ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖوَعَلَيْهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُتَوَكِّلُونَ ﴿٦٧﴾

67. Na akasema: Enyi wanangu! Msiingie kupitia mlango mmoja, bali ingieni kupitia milango tofauti. Na mimi siwezi kukufaeni chochote kwa Alilolipanga Allaah. Hapana hukumu isipokuwa ya Allaah tu. Kwake natawakali. Na Kwake watawakali wanaotawakali.

 

 

 

وَلَمَّا دَخَلُوا مِنْ حَيْثُ أَمَرَهُمْ أَبُوهُم مَّا كَانَ يُغْنِي عَنْهُم مِّنَ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ إِلَّا حَاجَةً فِي نَفْسِ يَعْقُوبَ قَضَاهَا ۚ وَإِنَّهُ لَذُو عِلْمٍ لِّمَا عَلَّمْنَاهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٦٨﴾

68. Na walipoingia kwa namna alivyowaamrisha baba yao, haikuwafaa kitu kwa Allaah isipokuwa haja iliyokuwa katika nafsi ya Ya’quwb aliyoitimiza.[10] Na hakika yeye alikuwa mwenye ilimu Tuliyomfunza, lakini watu wengi hawajui.

 

 

 

وَلَمَّا دَخَلُوا عَلَىٰ يُوسُفَ آوَىٰ إِلَيْهِ أَخَاهُ ۖ قَالَ إِنِّي أَنَا أَخُوكَ فَلَا تَبْتَئِسْ بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٦٩﴾

69. Na walipoingia kwa Yuwsuf, alimuweka ndugu yake karibu naye. Akasema: Hakika mimi ni kaka yako, basi usisikitike kwa yale waliyokuwa wakiyafanya.

 

 

 

فَلَمَّا جَهَّزَهُم بِجَهَازِهِمْ جَعَلَ السِّقَايَةَ فِي رَحْلِ أَخِيهِ ثُمَّ أَذَّنَ مُؤَذِّنٌ أَيَّتُهَا الْعِيرُ إِنَّكُمْ لَسَارِقُونَ﴿٧٠﴾

70. Na alipowatayarishia mizigo yao alikitia kikopo cha kutekea katika mzigo wa ndugu yake, kisha mwenye kunadi akanadi: Enyi wasafiri! Hakika nyinyi ni wezi!

 

 

 

قَالُوا وَأَقْبَلُوا عَلَيْهِم مَّاذَا تَفْقِدُونَ ﴿٧١﴾

71. Wakasema na huku wamewakabili: Mmepoteza nini?

 

 

 

قَالُوا نَفْقِدُ صُوَاعَ الْمَلِكِ وَلِمَن جَاءَ بِهِ حِمْلُ بَعِيرٍ وَأَنَا بِهِ زَعِيمٌ ﴿٧٢﴾

72. Wakasema: Tumepoteza bika ya kupimia ya mfalme. Na atakayekuja nayo atapewa shehena ya ngamia, nami kwa hayo ni mdhamini.

 

 

 

قَالُوا تَاللَّـهِ لَقَدْ عَلِمْتُم مَّا جِئْنَا لِنُفْسِدَ فِي الْأَرْضِ وَمَا كُنَّا سَارِقِينَ ﴿٧٣﴾

73.  Wakasema: Ta-Allaahi (Tunaapa kwa Allaah)![11] Nyinyi mmeshapata uhakika kuwa hatukuja kufanya ufisadi katika ardhi, na hatuna historia ya kuwa wezi.

 

 

 

قَالُوا فَمَا جَزَاؤُهُ إِن كُنتُمْ كَاذِبِينَ ﴿٧٤﴾

74. Wakasema: Basi nini adhabu yake, mkiwa ni waongo? 

 

 

 

قَالُوا جَزَاؤُهُ مَن وُجِدَ فِي رَحْلِهِ فَهُوَ جَزَاؤُهُ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ ﴿٧٥﴾

75. Wakasema: Adhabu yake ni yule ambaye itapatikana (bika ya mfalme) kwenye mzigo wake, basi yeye ndiye adhabu yake.[12] Hivyo ndivyo tunavyowalipa madhalimu

 

 

 

فَبَدَأَ بِأَوْعِيَتِهِمْ قَبْلَ وِعَاءِ أَخِيهِ ثُمَّ اسْتَخْرَجَهَا مِن وِعَاءِ أَخِيهِ ۚ كَذَٰلِكَ كِدْنَا لِيُوسُفَ ۖ مَا كَانَ لِيَأْخُذَ أَخَاهُ فِي دِينِ الْمَلِكِ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاءُ ۗ وَفَوْقَ كُلِّ ذِي عِلْمٍ عَلِيمٌ ﴿٧٦﴾

76. Akaanza (kutafuta) katika mizigo yao kabla ya mzigo wa ndugu yake. Kisha akaitoa kutoka katika mzigo wa ndugu yake. Hivyo ndivyo Tulivyosahilisha mpango[13] wa Yuwsuf. Hakuweza kumchukua ndugu yake katika sharia ya mfalme isipokuwa Atake Allaah. Tunampandisha vyeo Tumtakaye. Na juu ya kila mwenye ilimu yuko mwenye ilimu zaidi.

 

 

 

قَالُوا إِن يَسْرِقْ فَقَدْ سَرَقَ أَخٌ لَّهُ مِن قَبْلُ ۚ فَأَسَرَّهَا يُوسُفُ فِي نَفْسِهِ وَلَمْ يُبْدِهَا لَهُمْ ۚ قَالَ أَنتُمْ شَرٌّ مَّكَانًا ۖ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا تَصِفُونَ ﴿٧٧﴾

77. Wakasema: Ikiwa ameiba, basi kaka yake aliiba pia zamani. Yuwsuf aliyafutika moyoni na wala hakuwadhihirishia. Akasema (moyoni): Nyinyi mna hali mbaya zaidi, na Allaah Anajua zaidi yale mnayoyavumisha.

 

 

 

قَالُوا يَا أَيُّهَا الْعَزِيزُ إِنَّ لَهُ أَبًا شَيْخًا كَبِيرًا فَخُذْ أَحَدَنَا مَكَانَهُ ۖ إِنَّا نَرَاكَ مِنَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٧٨﴾

78. Wakasema: Ee ‘aziyz! Hakika yeye ana baba mkongwe, basi chukua mmoja wetu mahali pake. Hakika sisi tunakuona ni miongoni mwa wafanyao ihsaan.

 

 

 

قَالَ مَعَاذَ اللَّـهِ أَن نَّأْخُذَ إِلَّا مَن وَجَدْنَا مَتَاعَنَا عِندَهُ إِنَّا إِذًا لَّظَالِمُونَ﴿٧٩﴾

79. Akasema: Tunajikinga kwa Allaah kumchukua isipokuwa yule tuliyekuta kifaa chetu kwake (tukifanya), hakika sisi hapo bila shaka tutakuwa madhalimu.

 

 

 

فَلَمَّا اسْتَيْأَسُوا مِنْهُ خَلَصُوا نَجِيًّا ۖ قَالَ كَبِيرُهُمْ أَلَمْ تَعْلَمُوا أَنَّ أَبَاكُمْ قَدْ أَخَذَ عَلَيْكُم مَّوْثِقًا مِّنَ اللَّـهِ وَمِن قَبْلُ مَا فَرَّطتُمْ فِي يُوسُفَ ۖ فَلَنْ أَبْرَحَ الْأَرْضَ حَتَّىٰ يَأْذَنَ لِي أَبِي أَوْ يَحْكُمَ اللَّـهُ لِي ۖ وَهُوَ خَيْرُ الْحَاكِمِينَ ﴿٨٠﴾

80. Basi walipokata tamaa ya kumpata, walijitenga kando kushauriana kisiri.  Mkubwa wao akasema: Je, hamkumbuki kwamba baba yenu amekwishachukua kwenu ahadi kutoka kwa Allaah, na kabla ya hapo uovu mliomfanyia Yuwsuf? Basi sitoondoka ardhi hii mpaka anipe idhini baba yangu, au Allaah Anihukumie. Naye Ni Mbora wa kuhukumu kuliko wote wenye kuhukumu.

 

 

 

ارْجِعُوا إِلَىٰ أَبِيكُمْ فَقُولُوا يَا أَبَانَا إِنَّ ابْنَكَ سَرَقَ وَمَا شَهِدْنَا إِلَّا بِمَا عَلِمْنَا وَمَا كُنَّا لِلْغَيْبِ حَافِظِينَ ﴿٨١﴾

81. Rejeeni kwa baba yenu, na semeni: Ee baba yetu! Hakika mwanao ameiba, nasi hatukutoa ushahidi (dhidi yake) isipokuwa kwa yale tuliyoyajua, na hatukuwa wenye kujua yatakayotokea mbeleni.

 

 

 

وَاسْأَلِ الْقَرْيَةَ الَّتِي كُنَّا فِيهَا وَالْعِيرَ الَّتِي أَقْبَلْنَا فِيهَا ۖ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ ﴿٨٢﴾

82. Na uliza mji ambao tulikuwa humo, na msafara ambao tumekuja nao, na hakika sisi ni wakweli.

 

 

 

قَالَ بَلْ سَوَّلَتْ لَكُمْ أَنفُسُكُمْ أَمْرًا ۖ فَصَبْرٌ جَمِيلٌ ۖ عَسَى اللَّـهُ أَن يَأْتِيَنِي بِهِمْ جَمِيعًا ۚ إِنَّهُ هُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ ﴿٨٣﴾

83. (Ya’quwb) akasema: Bali nafsi zenu zimekushawishini jambo. Basi subira njema nitaishikilia. Asaa Allaah Aniletee wote pamoja. Hakika Yeye Ndiye Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

وَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا أَسَفَىٰ عَلَىٰ يُوسُفَ وَابْيَضَّتْ عَيْنَاهُ مِنَ الْحُزْنِ فَهُوَ كَظِيمٌ ﴿٨٤﴾

84. Akajitenga nao, na akasema: Ee majonzi yangu juu ya Yuwsuf. Na macho yake yakageuka meupe kutokana na huzuni, naye huku akiwa amezuia ghaidhi za huzuni zilizomjaa.

 

 

 

قَالُوا تَاللَّـهِ تَفْتَأُ تَذْكُرُ يُوسُفَ حَتَّىٰ تَكُونَ حَرَضًا أَوْ تَكُونَ مِنَ الْهَالِكِينَ ﴿٨٥﴾

85. Wakasema: Ta-Allaahi (Tunaapa kwa Allaah)! Hutoacha kumkumbuka Yuwsuf mpaka uwe mgonjwa mahututi, au uwe miongoni mwa wenye kuhilaki.

 

 

 

قَالَ إِنَّمَا أَشْكُو بَثِّي وَحُزْنِي إِلَى اللَّـهِ وَأَعْلَمُ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٨٦﴾

86. Akasema: Hakika mimi nashitakia dhiki ya majonzi yangu na huzuni zangu kwa Allaah. Na najua kutoka kwa Allaah yale msiyoyajua.

 

 

 

يَا بَنِيَّ اذْهَبُوا فَتَحَسَّسُوا مِن يُوسُفَ وَأَخِيهِ وَلَا تَيْأَسُوا مِن رَّوْحِ اللَّـهِ ۖ إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِن رَّوْحِ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ ﴿٨٧﴾

87. Ee wanangu! Nendeni mkawatafute Yuwsuf na ndugu yake, na wala msikate tamaa na Faraja ya Allaah. Hakika hawakati tamaa na Faraja ya Allaah isipokuwa watu makafiri.

 

 

 

فَلَمَّا دَخَلُوا عَلَيْهِ قَالُوا يَا أَيُّهَا الْعَزِيزُ مَسَّنَا وَأَهْلَنَا الضُّرُّ وَجِئْنَا بِبِضَاعَةٍ مُّزْجَاةٍ فَأَوْفِ لَنَا الْكَيْلَ وَتَصَدَّقْ عَلَيْنَا ۖ إِنَّ اللَّـهَ يَجْزِي الْمُتَصَدِّقِينَ ﴿٨٨﴾

88. Walipoingia kwake wakasema: Ee ‘aziyz!  Dhara imetugusa sisi pamoja na ahli zetu, na tumekuja na bidhaa isiyo na thamani, basi tutimizie kipimo, na tupe swadaqa. Hakika Allaah Anawalipa watoao swadaqa.

 

 

 

قَالَ هَلْ عَلِمْتُم مَّا فَعَلْتُم بِيُوسُفَ وَأَخِيهِ إِذْ أَنتُمْ جَاهِلُونَ ﴿٨٩﴾

89. Akasema: Je, mmejua yale mliyomfanyia Yuwsuf na ndugu yake wakati nyinyi majahili?

 

 

 

قَالُوا أَإِنَّكَ لَأَنتَ يُوسُفُ ۖ قَالَ أَنَا يُوسُفُ وَهَـٰذَا أَخِي ۖ قَدْ مَنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا ۖ إِنَّهُ مَن يَتَّقِ وَيَصْبِرْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٩٠﴾

90.  Wakasema: Je, kwani wewe ndio Yuwsuf? Akasema: Mimi ni Yuwsuf, na huyu ni ndugu yangu. Kwa yakini Allaah Ametufanyia ihsaan. Hakika mwenye kuwa na taqwa na akasubiri, basi hakika Allaah Hapotezi ujira wa watendao ihsaan.

 

 

 

قَالُوا تَاللَّـهِ لَقَدْ آثَرَكَ اللَّـهُ عَلَيْنَا وَإِن كُنَّا لَخَاطِئِينَ ﴿٩١﴾

91. Wakasema: Ta-Allaahi (Tunaapa kwa Allaah)! Kwa yakini Allaah Amekufadhilisha wewe kuliko sisi (kwa tabia zote njema), nasi bila shaka tulikuwa wakosa.

 

 

 

قَالَ لَا تَثْرِيبَ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ ۖ يَغْفِرُ اللَّـهُ لَكُمْ ۖ وَهُوَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ ﴿٩٢﴾

92. Akasema: Hakuna lawama juu yenu leo. Allaah Atakughufurieni. Naye Ni Mbora zaidi wa Kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu.

 

 

 

اذْهَبُوا بِقَمِيصِي هَـٰذَا فَأَلْقُوهُ عَلَىٰ وَجْهِ أَبِي يَأْتِ بَصِيرًا وَأْتُونِي بِأَهْلِكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٩٣﴾

93. Nendeni na kanzu yangu hii, na itupeni kwenye uso wa baba yangu, atakuwa mwenye kuona, na nijieni na ahli zenu nyote pamoja.

 

 

 

وَلَمَّا فَصَلَتِ الْعِيرُ قَالَ أَبُوهُمْ إِنِّي لَأَجِدُ رِيحَ يُوسُفَ ۖ لَوْلَا أَن تُفَنِّدُونِ ﴿٩٤﴾

94. Na ulipoondoka msafara, baba yao alisema: Hakika mimi nasikia harufu ya Yuwsuf, ikiwa hamkunidhania nachanganyikiwa akili.

 

 

 

قَالُوا تَاللَّـهِ إِنَّكَ لَفِي ضَلَالِكَ الْقَدِيمِ ﴿٩٥﴾

95. Wakasema: Ta-Allaahi (Tunaapa kwa Allaah)! Hakika wewe bado umo katika kosa lako la zamani.

 

 

 

فَلَمَّا أَن جَاءَ الْبَشِيرُ أَلْقَاهُ عَلَىٰ وَجْهِهِ فَارْتَدَّ بَصِيرًا ۖ قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ إِنِّي أَعْلَمُ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٩٦﴾

96. Basi alipokuja mtoaji bishara (ya kuwa Yuwsuf kapatikana), aliitupa (kanzu) juu ya uso wake akarudi kuona. Akasema: Je, sikukuambieni kwamba hakika mimi najua zaidi kutoka kwa Allaah yale msiyoyajua?

 

 

 

قَالُوا يَا أَبَانَا اسْتَغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا إِنَّا كُنَّا خَاطِئِينَ ﴿٩٧﴾

97. Wakasema: Ee baba yetu! Tuombee maghfirah madhambi yetu, hakika sisi tulikuwa wakosa.

 

 

 

قَالَ سَوْفَ أَسْتَغْفِرُ لَكُمْ رَبِّي ۖ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ ﴿٩٨﴾

98. Akasema: Nitakuombeeni maghfirah kwa Rabb wangu. Hakika Yeye Ndiye Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

فَلَمَّا دَخَلُوا عَلَىٰ يُوسُفَ آوَىٰ إِلَيْهِ أَبَوَيْهِ وَقَالَ ادْخُلُوا مِصْرَ إِن شَاءَ اللَّـهُ آمِنِينَ ﴿٩٩﴾

99. Na walipoingia kwa Yuwsuf akawaweka karibu naye wazazi wake. Na akasema: Ingieni Misri In Shaa Allaah mkiwa mmo katika amani.

 

 

 

وَرَفَعَ أَبَوَيْهِ عَلَى الْعَرْشِ وَخَرُّوا لَهُ سُجَّدًا ۖ وَقَالَ يَا أَبَتِ هَـٰذَا تَأْوِيلُ رُؤْيَايَ مِن قَبْلُ قَدْ جَعَلَهَا رَبِّي حَقًّا ۖ وَقَدْ أَحْسَنَ بِي إِذْ أَخْرَجَنِي مِنَ السِّجْنِ وَجَاءَ بِكُم مِّنَ الْبَدْوِ مِن بَعْدِ أَن نَّزَغَ الشَّيْطَانُ بَيْنِي وَبَيْنَ إِخْوَتِي ۚ إِنَّ رَبِّي لَطِيفٌ لِّمَا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ هُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ ﴿١٠٠﴾

100. Akawapandisha wazazi wake wawili juu ya kiti cha ufalme, wakaporomoka wote kumsujudia.[14] Na akasema: Ee baba yangu kipenzi! Hii ni tafsiri ya njozi yangu hapo kabla, Rabb wangu Ameijaalia kweli. Na hakika Amenifanyia ihsaan Aliponitoa kutoka jela, na Akakuleteni kutoka jangwani baada ya shaytwaan kuchochea baina yangu na baina ya kaka zangu. Hakika Rabb wangu Ni Latifu kwa Atakayo. Hakika Yeye Ndiye Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

رَبِّ قَدْ آتَيْتَنِي مِنَ الْمُلْكِ وَعَلَّمْتَنِي مِن تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ ۚ فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَنتَ وَلِيِّي فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ تَوَفَّنِي مُسْلِمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ ﴿١٠١﴾

101. Rabb wangu! Kwa yakini Umenipa utawala, na Umenifunza tafsiri ya khabari (kuhusu njozi, ndoto na matukio). Muanzilishi wa mbingu na ardhi. Wewe ni Mlinzi wangu duniani na Aakhirah. Nifishe hali ya kuwa Muislamu na Unikutanishe na Swalihina.

 

 

 

ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيْكَ ۖ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ أَجْمَعُوا أَمْرَهُمْ وَهُمْ يَمْكُرُونَ ﴿١٠٢﴾

102. Hizo ni baadhi ya khabari za ghaibu Tunakufunulia Wahy kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na hukuwa pamoja nao pale walipokubaliana jambo lao, nao wakifanya njama.

 

 

 

وَمَا أَكْثَرُ النَّاسِ وَلَوْ حَرَصْتَ بِمُؤْمِنِينَ ﴿١٠٣﴾

103. Na wengi wa watu hawatoamini japokuwa utatilia hima.[15]

 

 

 

وَمَا تَسْأَلُهُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٠٤﴾

104. Na huwaombi kwa haya ujira wowote (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Hii (Qur-aan) si chochote isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu.

 

 

 

وَكَأَيِّن مِّنْ آيَةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يَمُرُّونَ عَلَيْهَا وَهُمْ عَنْهَا مُعْرِضُونَ ﴿١٠٥﴾

105. Ni Aayah (Ishara, Dalili) nyingi sana katika mbingu na ardhi wanazipitia na huku wao wanazipuuza.[16]

 

 

 

وَمَا يُؤْمِنُ أَكْثَرُهُم بِاللَّـهِ إِلَّا وَهُم مُّشْرِكُونَ ﴿١٠٦﴾

106. Na wengi kati yao hawamwamini Allaah isipokuwa wao ni wenye kufanya shirki.  

 

 

 

أَفَأَمِنُوا أَن تَأْتِيَهُمْ غَاشِيَةٌ مِّنْ عَذَابِ اللَّـهِ أَوْ تَأْتِيَهُمُ السَّاعَةُ بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿١٠٧﴾

107. Je, wanaaminisha kuwa haitowafikia Adhabu ya Allaah ifunikizayo au itawafikia Saa kwa ghafla nao hawahisi?

 

 

 

قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَسُبْحَانَ اللَّـهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٠٨﴾

108. Sema: Hii ndio njia yangu nalingania kwa Allaah, juu ya baswiyrah (nuru za ilimu na utambuzi) mimi na anayenifuata. Na Utakasifu ni wa Allaah, nami si miongoni mwa washirikina.

 

 

 

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِي إِلَيْهِم مِّنْ أَهْلِ الْقُرَىٰ ۗ أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۗ وَلَدَارُ الْآخِرَةِ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ اتَّقَوْا ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿١٠٩﴾

109. Na Hatukutuma kabla yako (Rasuli) isipokuwa wanaume Tuliowafunulia Wahy katika watu wa miji. Je, basi hawatembei katika ardhi wakatazama vipi ilikuwa hatima ya wale wa kabla yao?[17] Na bila shaka nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi kwa wale waliokuwa na taqwa. Je, basi hawatii akilini?

 

 

 

حَتَّىٰ إِذَا اسْتَيْأَسَ الرُّسُلُ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ قَدْ كُذِبُوا جَاءَهُمْ نَصْرُنَا فَنُجِّيَ مَن نَّشَاءُ ۖ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُنَا عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ ﴿١١٠﴾

110. (Wakaendelea kulingania) mpaka walipokata tamaa Rusuli, na wakawa na yakini kuwa wamekadhibishwa (hakuna tena tamaa ya watu wao kuamini), hapo ikawajia Nusra Yetu na Tukawaokoa Tuwatakao. Na Adhabu Yetu hairudishwi nyuma kwa watu wakhalifu.

 

 

 

لَقَدْ كَانَ فِي قَصَصِهِمْ عِبْرَةٌ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ۗ مَا كَانَ حَدِيثًا يُفْتَرَىٰ وَلَـٰكِن تَصْدِيقَ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ كُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿١١١﴾

111. Kwa yakini katika visa vyao kuna mazingatio (na mafunzo) kwa wenye akili. Haikuwa (Qur-aan) hadithi zinazotungwa, lakini ni sadikisho la (Vitabu) vya kabla yake na tafsili ya waziwazi ya kila kitu, na ni mwongozo na rehma kwa watu wanaoamini.

 

 

 

 

 

[1] الحروف المقطعة  (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):

 

Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة  (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).

 

[2] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Sababu ya kuteremshwa Aayah (1-3): Bonyeza kiungo kifuatacho:   

 

012-Asbaabun-Nuzuwl: Yuwsuf Aayah 1-3: نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَص

 

[3] Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام)  Ni Mtukufu Zaidi Miongoni Mwa Watu Na Amepewa Nusu Ya Ujamali Wa Dunia:

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amemsifia Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام)  kuwa ni mtu mtukufu zaidi miongoni mwa watu. Naye ni Nabiy pekee ambaye baba yake ni Nabiy naye ni Ya’quwb (عليه السّلام), na kisha babu yake Is-haaq (عليه السّلام)  ambaye pia ni Nabiy, kisha baba wa babu yake Ibraahiym (عليه السّلام)  ambaye pia ni Nabiy: 

Amesimulia Abu Hurayrah (رضي الله عنه): Baadhi ya watu walimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Nani aliye mtukufu zaidi miongoni mwa watu? Akajibu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):   "Mtukufu zaidi miongoni mwao ni yule mwenye taqwa zaidi.” Wakasema: Ee Nabiy wa Allaah! Hatuulizi hili. Akasema: "Basi mtukufu zaidi ni Yuwsuf, Nabiy wa Allaah, mwana wa Nabiy wa Allaah, mwana wa Nabiy wa Allaah, mwana wa Kipenzi cha Allaah (Nabiy Ibraahiym).”   Wakasema: Hatuulizi hili. Akasema: “Basi mnataka kuniuliza kuhusu koo asili za Waarabu?” Wakasema: Naam.  Akasema: “Wale waliokuwa bora katika zama za Ujaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Uislamu) ndio wabora katika Uislamu, kama watakuwa na ufahamu wa kina (wa Dini).” [Al-Bukhaariy]

 

Na pia: Amesimulia Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mtukufu (kati ya watu) ni mwana wa mtukufu, mwana wa mtukufu, mwana wa mtukufu; ni Yuwsuf bin Ya’quwb bin Is-haaq bin Ibraahiym (عليهم السّلام) [Al-Bukhaariy]

 

Nabiy Yuwsuf amesifika pia kwa ujamali (uzuri) kama alivyosema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth ndefu ya Israa wal-Mi’raaj: “Nikamuona Yuwsuf (عليه السّلام)  ambaye alimepwa nusu ya ujamali wa dunia.” [Muslim]

 

[4] Njozi Za Manabii Ni Wahyi Kutoka Kwa Allaah (سبحانه وتعالى):

 

Tofauti Kati Ya Ndoto Na Njozi:

 

Kwa mujibu wa Hadiyth ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), anayoyaona mwenye kulala usingizini ni matatu:

 

i- Njozi "رُؤْيَا"   . Hii aghalabu huwa inatoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى). Mtu huona njozini mambo ya kupendeza na kufurahisha, au ya kumtahadharisha na shari, au ya kumwongoza. Akiona haya, imesuniwa amhimidi Allaah (سبحانه وتعالى) na awajulishe tu jamaa zake, na si watu wengineo.

ii- Ndoto "حُلْمٌ". Hii aghalabu huwa inatokana na shaytwaan, na mtu huona usingizini mambo ya kuchukiza. Akiota hivi, basi imesuniwa ajilinde kwa Allaah kutokana na shaytwaan, atafili upande wake wa kushoto mara tatu, ageuze ubavu aliokuwa ameulalia, na aswali rakaa mbili ikiwezekana. Pia asiisimulie kwa watu.

iii- Mtu kuzungumza mwenyewe usingizini "حَدِيْثُ النَّفْسِ". Hii si njozi wala ndoto, bali hutokana na hofu au matukio yaliyoko ndani ya kumbukumbu ya mtu na kwenye akili yake ya ndani. Haya yote hujiunda wakati mtu amelala, na hata wakati mwingine husikika akizungumza peke yake yasiyofahamika.

 

Katika Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Muda utakapokuwa mfupi, njozi ya Muumini itakuwa haiongopi tena, na mwenye njozi ya kweli zaidi kati yenu ni yule aliye msema kweli zaidi, na njozi ya Muumini ni sehemu moja kati ya sehemu 46 za Unabii.  Na ndoto ni aina tatu: Njozi njema ambayo ni bishara toka kwa Allaah, na ndoto ya kuhuzunisha itokanayo na shaytwaan, na ndoto kutokana na mtu kuizungumzisha nafsi yake (mawazo yaliyotawala zaidi kwenye akili yake).” [Muslim 2263]

 

Na ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema kuwa njozi za Manabii ni Wahyi kutoka kwa Allaah [Tafsiyr Ibn Kathiyr] Ni kama vile ndoto ya Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) alipoota anamchinja mwanawe Ismaaiyl (عليه السّلام). Rejea Aw-Swaffaat (37:102). Na pia njozi ya Nabiy Muhammad  (صلى الله عليه وآله وسلم) pindi walipozuiliwa na makafiri kuingia Makkah walipofika Hudaybiyah, akaona njozini kwamba wataingia Masjid Al-Haraam Makkah kutekeleza ‘Umrah na kuwa watanyoa au kupunguza nywele zao. Rejea Al-Fat-h (48:27) na ikaja kuhakiki.

 

[5] Nyota Kumi Na Moja, Jua Na Mwezi Katika Njozi Ya Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام)

 

Wafasiri wa Qur-aan wameelezea kuwa njozi ya Nabiy Yuwsuf   (عليه السّلام) ya kusujudiwa na nyota kumi na moja, ni ndugu zake ambao walikuwa ni kumi na moja. Na jua na mwezi ni baba yake na mama yake. Imesimuliwa na Ibn ‘Abbaas, Adhw-Dhwahhaak, Qataadah, Sufyaan Ath-Thawriy na ‘Abdur-Rahmaan bin Zayd Bin Aslam. Na kwamba njozi hii imekuja kuhakiki baada ya miaka arubaini. Wengineo wamesema imehakiki baada ya miaka themanini wakati Yuwsuf alipowapandisha wazazi wake katika kiti chake cha enzi na nduguze wakiwa mbele yake. Rejea Aayah namba (100).  [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

[6] Bin-yamiyn Mdogo Wa Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام):

Bin-yamiyn ni mdogo wake Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام) ambaye ni shakiki (wa baba na mama mmoja). Ama ndugu zake wengineo, hao wamechangia, na hawa wawili kwa baba tu ambaye ni Nabiy Ya’quwb (عليه السّلام).   

 

[7] Maana Ya ‘Aziyz

 

Maana ya ‘aziyz ni kigogo au waziri. Huyo ndiye mtu aliyepewa cheo cha ‘aziyz ambaye ametajwa katika Aayah (23), (25), (30), (31), (51) na (52), na ambaye ndiye aliyemlea Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام)  nyumbani kwake baada ya kumnunua hapo alipotolewa kisimani. Kisha alipofikia umri wa kubaleghe, ndipo ikatokea mkasa wa mke wa ‘aziyz kumtongoza Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام). Hivyo basi, ‘aziyz ilitumika Misri kwa mtu mwenye cheo kikubwa ambaye hawezi kupingwa wala kuasiwa. Na pia kauli nyenginezo za ‘Ulamaa ni kwamba ‘aziyz ilitumika kwa mfalme wa Misri katika zama hizo. [Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb Juz (5) Uk. (2)]. Na kwa mujibu wa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما), ‘aziyz alikuwa ni afisa wa hazina ya kifalme. [Ibn Jariyr]. Na kauli hii ya ‘Ibn ‘Abbaas inakubalika zaidi kwa sababu Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام)  alipewa cheo hiki cha ‘aziyz pale mfalme wa Misri alipompa madaraka ya hazina za Misri. Na nduguze waliporudi tena Misri kutoka Palestina kuja kuomba chakula, wakamwita Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام)  kwa cheo hicho cha ‘aziyz kama ilivyotajwa katika Aayah: (78) (88).

 

[8] Rabbiy:

 

Katika Aayah imetajwa Rabb ambalo linatumika kwa “bwana wa nyumba au mlezi.” Na rabb imetumika tena kumaanisha “bwana wa nyumba” katika Aayah (41), (42), na (50). Basi isije kufahamika ndivyo sivyo kwamba Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام)  amemfanya ‘aziyz ambaye ni mlezi wake na bwana wa nyumba yake kuwa ni Mola au Muumba wake. Haiwezekani hivyo kwa sababu: Kwanza: Ni mustahili kwa hadhi ya Nabiy kutenda dhambi ya kumshirikisha Allaah kwa kumhusisha kiumbe kuwa sawa na Allaah. Pili: Hakuna mfano hata mmoja katika Qur-aan ambao Nabiy aliwahi kumwita yeyote asiyekuwa Allaah kuwa ni Rabb wake. Nabiy Yuwsuf mwenyewe anatofautisha kati ya ‘Aqiydah (itikadi) yake na ile ya Wamisri waliokuwa katika jela pamoja naye katika Suwrah hii ya Yuwsuf Aayah (37-40) akiweka wazi kwamba Rabb wake ni Allaah wakati wao wamewafanya wanaadam wengine kuwa Mola wao.

 

[9] Aina Tatu Za Nafsi:

 

Nafsi ziko aina tatu: (i) Nafsi yenye kuamrisha sana maovu; Rejea Yuwsuf: (12:53). (ii) Nafsi ya kulaumu; Rejea Al-Qiyaamah (75:2). (iii) Nafsi iliyotua; Rejea Al-Fajr (89:27).

 

Nafsi ya kuamrisha sana maovu ni ile ambayo inamwamrisha mtu wake kufanya inayoyopenda katika matamanio ya haramu na kufuata batili. Ama nafsi ya kulaumu, hii ni ile ambayo inamlaumu mtu wake kuhusu mambo ya kheri (na ibaada) yaliyompita (akawa hakuyatenda), hivyo basi nafsi inayajutia. Ama nafsi iliyotua, hii  ni ile ambayo imejikita na kutulia thabiti kwa Rabb wake, na katika kumtii, kufuata amri Zake na kumdhukuru, na haijatuama kwa mwingine yoyote isipokuwa Kwake tu. [Shaykh Swaalih Fawzaan Al-Fawzaan]

 

[10] Haja Katika Nafsi Ya Ya’quwb:

 

Ni huruma ndani ya nafsi yake ili wasipate jicho na husuda. [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

[11] Herufi Za Kuapia: Rejea An-Nahl (16:56).

 

[12] Hukmu Ya Mwizi Katika Dini Ya Zama Hizo: Hiyo ilikuwa ni (hukumu katika) Dini yao kwamba mwizi akithibitika kuwa ameiba, basi anakuwa anamilikiwa na mwenye mali iliyoibiwa. [Tafsiyr As-Sa’dy]

 

[13] Hila Au Mpango Wa Yuwsuf:

 

Ni mpango ambao Anauridhia Allaah (عزّ وجلّ) kutokana na hikma yake kutafuta maslahi yake. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Imaam As-Sa’diy amesema: Tulimsahilishia hila hii iliyompeleka kwenye jambo lisilokuwa la lawama. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[14] Kumsujudia Binaadam Ni Haramu Katika Sharia Yetu Ya Kiislamu:

 

Katika sharia ya zama hizo, Sujuwd iliruhusika kwa binaadam kwa kuwa ilimaanisha heshima. Na hapo wazazi wake Yuwsuf na nduguze, ambao jumla yao walikuwa kumi na moja, walimsujudia Yuwsuf kumdhihirishia heshima yao kwake. Wala haikumaanisha kuwa ni ibaada ya kunyenyekea au kuabudu. Ama katika sharia yetu imeharamishwa kwa sababu ya kuzuia kumshirikisha Allaah (عزّ وجلّ). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amethibitisha haya katika Hadiyth aliyosimulia ‘Abdullaah bin Abiy Awfaa (رضي الله عنه): Muaadh aliporudi kutoka Shaam, alimsujudia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Nabiy akasema: “Ee Mu’aadh! Imekuwaje kufanya hivyo?”  Akasema: Nimekuja kutoka Shaam, nikawakuta wanawasujudia Maaskofu na Mapadri wao, basi nafsi yangu ikapenda nikufanyie hivyo. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Usifanye hivyo! Kwani ingekuwa ni kumuamrisha mtu amsujudie asiyekuwa Allaah, basi ningeliamrisha mke amsujudie mumewe.”  [Kuna Riwaayah mbali mbali kama hiyo, na hii ni lafdhw ya Ibn Maajah (1853), na Al-Albaaniy ameisahihisha]

 

[15] Kufuata Watu Wengi Jambo La Haramu Au Batili Au La Uzushi:

 

Imaam Ibn Baaz (رحمه الله)  amesema katika nasaha zilizoelekezwa kwa Waislamu wote:  Na kila Muislamu ajitahadhari na kudanganywa na wengi, na kusema: “Watu wamefuata jambo kadha wa kadha na wamezoea jambo kadha wa kadha, basi mimi niko pamoja nao.” Huu ni msiba mkubwa, na wengi waliopita wameangamia kwa hayo. Lakini ee mwenye akili! Inakupasa ujitazame nafsi yako, na ujitathmini na ushikamane na haki hata watu wakiiacha. Na jitahadhari na yale Aliyokataza Allaah (سبحانه وتعالى) hata watu wakiyafanya, kwani ukweli ndio unaostahiki zaidi kufuatwa kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ ﴿١١٦﴾

“Na kama ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, watakupoteza Njia ya Allaah. Hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawakuwa ila wenye kubuni uongo.” [Al-An’aam (6:116] Na pia Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) kwenye Aayah hii ya Suwrat Yuwsuf (12:103)].  Na baadhi ya Salaf (رحمهم الله) wamesema: “Usiikane haki kwa sababu ni wachache wanaoifuata, na wala usidanganywe na uwongo kwa sababu ya wingi wa walioangamia.”   [Fataawaa Al-Lajnah Na Maimamu Wawili] 

 

Basi na wazingatie na watahadhari watu wanaofuata mambo na vitendo vinavyoharamishwa katika Dini ili kujiepusha na haramu na adhabu za Allaah (سبحانه وتعالى). Na pia kutahadhari na kujiepusha na mambo au vitendo ambavyo havikuthibiti katika mafundisho ya Sunnah ili kujiepusha na uzushi japokuwa watu wengi wanafuata, kwani kila uzushi ni upotofu, na kila upotofu unaelekeza motoni kama ilivyothibiti katika Hadiyth ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).

 

[16] Ishara Na Dalili Za Allaah (عزّ وجلّ) Mbinguni Na Ardhini Zinathibitisha Tawhiyd Yake:

 

Rejea Fusw-Swilat (41:53), Adh-Dhaariyaat (51:20). Rejea pia Al-Qamar (54:5) kwenye maelezo na rejea mbalimbali:

 

[17] Zingatio Kwa Makafiri Watembee Maeneo Ya Ardhi Mbalimbali Wajionee Na Watambue Hatima Za Waliokadhibisha. Rejea Aal-‘Imraan (3:137). Al-An’aam (6:11), Faatwir (35:43-44).

 

 

 

Share